Lundenga amtimua mrembo jukwaani baada ya kutinga na kivazi cha nusu uchi....

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,471
33,413
[h=3]LUNDENGA AMTIMUA MREMBO JUKWAANI BAADA YA KUTINGA NA KIVAZI CHA NUSU UCHI....[/h]MWENYEKITI wa Kamati ya Mashindano ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga Jumamosi iliyopita alimtimua mshiriki wa shindano la Redd’s Miss Morogoro 2013, Saphina Chumba (20) jukwaani wakati shindano hilo lilipokuwa likiendelea.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita katika Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Nashera mjini hapa wakati mrembo huyo alipokuwa akiwania kuvaa taji la mkoa huo.
Kisa cha mrembo huyo aliyevalia namba 5 kutimuliwa ni kukiuka maadili na kanuni za mashindano hayo kwa kuvaa nusu utupu mbele ya mgeni rasmi ambaye alikuwa Mbunge wa Kilosa, Mustapha Mkulo na mbele ya Kamati nzima ya Miss Tanzania.Baada ya kuona jinsi alivyovaa, Lundenga na kamati yake walikubaliana kumtimua mshiriki huyo kwa kumwita Jaji Mkuu wa shindano, Alex Niktasi na kumtaka amuondoe haraka.

Mbali na Chumba, pia jaji alimtimu mrembo mwingine aliyevalia namba 8, Neema Joel (20) kutokana na kushiriki shindano hilo mara mbili mwaka huu, inadaiwa mara ya kwanza alishiriki mkoani Arusha.

Lundenga alipohojiwa na mwandishi wetu alisema kamati yake inataka kuendeleza nidhamu tangu ngazi ya chini, hivyo hawawezi kuruhusu utovu wa nidhamu.LUNDENGA AMTIMUA MREMBO JUKWAANI BAADA YA KUTINGA NA KIVAZI CHA NUSU UCHI.... - MPEKUZI HURU
 
LUNDENGA AMTIMUA MREMBO JUKWAANI BAADA YA KUTINGA NA KIVAZI CHA NUSU UCHI....

MWENYEKITI wa Kamati ya Mashindano ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga Jumamosi iliyopita alimtimua mshiriki wa shindano la Redd's Miss Morogoro 2013, Saphina Chumba (20) jukwaani wakati shindano hilo lilipokuwa likiendelea.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita katika Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Nashera mjini hapa wakati mrembo huyo alipokuwa akiwania kuvaa taji la mkoa huo.
Kisa cha mrembo huyo aliyevalia namba 5 kutimuliwa ni kukiuka maadili na kanuni za mashindano hayo kwa kuvaa nusu utupu mbele ya mgeni rasmi ambaye alikuwa Mbunge wa Kilosa, Mustapha Mkulo na mbele ya Kamati nzima ya Miss Tanzania.Baada ya kuona jinsi alivyovaa, Lundenga na kamati yake walikubaliana kumtimua mshiriki huyo kwa kumwita Jaji Mkuu wa shindano, Alex Niktasi na kumtaka amuondoe haraka.

Mbali na Chumba, pia jaji alimtimu mrembo mwingine aliyevalia namba 8, Neema Joel (20) kutokana na kushiriki shindano hilo mara mbili mwaka huu, inadaiwa mara ya kwanza alishiriki mkoani Arusha.

Lundenga alipohojiwa na mwandishi wetu alisema kamati yake inataka kuendeleza nidhamu tangu ngazi ya chini, hivyo hawawezi kuruhusu utovu wa nidhamu.LUNDENGA AMTIMUA MREMBO JUKWAANI BAADA YA KUTINGA NA KIVAZI CHA NUSU UCHI.... - MPEKUZI HURU

Maji wameyavulia nguo halafu wanakataa kuyaoga, jee waliwawekea dress code kabla ya mashindano? kama hakuna basi hakuna kosa !!!
 
Mimi nashindwa kuelewa hadi leo hii umuhimu wa haya mashindani ya urembo, kwani mrembo ninani? jee kuna msichana ambae si mrembo? kama yuko jee ni haki kutafuta warembo na kuwatunukia zawadi, jee hao wanaoshinda huo urembo ni kweli ni warembo zaidi ya wengine. jee makampuni yanayofadhili urembo yanafaidika nini, na jee serikali inapata faida gani, kama hakujitokeza mtu yeyote kuangalia hao wanaoshindania urembo kutakua na athari gani??? I always ask these questions myself, you can have idea of all or some of them, naomba ufafanizi kidogo ili na mimi nishawishike kuwa mdau !!
 
Lundenga aache unafiki, kosa la kuwakaza watoto wa watu kuwadanganya eti atawapa Taji ni kubwa na baya kuliko hilo la kupanda na Gagulo fupi jukwaani, kuna mashindano flan mwaka Jana kuna Binti alizimia baada ya kushindwa alipodadavuliwa ikagundulika kuwa watu walikula Mzigo kwa Ahadi ya kumpa Taji. Wengine wanaweza kuzungumzia Maadili lakin sio huyu Fedhuli, Baradhuli, Shuwain, Afriit anaejifanya Mswati wa Tasnia ya Ulimbwende, Lundenga ndo Jaji wa Ulimbwende wa Mbunye!
 
Back
Top Bottom