Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,385
- 38,657
Miongoni mwa wana wa Afrika aliyeacha sifa yenye Kutukuka na Uzalendo usiopimika kwa nchi yake, aliyekuwa na hamu ya umajumui wa Afrika iliyopindukia mipaka, si Mwingine bali ni Patrice Lumumba. Lakini pia kwenye nchi yetu tuna mtaa ambao mambo mengi yanayoliangamiza taifa letu hupangwa kwenye mtaa huo wenye jina la mwana Afrika huyu adhimu. Hii, imekuwa ni bahati mbaya sana!!