Lumumba, Dar: Mzee Kinana na Mzee Makamba waitikia wito Kamati ya Maadili ya CCM

Fiziolojia

JF-Expert Member
Oct 19, 2019
819
1,079
Kuna habari zinazosemekana kuwa mzee Makamba na Abdulrahman Kinana (makatibu wakuu wa zamani CCM) wanaweza kuhojiwa na kamati ya maadili CCM leo hii jumatatu ya tarehe 10 February, 2020.

Hii ni baada ya wazee hao wakongwe wa chama hicho kuwachomesha mahindi wajumbe wa kamati ya maadili kwa siku mbili mfulizo (ijumaa na j'mosi) ambao walikaa kuanzia asubuhi mpaka jioni kuwasubiri bila ya mafanikio.
------------ ----------- ------------ ------------ -------

UPDATE

Makatibu wakuu wastaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Yusuf Makamba na Abdulrahaman Kinana wamefika mbele ya kamati ndogo ya Usalama na Maadili katika ofisi ndogo za CCM Lumumba Jijini, Dar

AC6B138D-1E15-409E-AA95-3C95F45D8155.jpeg

EA67DD47-FDB8-4514-9507-6A89DAD415E1.jpeg
 
CCM imekua haina maadili, umoja, maelewano. Inafanya kazi kwa "DOUBLE-STANDARD", mtu akiwa anacheo ndani ya CCM basi anapata haki zote za kisheria za KUTUKANA/KUDHARAU/KUPONDA watu, ila akishamaliza muda wake basi anageuzwa "PUNCHING BAG" la wengine kumrushia matusi na kutafutia kiki.

Wote waliokua na "VYEO" sasa hivi wajipange kisaikolojia pindi watakapomaliza muda wao.

Ama kweli mkwere mwaka 2015 umetukosea heshima sana watanzania.
 
Kuna habari zinazosemekana kuwa mzee Makamba na Abdulrahman Kinana (makatibu wakuu wa zamani CCM) wanaweza kuhojiwa na kamati ya maadili CCM leo hii jumatatu ya tarehe 10 February, 2020.

Hii ni baada ya wazee hao wakongwe wa chama hicho kuwachomesha mahindi wajumbe wa kamati ya maadili kwa siku mbili mfulizo (ijumaa na j'mosi) ambao walikaa kuanzia asubuhi mpaka jioni kuwasubiri bila ya mafanikio.
------------ ----------- ------------ ------------ ----------

Usikute bado posho zao za kikao walilipana!
 
Back
Top Bottom