Lulu Diva asema hawezi kuwa na Mwanaume asiekua na pesa

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
2,845
7,794
Msanii wa Bongo Fleva Lulu Diva amesema hajawahi kuhongwa, wala kujihusisha na kimapenzi na mtu ajipatike kipato, ila amesema hawezi kuwa na mwanaume ambaye hawezi kumuhudumia.

Lulu Diva ametoa kauli hiyo akiwa anazungumza kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV cha kila Jumatano kuanzia saa 8 : 30 Mchana, ambapo amesema tuhuma za kudanga si kweli.

"Kiukweli sijawahi kudanga, ila kuhusu gari ninayoitumia nilipewa na mpenzi wangu wakati wa birthday yangu, kwa hiyo nikipewa na mpenzi wangu siwezi kusema ni kudanga." amesema Lulu Diva

"Mimi sijawahi kudanga, ila siwezi kuwa na mwanaume ambaye hawezi kunihudumia, siwezi kuwa na Mario, mwanaume ambaye hana kazi hata nikimwambia nina tatizo hili, hawezi kunisaidia" amesema Lulu Diva

Kwa sasa Lulu Diva anatamba na ngoma ya Chekecha.

Tazama mahojiano kamili kwenye link ya Youtube hapo chini.

"Kiukweli sijawahi kudanga, ila kuhusu gari ninayoitumia nilipewa na mpenzi wangu wakati wa birthday yangu, kwa hiyo nikipewa na mpenzi wangu siwezi kusema ni kudanga."

Yaani hapa sawasawa na mtu anayesema "Mimi sipendi kula WALI ,ila napenda sana kula UBWABWA".

Kazungaka weeee mwisho wa siku karudi katika point ile ile ya mdangaji.
 
"Kiukweli sijawahi kudanga, ila kuhusu gari ninayoitumia nilipewa na mpenzi wangu wakati wa birthday yangu, kwa hiyo nikipewa na mpenzi wangu siwezi kusema ni kudanga."

Yaani hapa sawasawa na mtu anayesema "Mimi sipendi kula WALI ,ila napenda sana UBWABWA".

Kazungaka weeee mwisho wa siku karudi katika point ile ile ya mdangaji.
Unajua maana ya kudanga?
 
"Kiukweli sijawahi kudanga, ila kuhusu gari ninayoitumia nilipewa na mpenzi wangu wakati wa birthday yangu, kwa hiyo nikipewa na mpenzi wangu siwezi kusema ni kudanga."

Yaani hapa sawasawa na mtu anayesema "Mimi sipendi kula WALI ,ila napenda sana kula UBWABWA".

Kazungaka weeee mwisho wa siku karudi katika point ile ile ya mdangaji.
Hahahahaha....
Au mtu kaulizwa, nyama ya kitimoto unatumia?
Halafu ajibu, hapana kwa kweli situmii kabisa nyama ya kitimoto, ni kinyume na imani yangu ya dini, ila mchuzi aake naupenda sana.
 
Kama Aliweza Kuwa Na Ujasiri Wa Kusema Yeye Ni Under 20 Basi Hata Haya Maneno Bayana Punje Ya Ukweli
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom