Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
KITENDO cha muigizaji wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, kutoa maneno ya kumtusi mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa, ni dalili za msichana huyo kuitafuta laana.
Hivi karibuni, mama Kanumba aliliambia gazeti moja nchini kuwa tabia ya mpenzi huyo wa zamani wa mwanaye imebadilika sana na kukosa maadili, kiasi cha kumuita yeye kuwa ni kubwa jinga.
“Sielewi jambo gani limemtokea huyo binti mpaka kufikia hatua ya kuniita mimi kubwa jinga, lakini yote namwachia Mungu maana anajua anachokifanya,” alisema mama huyo huku akionekana kulengwa na machozi.
Kwa upande wake, alipoulizwa kuhusu kutoa kauli nzito kwa mama huyo, Lulu alijibu kwa nyodo na kusema hapendi kumzungumzia chochote kwani siyo staili yake kuzungumzia mambo ya wengine katika vyombo vya habari.
“Kama yeye amesema hivyo kwenye vyombo vya habari ni staili yake, mimi staili yangu ni ya kukaa kimya, sitaki kabisa kumzungumzia huyo mama,” alisema Lulu.
Naona huyu dogo umaarufu unaanza kumpa kichwa, anaanza kuvuka redline.