Lula wa Ndali ushabiki pekee hautoshi tujadili kwa hoja

Naomba niseme hivi kwamba mifano ya mapadri waliooa na kuazaa haituhusu watanzania kwa maana hao hawajachukua fom za urais wa Tanzania hapa tunamjadili Dkt Slaa ambaye bila shaka haeleweki kabisa kwa maana kama kweli hakuwa na wito angeacha tangu akiwa seminari ndogo kama nilivyofanya mimi sasa kwanini aache baada ya kupata daraja hilo?

Unajua watanzania wenzangu hili si jambo la mzaa hata kidogo ni jambo zito kwa maana kiongozi huyu hana msimamo hii ndio dhamira nayojaribu kuizungumza , naomba kwanza anayedhani nimechanganyikiwa ajue mimi ni kijana mwenye akili timamu ambaye naamini katika mapambano ya hoja na si vinginevyo.
 
Mwacheni dogo anajifunza kuandika makala, nyie si mmeona kamaliza seminari mwaka 2007? Itakuwa "O" level hiyo!! Mwacheni dogo jamani.
 
Naomba niseme hivi kwamba mifano ya mapadri waliooa na kuazaa haituhusu watanzania kwa maana hao hawajachukua fom za urais wa Tanzania hapa tunamjadili Dkt Slaa ambaye bila shaka haeleweki kabisa kwa maana kama kweli hakuwa na wito angeacha tangu akiwa seminari ndogo kama nilivyofanya mimi sasa kwanini aache baada ya kupata daraja hilo?

Hapana inatuhusu; kwa sababu ni wewe uliyeleta suala la "wito" na kutuachia taswira kwamba mtu akiwa padre basi ni lazima awe na wito hata kama matendo na maisha yake hayaakisi tena wito huo? Suala la kugombea urais halina tatizo kwani Katiba ina vigezo vichache sana vya mtu anayetakiwa kuwa Rais.

Kwa hiyo naomba utusaidie je wale wote walio mapadre sasa hivi bila kujali maisha yao na jinsi wanavyoishi wote wana wito wa upadre?

Unajua watanzania wenzangu hili si jambo la mzaa hata kidogo ni jambo zito kwa maana kiongozi huyu hana msimamo hii ndio dhamira nayojaribu kuizungumza , naomba kwanza anayedhani nimechanganyikiwa ajue mimi ni kijana mwenye akili timamu ambaye naamini katika mapambano ya hoja na si vinginevyo.
Mtu mwenye msimamo ni yupi? Ni yule ambaye ameamua kuacha upadre kwa sababu amepoteza wito au yule ambape amepoteza wito lakini bado yuko kwenye upadre? Unataka tuamini kuwa huyo wa pili ana msimamo zaidi?
 
Kinachokuponza Nova hapa ni kung'ang'ania hicho kineno "MSIMAMO" kwa maana ambayo unataka kila mtu aielewe kwa ucheche kama unavyoelewa.

Tafakari tena kuwa na msimamo maana yake nini hasa?

Je, ni kuendelea kutafuna kokoto ukidhani karanga hata kama meno yako yapukutika?
Je, ni kundelea kuimba nyimbo za uhuru hali kuwa na hakika ya kuwa unanyonywa na kukandamizwa?
Je, ni kuendelea kumtukuza Shetani hali ya kuwa umefunuliwa kwa kufanya hivyo hutaionja pepo?
Je, ni kuendelea kukumbatia jambo ambalo dhamiri yako inakataa na kwa vipimo vyote halina madhara kuachana nalo?

Nini maana ya msimamo! Ukiamini kwamba kuacha upadre ni kutokuwa na msimamo juu yako, lakini umejaribu kujiuliza kwa nini uliwekwa utaratibu wa kuacha upadre? (kwa sababu sio lazima kufa nao), ukiamini kuwa kuacha mke na kuoa mwingine ni kutokuwa na msimano shauri yako,sikuombei yakukute ya kukuta na mwandani wako kama unaye au ukiwa naye.
 
Asante sana Mzee Mwanakijiji labda nikuulize swali rahisi kwamba je kila anayekidhi matakwa ya katiba kuwa rais basi anafaa kuwa rais ?

....labda ni mantiki lakini haina mashiko (may be it is logical but not valid). Tanzania tunahitaji rais bora sio bora rais nachojaribu kufanya hapa ni kufikiri kwa mantiki kama mtu kakosa msimamo kwenye wito wake atakuwaje na msimamo kwenye mambo ya kitaifa?

Na swala la kutoorodheshea mifano mingi ya mapadri haitujengi kwa maana mjenga nchi ni mwananchi hata hoja za slaa hebu zijibiwe kwa kumwongelea slaa mwenyewe sio kuorodhesha mifano isiyokuwa na mwisho.

....tumeelewana?
 
Naona kwa leo niishie hapa acha nikaendeleze harakati mtaani wanajukwaa wenzangu tutaendelea kesho...................hoja kwa hoja hakuna jazba wala matusi.
 
Ntemi Kwizile nasikitika kuona unashindwa kujadili kwa hoja badala yake unajadili kwa jazba na ushabiki, hebu soma pia article yangu yenye kichwa cha habari what is it? Labda utanielewa mimi ni mwandishi wa namna gani?

Nachelea kusema hujanielewa sawia ndio maana umejikita kwenye kujadili udhaifu wangu bila kujadili udhaifu wa hoja zangu.


aahahh huyu jama vipi? mbona wewe unapomzungumzia Dr.Slaa unajadili UDHAIFU WAKE badala ya kujadili UDHAIFU WA HOJA ZAKE.

au mimi KILAZA sielewi kitu hapa?

MIJITU MINGINE BWANA? ushaambiwa ukitaka MAFISADI wakuone kuwa MWANAHARAKATI kama wakina NAPE na sio BAGENDA.
 
...hapa tunamjadili Dkt slaa ambaye bila shaka haeleweki kabisa kwa maana kama kweli hakuwa na wito angeacha tangu akiwa seminari ndogo kama nilivyofanya mimi sasa kwanini aache baada ya kupata daraja hilo?

Huyu jamaa bado ana matatizo, Inamaana wewe ULIYEFELI KIDATO CHA NNE ni BORA ZAIDI YA ALIYEFELI VITADO VYA JUU( tuseme masters).

Wewe si ulisema kila ngazi kuna mitihani yake na wito wake? au?
 
Naona kwa leo niishie hapa acha nikaendeleze harakati mtaani wanajukwaa wenzangu tutaendelea kesho...................hoja kwa hoja hakuna jazba wala matusi.

Kaka unachemka sasa unaanzisha mada kama hiii ukiwa internet cafe? Pole sana; wenzio wakina YAYA, MS, TanzaleOne wote wana laptop na modem wamepewa na MAFISADI na wanalipwa kwa POST, huoni watu wana wiki tu POST 300, yani ni mwendo wa posti kama 50 kwa siku wewe unakaribia mwaka unapost 10 tu.

Pole sana unajinyima Elfu moja yako kwa kwenda cafe wakati ungeweza kwenda kununua MATUNDA yaka kusaidia kulinda mwili.

YAYA and Co. please do something mwenzenu huyu msaidiieni hata SIMU YA MCHINA na salie angalau ata Bundle ya mwezi mmoja huu najua ata 15,000/= itamtosha.
 
Mods.........Hii 'sredi' haina mashiko,nashauri iondolewe ati...

Nilitegemea majibu ya huyu Mseminari mwenzangu(yeye ni junior Seminarist from St.Mary's Visiga seminary....) angekuja na majibu(hoja) zitakazotufanya wasomaji tuone ni jinsi gani Lula alivyo na ushabiki...Binafsi niliisoma hoja ya Lula na kuielewa vizuri hasa(haihitaji viboko kuielewa makala ile ya Lula).......Sasa huyu Mfolo(ni lugha ya tuliyoitumia Kaengesa seminary kwa waseminari waliokuwa madarasa ya chini hasa wa O-level kama huyu) yeye kaja na hoja ambazo zimeelekeza zaidi kumshambulia Dk.Slaa badala ya kueleza tatizo/kasoro za hoja za Lula........

Slaa hajafanya kosa kugombea urais na hata upadre wenyewe aliuacha kwa kufuata taratibu/kanuni zote za kanisa na akaruhusiwa kuacha ikiwa ni pamoja na kupata ruhusa ya kuoa(akitaka)..........Ishu ya Slaa ni tofauti na ile ya mapadre wengine(baadhi yao wanajulikana hata ndani ya Tanzania-waTanzania) ambao ama wameachishwa ama wamefukuzwa katika upadre na kutengwa na kanisa.......

Nova........kuna njia nyingi za kujifunza kuandika makala na kuwa maarufu badala ya 'kutoka' kwa kumjibu Lula............Ubarikiwe sana
 
Asante sana Mzee Mwanakijiji labda nikuulize swali rahisi kwamba je kila anayekidhi matakwa ya katiba kuwa rais basi anafaa kuwa rais?

Kama anatimiza vigezo vya Kikatiba ya Tanzania kuhusu Urais basi anayo haki ya kugombea Urais. Kwamba anafaa ni uamuzi wa wapiga kura baada ya kusikiliza hoja na ajenda yake na kumpima kwa vigezo vya kisheria vilivyowekwa.

........labda ni mantiki lakini haina mashiko(may be it is logical but not valid). Tanzania tunahitaji rais bora sio bora rais nachojaribu kufanya hapa ni kufikiri kwa mantiki kama mtu kakosa msimamo kwenye wito wake atakuwaje na msimamo kwenye mambo ya kitaifa?
Hapa ndiyo tatizo lako... mtu mwenye msimamo ni yupi kati ya hawa wawili?

a. Yule ambaye haaimini katika tunu za upadre (kama useja, mafundisho ya kanisa n.k) na anaendelea kuwa padre huku akiwa na mabinti pembeni, akichota fedha za Parokia na kusupport familia yake?

b. Yule ambaye ameona kuwa hawezi kuwa padre na akafuata utaratibu uliowekwa na Kanisa kuacha upadre, na Kanisa likamruhusu atoke na kumrudisha kwenye ulei?

Nikikusikiliza unasema mwenye msimamo ni yule ambaye ameendelea kuwa padre lakini akiishi maisha yasiyoendana na wito wake huo. Lakini anayeacha ili asiwe mnafiki kwako wewe unaona kuwa huyo hana msimamo sivyo?

na swala la kutoorodheshea mifano mingi ya mapadri haitujengi kwa maana mjenga nchi ni mwananchi hata hoja za slaa hebu zijibiwe kwa kumwongelea slaa mwenyewe sio kuorodhesha mifano isiyokuwa na mwisho..............tumeelewana?
Hatujaelewana! Kwanza kwa sababu mnataka tuamini kuwa uamuzi wa Slaa kuacha Upadre na kuingia kwenye siasa kuwa ni jambo la ajabu sana; na siyo hivyo tu unataka tuamini kuwa mtu kuacha upadre na kutaka urais wa nchi yake ni jambo ambalo halijawahi kutokea. Tumeweza kuonesha kuwa Slaa siyo Mkatoliki wa kwanza kuacha upadre na kutaka kuwa Rais wa nchi. Sasa hii inaitwa ni precedence. Jaribio la kutaka watu waangalie mambo nje ya maudhui kana kwamba ni isolated incidence haliwezi kufanikiwa.

Kwa hiyo kwanza tunatakiwa kukubaliana mambo kadhaa:

a. Siyo ajabu kwa padre wa Kikatoliki kuacha Upadre na kuingia maisha ya Ulei akifuata taratibu zilizowekwa, - hili ni kweli.
b. Siyo ajabu kwa aliyeacha kuwa padre kwa misingi ya a. kuamua kuingia katika fani nyingine ya kazi huku akiendelea kuwa mkatoliki - hili ni kweli.
c. Siyo ajabu kwa mkatoliki mlei (aliyewahi kuwa padre) kuamua kugombea nafasi ya uongozi wa kisiasa - hili ni kweli
d. Siyo ajabu kwa Mkatoliki Mlei (aliyewahi kuwa padre) kuamua kugombea nafasi ya Urais wa nchi yake - hili ni kweli
e. Siyo ajabu kwa Mkatoliki Mlei (aliyewahi kuwa padre) kushinda nafasi ya Urais wa nchi yake - hili ni kweli

Sasa kama a - e ni kweli kama nilivyoonesha na kuwa Dr. Slaa aliwahi kuwa padre, akaacha nafasi ya upadre na kuingia katika maisha ya ulei na kutimiza masharti yote ya Kikatiba kwanini asipewe nafasi ya kugombea?
 
HUYU KIJANA NASHANGAA KWA NINI HAKUPUUZWA MAANA DAWA YA MPUUZI NI KUPUUZWA.
ILA KWA KUWA NIMEONA WAKONGWE WANAENDA NAYE SAMBAMBA NIMEONA NA MIMI NIJITOSE INAONEKANA MAY BE UPUUZI WAKE UNA MADHARA UKIPUUZWA.

Ndugu Novatus

Ukisoma body yako inaonyesha kuwa una portray kuwa Slaa hafai ,watu wanaposoma wanakujibu kutokana na maudhui yaliyo kwenye body wewe unakwepa na kusema hamnielewi soma kichwa,I tell you what !mimi ningekuwa nimesoma hivyo habari na kisha nikaambiwa niseme kicha cha habari hii kiwe vipi hakika ulichoweka kingekuwa cha tano chini ingawa una mjibu LULA.

Platform ya habari yako ni very weak kama unasoma biblia vema tusoma Mtume Paul anasema angeshauri watu wawe waseja(bachelor) kama yeye ila kuliko kuwaka tamaa ni bora mtu akaoa ,mtu aliyefata ushauri wa Paul na kufata taratibu zote za kanisa lenu(umesema ni mseminary) leo unamwita hana msimamo.

Hoja yako kuwa rais anatakiwa kuwa na msimamo ni sahihi sana ila ulipotohoa kuwa Slaa hana msimamo ndio tatizo is logical irrelevant otherwise you should come with statistics za watu walio acha upadre walikuwa ni watu wasio na msimamo this is how researcher/writer come to conclusion.Lakini ww hapa unagoma kuwa sifa za mtu kama yeye hazitokani na kumfananisha na watu kama yeye quote

" uimara wa Dk. Slaa kamwehauletwi na mifano ya watu ambao waliwahi kuwa mapadre na mwishowe kuukwaa urais, hapa nakusudia kusema kuwa hoja hizi kumhusu Dk. Slaa hazikupaswa kujibiwa kwa orodha ya mifano ya mapadre waliowahi kuwaniaurais au kuupata urais mifano hiyo ni pamoja na padre Edd Panlilio waUfilipino au Askofu Ferdando Lugo wa San Pedro Paraguay".

Kwanza kabisa ktk kujibu hoja zako najibu ktk msingi ya nani anafaa kuwa rais kama Slaa hafai kutokana na sababu ulizosema.

Sababu ya kufanya hivyo ni kutokana na wanasiasa maarufu walivyowahi kusema na pia jinsi ambavyo inaweza kusound logical to most of us.

Walisema hivi "Don't compare me to God compare me to alternative"

So hapa unaona watu wengi wanaona kuwa wewe una "suggest" Slaa hafai uki compare na his alternative (JK,.....) Kitu kinachoonekana ni wrong, tuna mifano dhahiri JK HAS PROVED FAILURE na kuna mifano dhahiri wa utendaji wa Slaa kuwa ni mwenye msimami in contrast to what your trying to portray.

Unataka kum-compare Slaa na God as if he is that perfect hutaki kum compare na alternatives, na ukiwa tayari kumu compare na his alternatives then we 'll go through their personal life but that is the last thing we should do.

The main issue here ni kuweka sifa za viongozi wanazotakiwa kuwa nazo na kuwavisha kila mmoja.
 
" uimara wa Dk. Slaa kamwehauletwi na mifano ya watu ambao waliwahi kuwa mapadre na mwishowekuukwaa urais, hapa nakusudia kusema kuwa hoja hizi kumhusu Dk. Slaahazikupaswa kujibiwa kwa orodha ya mifano ya mapadre waliowahi kuwaniaurais au kuupata urais mifano hiyo ni pamoja na padre Edd Panlilio waUfilipino au Askofu Ferdando Lugo wa San Pedro Paraguay".

I love this kind of arguments! Kuna watu wanakuja na upupu hapa nashindwa jua kama brain zao ziko kichwani ama ziko kwenye inguinal canal. Nimejifunza kitu asante mkuu MUTU! This is what we should get from great thinkers si hawa jamaa wa mahoka.

Mfano mwingine, Jean-Bertrand Aristide is a Haitian politician and former priest who served as Haiti's first democratically elected president. Dr Slaa hatakuwa rais wa kwanza kutokea kwenye utawa.

http://en.wikipedia.org/wiki/Jean-Bertrand_Aristide
 
Kichefu chefu cha aina yake.

Muulize Godfather wa Slaa na Pope. Tunaangalia maisha ya kisiasa ya mafanikio ya Dr. Slaa. Hivi Papa anapo-apologise kwa ufuska wa mapadre wake uingereza unataka apanue apology kwa slaa kuacha upadre? Ok ukishashindwa upadre je umeshindwa kila kitu?

NDIYO MAANA UNAJIHIDI KUCHAFUA DR. KWA SABABU UNAKUBALI KUSHINDWA. Hapa siyo recruitment arena ya mapdre hapa ni issues (masuala) za kitaifa.
 
Sasa mbona tunashindwa kuelewana kitu rahisi tu? Hata mtoto wa darasa la kwanza anaelewa.

.....sasa kama Dkt Slaa amekosa msimamo kwenye maisha yake binafsi atawezaje kuwa na msimamo kwenye mambo ya kitaifa?

Kashindwa maisha yake mwenyewe atawezaje maisha ya watanzania milioni arobaini? Au ndio kusema kama padri kashindwa kuongoza parokia yenye waumini wachache akipewa uaskofu kuongoza jimbo zima ataweza?

Naona hapa ndio unapojichanganya. Amekuambia nani kuwa Dr.Slaa alishindwa kuongoza parokia fulani. Kwa taarifa yako Dr. Slaa alikuwa na nafasi kubwa katika kanisa hadi alipoacha. Dr. aligundua wito mwingine katika maisha yake, akaamua kuufuata na huo ndio ushujaa.

Wewe ulishindwa nini ulipoacha kufuata upadre baada ya kidato cha sita. Naamini uligundua wito mwingine ukaufuata, vinginevyo ulikuwa mwizi wa elimu ulijipenyeza katika seminari ukijinafikisha kumbe hata wito huo hukuwa nao tangu mwanzo.

Tatizo lako ni utoto wa hoja unakusumbua. Unadhani tupo kwenye debate ya sekondari? Jadili hoja ya maana kwa manufaa ya nchi kuliko kupoteza muda wa wengine kwa hoja za kitoto.
 
Kambota,

Anza kujadili maisha ya kila aliyewahi kuiongoza nchi yetu. Dr. Slaa ni mwanadamu na hakuna binadamu aliye kamili. Roman Catholic ni dini ambayo ililetwa na mwanadamu na kati ya hao wanadamu walikuwepo wenye mapungufu sasa iweje leo ajabu kwa Dr. Slaa kuuacha upadre uwe ni udhaifu wa kushindwa kuliongoza taifa.

Hata wewe uliyesomea huo upadre una mapungufu. Wewe ndio usipende kuwapotosha wananchi kwa uchambuzi wako hafifu na roho ya kwa nini?? Kwani una ulazima wa kumpigia kura Dr.Slaa mpigie yule wewe unaona atakufaa.

Otherwise tafuta hoja nyingine ya msingi tujadili sio Dr. Slaa kaacha upadre(kwani upadre ndio nini??) mara kaacha mke (so what) wangapi wameacha na kuoa na kuacha na kuoa na kuwa na vimada hapa na pale. Acha kutupotezea muda na agenda zako za kuota.
 
Back
Top Bottom