Lula wa Ndali ushabiki pekee hautoshi tujadili kwa hoja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lula wa Ndali ushabiki pekee hautoshi tujadili kwa hoja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nova Kambota, Sep 20, 2010.

 1. Nova Kambota

  Nova Kambota Member

  #1
  Sep 20, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  LULA AMEPOTOSHA HOJA ZINAZOMHUSU DK. SLAA

  Novatus .S. kambota

  Leo nimejitokeza kwenye gazeti hili la Raia Mwema ili kujibu makala ya mwandishi Lula wa Ndali Mwananzela kwenye toleo namba 149 la septemba 1 mwaka 2010.

  Kuna sababu kuu nne zilzonisukuma kujibu makala ile iliyokuwa na kichwa cha habari kwanini hoja ya upadre wa Dk. Slaa haina msingi, sababu hizo ni kama ifuatavyo ; kwanza nimeamua kujibu kwa sababu na amini kuwa Raia Mwema ni gazeti huru lisilo na upendeleo kwa yeyote hivyo basi ni matumaini yangu kuwa makala hi itachapwa kama ilivyo bila kupindishwa hata kidogo, pili ni kumkosoa Lula ambaye kwenye makala yake ile alishindwa kuchambua hoja za msingi zinazomhusu Dk. Slaa na badala yake alifanya usanii wa kuzungukazunguka hoja za msingi bila kuzama ndani ya hoja hizo, tatu ni kuzichambua hoja hizo bila kifcho ili watu waweze kumwelewa kiundani Dk. Slaa na nne ni kutoa angalizo kwa waandishi wengine kuwa si vema kufanya usanii kwa kutumia taaluma yao bali wanapaswa wawe wakweli na wasiwe wapiga debe wa wanasiasa.

  Sasa nizame kwenye hoja zenyewe ambazo watu wanapaswa kuzielewa kiundani, hoja kuu hapa ni safari ya kisiasa ya Dk. Slaa yenye kila aina ya utata na alama nyingi za kuuuliza, safari hiyo ni ile ya kutoka kwenye kuta za seminari, altare ya Bwana, upadre, katibu wa baraza la maaskofu , ubunge wa karatu mpaka sasa anapowania urais kwa tiketi ya CHADEMA.

  Naomba nitoe mifano halisi
  ili nieleweke, kwanza mimi mwenyewe nimesoma seminari ndogo ya Mtakatifu Maria visiga ya jimbo kuu la Dar es salaam kwa miaka minne (2004-2007).

  Nilipokuwa seminarini hapo kwa kawaida walezi wetu walikuwa kila mmoja wetu iwapo kweli ana wito wa upadre au la, na iwapo ilibainika kwa hukuwa au matendo hayaendani na wito huo mtakatifu hakukuwa na subira isipokuwa kuondolewa seminarini sio hivyo tu ulipofika mda wa kuhitimu kidato cha nne kwa kawaida kulikuwa fomu maalumu za kujaza iwapo kweli unawito wa upadre au hapana na ili swala hilo lifanyike kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kulikuwa na sala maalumu iliyoongozwa na baba wa kiroho (spiritual father) kwaajili ya kumwomba Mungu ili amjalie kila mmoja wetu kutambua wito wake na hivyo kujaza fomu hizo kwa umakini na muongozo wa Roho Mtakatifu na ni matumaini yangu kuwa hata wakati wa kuhitimu kidato cha sita utaratibu ni huohuo na hata baada ya kuwa frateri na shemasi kuelekea upadre fomula ni hiyohiyo ya kumwomba Roho Mtakatifu akusaidie (mseminari) kutambua wito wako.

  Sasa kwa mazingira haya sijui Lula ana la kujibu kuhusu Dk. Slaa? Kwa maana Dk. Slaa alipitia hatua hizi na kote huko aliongozwa na Roho Mtakatifu kufanya uamuzi wake na mpaka akafikia kwenye sakramenti takatifu (isiyofutika) ya upadre. Sasa kinachotutatiza wengi ni swala la Dk. Slaa kutoka kwenye wito wake wa upadre na kuingia kwenye siasa, hapa kuna maswali kadhaa ya msingi ya kujiuliza ; kwanza kwa kuacha upadre Dk. Slaa anataka kutudhihirishia kuwa alipokuwa seminari alikuwa bendera fata upepo? Mpaka akajikuta ameangukia kwenye upadre pasipo kuwa na wito huo? Au labda Dk. Slaa alidanganywa na Roho Mtakatifu na kujikuta amekuwa padre bila kupenda? Au Dk. Slaa ni mtu wa namna gani basi?

  Kama ni kweli Dk. Slaa ni bendera fata upepo basi ni mtu hatari kwa maana kwa uelewa wa kawaida tu raisi mfata upepo hafai kwa maana si ajabu akiwa rais
  anaweza kufanya maamuzi kwa kufata upepo na bila shaka ameshaonyesha mwenendo wake huo wa kufata mkumbo, kwa maneno yake mwenyewe Dk. Slaa amesema kuwa hakuwa na lengo la kuwania urais na kwamba alishachukua fomu ya kuwania ubunge wa karatu na ghafla kabadili mawazo na kuingia kwenye kinyang’anyiro cha urais kwa kushawishiwa tu na wanachama wa CHADEMA , hii kweli ni ajabu na bila shaka inadhihirisha tabia ya kufata mkumbo ya Dk. Slaa.

  Na iwapo alidanganywa na Roho Mtakatifu basi ni mwongo au sio msikivu kwa maana Roho Mtakatifu kamwe hawezi kuwa mwongo, pengine wakati Roho Mtakatifu alimfunulia Dk. Slaa kuwa upadre haukuwa wito wake yeye hakuwa msikivu alikuwa mkadi na hivyo aling’ang’ania na baadae upadre ukamshinda na ule methali maarufu ya asiyesikia la mkuu……..huvunjika guu imemtokea Dk. Slaa.

  Sasa Lula ilibidi ajibu hoja hizi na sio kujikanyaga kanyaga kwenye makala yake ile ambayo kimsingi haikulenga kuchambua kwa mantiki hoja hizi badala yake ilikuwa makala ya kisiasa iliyolenga kumpigia debe Dk. Slaa, kwa kweli sikutegemea na kamwe sitaki kuamini kuwa makala ile iliandikwa na mwandishi wa viwango vya Lula labda siye yeye, pengine labda Lula alikuwa hayupo kwenye hali yake ya kawaida alikuwa anaumwa ladda kwa maana nilitegemea makala ile iandikwe na mkurugenzi wa propaganda wa CHADEMA (kama yupo) na sio mwandishi wa ubora wa Lula.

  Lula alipaswa ajibu hoja za msingi kama vile kwa nini Dk. Slaa hana msimamo? Na je tukimpa urais hatokuwa na maamuzi legelege ya kufata mkumbo? Au hataendeleza tabia yake ya kutokuwa msikivu au mkaidi? Lula anapaswa ajue kuwa kuhoji maswali haya sio kumpinga Dk. Slaa bali kiu ya kujiridhisha kwa maana uraisi sio lele mama . Tunahitaji mtu makini ambaye ana utashi mkubwa wa kisiasa na mwenye kufikiri kwa mantiki na kuamua kwa hoja nzito na zenye mashiko na sio maamuzi legelege ya kufata mkumbo.

  Lula alipaswa aende mbali zaidi kwa kuhusanisha hulka ya Dk. Slaa kutokuwa na msimamo na swala la padre huyo kuvunja viapo vyake vya upadre iwe kwa ruhusa ya Vatican au la? Kwanini Dk. Slaa ameoa na ana watoto wawili kinyume na maadili ya wito wake ambao yeye mwenyewe aliukubali pasipo kulazimishwa? Je yeye ni mwasi? Na je iwapo atabahatika kuingia kwenye kuta za magogoni hataasi kwa maana ya kutofata katiba ipasavyo kama alivyoasi kwenye kanisa katoliki?

  Haya ni maswali ambayo Lula alipaswa kuyajibu kwa hoja moja baada ya lingine.

  Kwa faida ya wasomaji wake Lula alipaswa kulitazama kiundani swala la hivi karibuni la Dk. Slaa kuachana na mkewe na kuoa mke mwingine, je lina uhusano na hulka yake ya kufata mkumbo au kufanya maamuzi legelege, je mwanzoni alifata mkumbo kumwoa mke wa kwanza na sasa amebadili uamuzi?

  Pengine hapa mtu anaweza kuja na hoja kuwa Dk. Slaa ni mtu makini ambaye anajirekebisha haraka na kuchukua hatua au kwanini hoja za udhaifu wa Dk. Slaa zinajitokeza sasa hivi? Kwanini hazikuwepo alipokuwa mbunge wa karatu?. Labda nitoe angalizo kuwa hata kama Dk. Slaa ana tabia ya kujirekebisha haraka bado hafai kwa maana kuwa rais wa nchi sio sawa na kuwa class-monitor kwa maana kama Dk. Slaa ni mtu wa namna hiyo basi tujiandae na rais mkoseaji kila siku na wapiga kura wa Tanzania wajue kwamba nchi inahitaji maamuzi makini na sio kukoseakosea kwa maana kuna mambo mengine ambayo yakikosewa hata mara moja tu basi ni angamizo la taifa zima (one mistake one goal).

  Pili Lula inabidi atambue kuwa kuna kila sababu ya kuhoji uimara wa Dk. Slaa na vilevile ni haki kabisa hoja hizi kuibuka wakati huu kwa maana raisi ni kiongozi mkuu wa nchi tofauti na mbunge ambaye ni mwakilishi wa jimbo lake (na hapa naomba nisieleweke vibaya kuwa natetea wabunge legelege), raisi akiboronga athari zake ni kubwa (tramendous effects) na zina uzito mkubwa sana tofauti na mbunge
  akiboronga ingawaje kuboronga ni kuboronga na dhambi ni dhambi tu.

  Lula inapaswa atambue kuwa Dk. Slaa hivi sasa anawahusu watanzania wote na sio wana karatu pekee hivyo tuna kila sababu ya kujiridhisha naye na anapaswa atoe ufafanuzi wa kina ili aeleweke na umma wa watanzania na sio kutoa majibu mepesi mepesi kwa hoja nzito kama alivyofanya Lula kwenye makala yake.

  Mwishowe Lula anapaswa atambue kuwa uimara wa Dk. Slaa kamwe hauletwi na mifano ya watu ambao waliwahi kuwa mapadre na mwishowe kuukwaa urais, hapa nakusudia kusema kuwa hoja hizi kumhusu Dk. Slaa hazikupaswa kujibiwa kwa orodha ya mifano ya mapadre waliowahi kuwania urais au kuupata urais mifano hiyo ni pamoja na padre Edd Panlilio wa Ufilipino au Askofu Ferdando Lugo wa San Pedro Paraguay. Orodha hii aliyoitoa Lula haina maana yoyote na wala haitoi ufumbuzi kwa hoja na maswali yenye utata yanayomuhusu Dk. Slaa bali Lula anapaswa azijibu hoja hizi nzito na kuzitolea ufafanuzi wa kina ambao utaeleweka kwa wapiga kura wote wa Tanzania.  Mwandishi wa makala hii anajulikana kama Novatus .S. Kambota (Mwanamapinduzi), yeye ni msomaji wa Raia Mwema pia ni mhitimu wa kidato cha sita wa sekondari ya Ilboru, kwa hivi sasa nimwanaharakati wa mazingira wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Jitume Environmental Society (JES) ya Kiwalani Dar es salaam na vilevile ni mwanachama wa mtandao wa kijamii unojihusisha na uchambuzi wa maswala mbalimbali ya kisiasa unaojulikana kama Taifa Huru Tanzania.

  Anapatikana kwa namba 0717-709618 au 0783-610926 au waweza kumwandikia kwa anwani ya barua pepe ; novakambota@gmail.com
   
 2. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwanza, Nova kambota Umejieleza na unaeleweka. Tatizo nililoliona umetumia nguvu nyingi kukosoa hoja za Lula badala ya kuelekeza hoja zako kwa Dr. Slaa mwenyewe. Kwa bahati Dr. Slaa huwa hujibu hoja za aina yako na waliotaka kuwelewa wamemwelewa. Tafadhali umwulize mwenyewe atakujibu.

  Pili, hata hivyo ninaona una mahangaiko mengi na maisha binafsi ya Dr. Slaa, lakini ninashindwa kukuelewa kama una msimamo kama huo kwa viongozi wengine wanaoongoza taifa hili au waliowahi kuongoza.

  Tatu, kwa utambulisho wako mdogo ulioueleza (rejea nukuu hapo juu) tunapata picha kwamba uliwahi kusoma Seminari. Ninavyofahahamu maana yake ni kuwa ulitaka kuwa padre, kwanini hukueleza zaidi kama uliacha mwenyewe au ulifukuzwa? Je, kutokuendelea na Seminari tuitafsiri kuwa ulikosa msimamo? Endapo uliacha mwenyewe, utakapoombwa siku moja kuwa ugombee utakataa na kujieleza kuwa wewe ni mtu asiye na msimamo?

  Mwisho, Lula alitoa maoni yake na wewe umetoa ya kwako na yote tunayapokea. Lula alimtetea Dr. Slaa (kwa mtazamo wako) na wewe tumekusikia. Hoja zako ni kuwa Dr. Slaa hana msimamo hivyo hafai kuongoza nchi. Huo ni upotoshaji wa hali ya juu. Nadhani kama unafuatilia siasa ya nchi hii yeye ndiye mzalendo pekee anayeonekana kuipenda nchi hii. Umeshindwa kutueleza wenye msimamo ni wepi badala yake unataka tu kutuaminisha kwa maelezo yako mengi kuhusu maisha binafsi ya Dr. Slaa. Achana na hoja hafifu ambazo bila shaka umetumwa kuja kuzieleza hapa.
   
 3. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,190
  Likes Received: 996
  Trophy Points: 280
  Mwandishi ni mtu anaeisaka ajira, na vyama visivyo vya kiserikali anavyojinadi kuvifanyia kazi nina uhakika vikichunguzwa vitakuwa vina mkono wa serikali ya kifisadi ya ccm.

  Kawaida ya tabia ya wanaharakati wengi ni kutetea maslahi ya wanyonge yaliyosahauliwa na serikali iliyo madarakani. Sasa mwandishi kapotea njia amejipanga kutetea maslahi ya wachecha wanaowanyonya wengi tena wanyonge.

  Nikirudi katika hoja ya mwandishi, nakiri kwamba sikufanikiwa kusoma makala ya Lula ila tu niseme kilicho katika hii makala ya kumjibu lula ni malalamishi yasiyo na nguvu zozote kihoja.

  Mfano mwandishi anatakiwa kufahamu kuwa Dr Slaa hajazuka tu katika taifa hili bali ni mtu aliyejijengea umaarufu akiwa bungeni kwa hoja zake nzito za kutetea maslahi ya umma. Ukizingatia kwamba bungeni ni mahali ambapo kwa kila utachozungumza kinatakiwa ushahidi kwani kinawekwa kwenye kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

  Slaa alitoa hoja zilizoweza kuiangusha serikali bungeni na imewekwa kama kumbukumbu. JK nae kajitutumua kutoa hutuba bungeni lakini ilipotakiwa kujadiliwa na wabunge, serikali haikukubali maana walijua wazi jinsi ile hotuba isivyokuwa sahihi na ilivyopotosha ukweli.

  Hoja kama zile zinatakiwa kwenye majukwaa ya kisiasa kusiko na kuhoji ila kuitikia ndio mzee. Ndio maana unaona hata sasa jk hathubutu kuweka mdahalo maana anajifahamu ni mweupe. Hivyo kumlinganisha jk na slaa ni makosa.

  Kuhusu upadre na siasa, unapaswa kufahamu hata papa mwenyewe ni mwanasiasa kwani ni kiongozi wa dola la vatican lenye mabalozi wa kisiasa duniani kote na hata mwakilishi wa kisiasa katika umoja wa mataifa. Hivyo jua wazi kwamba kuna mafungamano kati ya kanisa la RC na siasa zinazoitawala dunia. Kinachotakiwa ni kujiweka wazi tu kama alivyofanya Dr Slaa.

  Kwa habari ya kuoa hivi ukishajiweka wazi na kuruhusiwa na kanisa kuishi maisha ya kilei kuna nini kinakufunga usioe? Slaa kama binadamu mwingine ana haki ya kuoa na ndio maana ametangaza uchumba hadharani na kama kutakuwa na pingamizi kama lilivyojitokeza basi zitaangaliwa njia zinazokubalika.

  Mwandishi atanificha ila tu nilitaka nimuulize ni wanawake wangapi ametembea nao huku nafsini mwake akijua kwamba hatawaoa? Haiyamkini ni wengi. Sasa huo ni udhaifu wa maisha ya kibinafsi ambayo watu wote wanayo. Anaesema kwamba hakuwahi kupatikana na kosa na awe wa kwanza kujitokeza hadharani na tuuone ushuhuda utakaokuja nyum yake.

  Kile kipaji kilichoonekana kwa Slaa ndicho kinachoshawishi watu kumuunga mkono kwani ameubeba ukomboziTZ
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  Sep 20, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Njaaa inakusumbua, kwa taarifa yako ukitaka kupata kacheo CCM kuwa na msimamo usiyo yumba watakununua kwa pesa nyingi ama watakuhonga kacheo kama Nape Nnauye, ukiwa mpiga makofi , mtu legelege kama alivyo mwandishi aaah wapi, nani atakuona, endelea kuandika kwa kudhani kama kuna kamkate katakuangukia, kina Prince Bagenda wanawalamba miguu waheshimiwa miaka nenda rudi, sasa miaka15, lakini waaapi, watu hawamuoni.
   
 5. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mimi ni msomaji mzuri wa makala za Lula na niliisoma makala ile kwa makini, nasikitika kusema kuwa watu wasioitakia nchi hii mema (akiwemo Novatus L Kambota) wanajaribu kila linalowezekana kutuaminisha kuwa Dr Slaa hafai kuaminiwa kwa sababu ameoa mke wa mtu, walipoona upepo ni mgumu kutumia hoja hii wanaanza kutuletea hoja zisizo na mashiko kama suala la upadre wake, na kwa sababu wanajua kuwa watu wengi hawasomi magazeti yao (ya New Habari Corporation) sasa wanaanza kujipenyeza kwenye magazeti pendwa na hoja zao dhaifu.

  Kama kweli Kambota ana weledi anaojaribu kutuaminisha kupitia makala yake, naamini asingepoteza muda wake kuwashawishi watanzania watafute mgombea mwingine wa kumpatia kura zao kwa sababu ni yeye pekee kati ya wale walioomba ridhaa ya kuichukua nafasi hiyo ndiye alionyesha kwa vitendo kupigania masilahi na heshima yetu kama watanzania.

  Amepigania kuhakikisha kuwa wote wanaodhuluma rasilimali za Tanzania wanajulikana (hata kama kufanya hivyo ni kuhatarisha uhai wake), ameonyesha uwajibikaji kwa kusimama kidete kutetea wanyonge bila kuchoka na ni yeye pekee aliyeombwa na wenzake kuwa agombee. Wengine wote akiwemo Kikwete wanalilia kuingia na kubaki ikulu kwa gharama zozote, kama ambavyo alituasa Nyerere kuwa Ikulu ni mzigo na yeyote anayepakimbilia anafaa kuogopwa kama ukimwi (JK ameituma familia yake yote kuzunguka nchi zima kuwalaghai watanzai ili aendelee kutuibia).
   
 6. Nova Kambota

  Nova Kambota Member

  #6
  Sep 20, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bila shaka sijaeleweka kwa maana walionijibu wamejadili udhaifu wangu mtoa hoja hawajajadili udhaifu wa hoja zangu , wameniita mpotoshaji bila kuonyesha kwa kiasi gani hoja zangu zinapotosha.

  Haitoshi wamenihusisha na CCM sasa hapa ndio nacheka sana kwani kuhoji mambo ya Dkt slaa ni lazima uwe CCM? Au ndio tuseme waandishi wanadhani kupingana na CCM ndio uzalendo au uanaharakati?

  Sasa naanza kuamini kuwa sio kila anayeandika huwa ana hoja wengine ni wadandia hoja.
   
 7. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #7
  Sep 20, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  KUPINGA ccm Ndio kuwa mwanaharakati, sasa ukiwa pamoja na majangili utawezaje kufanya harakati zako, kwanza wao hawataki wanaharakati katika chama chao.

  Mwanaharakati CCM ni Makamba na Tambwe Hiza pekee, wengine woote njaa tu.
   
 8. Nova Kambota

  Nova Kambota Member

  #8
  Sep 20, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ntemi Kwizile nasikitika kuona unashindwa kujadili kwa hoja badala yake unajadili kwa jazba na ushabiki, hebu soma pia article yangu yenye kichwa cha habari what is it? Labda utanielewa mimi ni mwandishi wa namna gani?

  Nachelea kusema hujanielewa sawia ndio maana umejikita kwenye kujadili udhaifu wangu bila kujadili udhaifu wa hoja zangu.
   
 9. S

  Safre JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2010
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 240
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mmmh kazi ipo mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe
   
 10. Nova Kambota

  Nova Kambota Member

  #10
  Sep 20, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nguvumali naona jaribu kuchimba hoja usidandie mistari mifupi fupi? Unadhani kwa mapadri wa Ireland walinajisi watoto basi kila mkatoliki ni mnajisi? Kama siyo kwanini unaita CCM majangili?

  ....tujadili kwa hoja sio jazba Jamii Forums ni jukwaa la hoja sio ushabiki, tulumbane na kisa kaka.
   
 11. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hujaeleweka kwa sababu umekita kuelezea maisha yake binafsi ili kujenga hoja ya kutokuwa na msimamo na hivyo kutofaa kuwa rais wa nchi badala ya kuhusisha zaidi misimamo yake katika maisha ya siasa.

  Nadhani kwa ufinyu wako wa akili unafikiri kuwa mtu kumwacha mke wake kunaweza kutosheleza kuelezea hoja ya kutokuwa na msimamo.

  Umemwelezea Dr. Slaa kuhusiana na urais 2010, lakini umeshindwa kutoa jibu kuwa nani anastahili na kwanini.

  Kwa mfano, kwako wengine hata wakiuza nchi kwako ni sawa ila mwingine akimwacha mke wake hata bila wewe kujua sababu yake unakurupuka na kubwabwaja maneno yasiyo na maana kwa watu eti fulani hana msimamo
   
 12. Nova Kambota

  Nova Kambota Member

  #12
  Sep 20, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa mbona tunashindwa kuelewana kitu rahisi tu? Hata mtoto wa darasa la kwanza anaelewa........ .....sasa kama Dkt Slaa amekosa msimamo kwenye maisha yake binafsi atawezaje kuwa na msimamo kwenye mambo ya kitaifa? Kashindwa maisha yake mwenyewe atawezaje maisha ya watanzania milioni arobaini?

  Au ndio kusema kama padri kashindwa kuongoza parokia yenye waumini wachache akipewa uaskofu kuongoza jimbo zima ataweza?
   
 13. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Hana hoja, hashawishi wala hadanganyi mtu, mpotezee.
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Sep 20, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nova, hivi mapadre ambao wanaendelea na uhudumu wa altare na wana wanawake nje na watoto bado wana wito wa upadre wa Roho Mtakatifu au Roho Mtakatifu ndio kawapa nguvu ya kupata huko nje?
   
 15. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Sasa kaka wewe ndio hueleweki.

  Ulimaliza seminari 2007 au ulifukuzwa? Na Roho Mtakatifu unaemwongelea ni yupi? Na alikuelekeza nini wewe ambacho unakifanyia kazi sasa?

  Kwanza kwa taarifa yako Dr Slaa ni binadamu [naona ulihisi ni malaika] halafu ujue watanzania wanataka rais anaetokana na wao.

  Na mpaka sasa hao ni kati ya hawa DR SLAA, LUTENI KIKWETE, PROF LIPUMBA, NDG MUGHANYWA, USTAADH RUNGWE NK. Sasa hatutaki porojo zako, tuambie tumchague nani kati ya hao na ni kwanini?

  Umeanza na madhaifu ya Slaa eleza madhaifu ya wote na mazuri yao kama yapo. Hapo ndipo tutakuelewa, sio unaleta hoja za kutumwa na mafisadai hap. Hiyo asasi unayofanyia kazi najua ina hela za wafadhili wanaohitaji ripoti mwisho wa siku.

  Mwisho nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitamshukuru aliyekutuma, ametuongoza kwa kipindi hicho na kuna mazuri aliyafanya ingawa yamezidiwa na aliyokosea au kusahau au uezo mdogo wa kutawala. Tunamwomba apumzike asubiri taji maaa lipo muda ukifika, na tuombe Mungu atupe kongozi [si mtawala] anaeweza kutuongoza kuanza safari ya kuwafukuzia waliotuacha katika safari ya maendeleo mf Koea kusini, ambao mtawala wetu akienda kule ni kuomba msaada.
   
 16. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kambota,

  Nimeisoma tena makala yako na kwa mara nyingine nadhani ama unamchukia Dr Slaa kama mtu binafsi (kitu ambacho siyo ajabu) ama unatumiwa na watu, mafisadi, ambao anawapiga vita na ameahidi kuwawajibisha kwa kuliibia taifa hili.

  Hoja zote na sababu zako za kutuaminisha kuwa Dr W Slaa hafai kwa sababu hana msimamo ni za kitoto na hazina mashika.
  • Katika masuala mazito kama uongozi wa wengine ni watu ndio wanakaa na kutazama nani miongoni mwao anafaa kuwa kiongozi wao, na kwa kazi nzito kama Urais waadilifu wa kweli hawawezi kuuomba kwa sababu ni mzigo mkubwa. Kama ulimsikiliza kwenye hotuba yake ya kukubali alikiri kuwa haikuwa kazi rahisi kukataa sauti za watanzania waliomuomba agombee na kwa kukubali ombi hilo haimaanishi kuwa hana msimamo. Ni kazi ya watu na alisubiri sauti zao ili ajitokeze
  • Kuacha upadre pia siyo hoja ya kusema kuwa alifuata mkubwa, nadhani yeye ni mtu wa kuigwa. Kuna watoto wangapi ambao wamezaliwa na mapadre wa RC? Mimi nawafahamu watatu na kuna mapadre zaidi ya watatu ambao nawafahamu wamekufa kwa ukimwi hawa wote walikuwa wanafiki kuendelea kuwa mapadre wakati waliona wameshindwa baadhi ya masharti ya upadre. Mtu anayetafakari nakuona njia niliyochagua siyo ya wito wangu ni mtu mwenye misimamo na anafaa kuigwa, siyo kubezwa.
   
 17. Nova Kambota

  Nova Kambota Member

  #17
  Sep 20, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF tuendelee kujadili au mmeshindwa? Someni pia kwenye menu kuu article yenye kichwa cha habari what is it?

  Kwa uwezo wangu wa kujenga na kubomoa hoja nitakavyo wanajamii wenzangu mna kibarua kigumu sasa kwa maana hapa ni mwendo wa hoja tu hakuna jazba, fujo wala matusi ni hoja tu kwenda mbele.
   
 18. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2010
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kambota,

  Mwambie Lula mwenyewe ajibu hizo hoja.

  Makala yako imetulia ndio maana huyo mpiga debe wa Chadema anaishia ku poromosha matusi tu
   
 19. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #19
  Sep 20, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,067
  Trophy Points: 280
  Hao wenye 'msimamo' na 'wanaomudu maisha yao binafsi' imekuwaje wakatufiukisha hapa tulipo? Tena bado wanataka kurudi tena na tena madarakani kuendelea kutudidimiza! Pengine sisi wapiga kura ndio hasa tunahitaji kuwa na msimamo maana tunazidi kuwa masikini lakini tunashindwa kusema NO!
   
 20. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #20
  Sep 20, 2010
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Safi kabisa! mjibu moja kwa moja badala ya kuzunguka mbuyu!
   
Loading...