Lukuvi ulikiwa unakusanya kodi ya majengo ili uje utubomolee nyumba?

Kwa Dom tuliza akili kidogo, kiwanja unacho unalipia ramani unasoteshwa miaka 3 hujaipewa unaomba kibali unasumbuliwa miaka mi 2 bado hujakipata UNASUBIRI NINI KUJENGA NA PESA HAIWEKEKI HASA KWASISI MASKINI!!!! MI YANGU IPO AREA D NIMEJENGA MWAKA 1999 WAJE TU WABOMOE !!!
 
Msimlaumu lukuvi. Anafuata maelekezo ya mkuu wake wa kazi. Rais ndiye aliyetoa haya maamuzi, lukuvi messenger tu.
 
Kwanza ile kodi najuta kuilipa maana inakwenda nusu mwaka sasa ile barua sijawahi kuipata kila ukienda TRA wanakwambia bado hatujaziandaa mpaka risti yao ishafutika nimebaki na copy, sasa ndo anataka kubomoa dah! Mi naomba Mungu ambomoe yeye kwanza kabla hajabomolea wananchi
 
Nimeona tangazo lako ukiwa Sumbawanga ukiwa unazungumzia ujenzi holela, na kutoa agizo kwa wakurugenzi wa halmashauri kubomoa nyumba za watu wote waliojenga ama kiholela ama bila kibali cha ujenzi, wakati unatutishia watanzania kuhusu kulipa kodi ya majengo naamini haya yoye ulikuwa unayajua ila ukataka ukusanye kwanza hela na kweli ulipata nyingi nakumbuka foleni ilikuwa inakesha ili mtu aweze kulipa kodi, leo watu wale wale uliochukua kodi zao unawatishia kuwabomolea nyumba, kiuhalisia zaidi ya asilimia themanini ya ardhi Tanzania haijapimwa na zaidi ya asilimia tisini ya majengo hayana vibali vya ujenzi kwa hiyo kama agizo lako litatekelezwa ina maana nyumba zitakazo baki no magorofa yale ya kariakoo ofisi za serikali na majumba makubwa ya ibada haya ndio huwa naona yanapewa kipaumbele kwenye kupewa vibali, hati nk, binafsi zoezi la kufuatilia hati mpaka sasa ni mwaka wa pili nishalipia voucher bado naambiwa nisubiri mpaka i printiwe kisha niletewe nitie sahihi halafu iandikwe barua kwa kamishna ndio hati iandaliwe ambapo pia kuna watu wengi wanasubiri zoezi kama hilo hivyo inabidi usubiri, na ukija kwenye vibali vya ujenzi hali kadhalika utaratibu ni kuandika barua kwa mkurugenzi nakala kwa afisa mipango miji wa eneo husika uambatanishe na hati ambayo imechukua miaka mitano kuipata na uorodheshe wakandarasi ambao watashiriki ujenzi wakiwamo mafundi umeme mafundi bomba mafundi ujenzi kisha baraza la madiwani kikae halafu wajadili kama nyumba yako inakidhi vigezo kifupi ni kitu ambacho kinaweza kuchukua miaka hata kumi kweli sisi waTanzania tuna amani upendo na uvumilivu na ujinga ndani yake lakini hapa nadhani ...badamu batamwagika....
Tuko namba 2 mpka 9 kazi tunayo..
 
Hizo process kwa tunaojenga chumba kimoja kimoja mpaka nyumba nzima inakamilika inawezekana kweli?
 
mwakani Lukuvi ataanxia wapi kudai kodi ya Majengo? Au kwa kuwa atakuwepo wizarani anataka kuwaharibia watakaochukua nafasi yake?????
 
Niliwahi jiuliza hilo swali iweje wanaolipa kodi za majengo hao hao tena wanabomolewa...
 
Ile kodi ya jengo iliyopigiwa chapuo ulikuwa ni utapeli tu, utalipaje kodi ya jengo ambalo haujamilikishwa kisheria? Mie nilimtimua mwenyekiti wa mtaa na silaha za jadi hakurudi,
 
Back
Top Bottom