Lukuvi: Tunakuja na bei elekezi kwa viwanja

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,961
Akijibu maswali bungeni kuhusu wizara ya ardhi na makazi, Wiliam Lukuvi amesema wapo watu na makampuni yanaoingia mikataba na wapimaji binafsi wa viwanja kisha kuviuza kwa bei ambazo hazinunuliki, kwa hiyo wizara yake itajikita kutoa bei elekezi ya upangaji wa bei za viwanja, ili watu wasijiuzie wanavyotaka.

Pia amezungumzia makampuni yanayonunua mashamba na kuyageuza kuwa viwanja, suala ambalo amesema halikubaliki.

Msikilize zaidi hapa

 
Waanze na viwanja vya serikali vinavyosimamiwa na manispaa, waende kwenye nyumba za serikali kupitia mashirika yake-sitaki kuamini kwamba Mtanzania wa kawaida anaweza kununua nyumba kwa zaidi ya M50! Lukuvi na serikali watuondolee huu usaniii!
 
Hakuna kiwanja ambacho hakinunuliki labda kiwe hakiendani na bei hiyo! We uliyeshindwa kununua kiwanja una shilingi ngapi na unataka ununue wapi?! Nilionya kuwa taifa linarudi kwenye ujamaa kiaina.! Huu ni mfumo wa hovyo kabisa!

Ushabiki mwingine sijui unamkomo nan na hapo unawadogo zako hawana viwanja pengine kwa sababi ya gharama kwa mfano mshahara wa selikal hauruhusu kununua kiwanja manake otafika mahali wafanyakaI wa umma hawatokuwa na viwanja kama hali itaendelea
 
Lukuvi kweli hapo umeongelea jambo la maana kabisa. Japokuwa nimesikia unasema eti almashauri zipate faida kwenye kupima viwanja! Hapa mimi nasema HAPANA, kazi ya kupima viwanja kwa Manispaa na Almashauri ni moja ya jukumu muhimu kwa niaba ya serikali kuu na kisiwe chanzo cha mapato.

Iweje sasa waanze kutaka kupata faida kwenye kupima viwanja? Tutiendekeza hizi faida hata kwenye Afya wataanza kulenga faida, Elimu itakuwa hivyo pia na mwishowe serikali itawahudumia matajiri tu.

Viwanja hasa mijini vinakuwa na bei isiyo na uhalisia. Ngoja tusubiri utekelezaji manake maneno matamu alikujanayo Prof. Anna Tibaijuka lakini hatukuona lolote!
 
Mtu ukiwa na shamba lako unakabidhi halmashauri kwa sheria ipi. Halmashauri ikitaka shamba lako ni lazima wakulipe fidia. Hayo mambo ya kurudisha halmashauri ni utopian
 
safi sana Lukuvi

wewe ni mmoja wa mawaziri ninaowaelewa sanaaa
Hata mimi namkubali sana huyo,swala la ardhi limekuwa shida sana.Unakuta eti kiwanja bagamoyo kinauzwa 18,500/- kwa m^2 can you imagine ili upate kiwanja angalau cha vyumba 3 tu lazima ikutoke si chini ya milioni 10, kwahiyo hii biashara ya ardhi kwa muda mrefu imekuwa jipu na unakuta ni watz wachache ambayo wanaweza kuafford pesa nyingi hivyo.Ukipigia na gharama za ujenzi si chini ya milioni 75 zinahitajika.

Mfanyakazi wa kawaida hawezi kujenga kwa namna hiyo hata kama atakwenda kukopa bank
 
Back
Top Bottom