Lukuvi: Serikali kuanza kutoza kodi kwa kumiliki ardhi isiyopimwa!!

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,292
Hayo yamesemwa na Waziri Lukuvi

Maoni yangu:
Serikali kabla ya kuchukua measures kama hizi, ijitidhishe impact yake katika vita dhidi ya umasikini, Matokeo ya measures kama hizi ni kwa raia wenye vipato vya chini kushindwa kumiliki ardhi kwa sababu it is too expensive kuimiliki na wale wachache wenye nacho pekee ndiyo watakuwa na uwezo huo.

Pili kitendo cha kuanza kuchukua kodi za viwanja kwa wale waliojenga kwenye squatters, kutasababisha watu wasimudu kuwa na uwezo wa kumiliki hata hivyo vinyumba , Wenye nyumba watapandisha kodi, kasi ya ukuaji wa miji itapungua, na hata lengo la serikali la kuongeza pato kupitia hizo kodi itakuwa counter productive.
 
Shida ya sera ya ardhi ina double std, huku wanahubiri Hati za kimila ambazo wenye benki hawataki hata kuziona, pia kuna zile kubwa, huku wakijua kuwa Hati za kimila ni utata mtupu linapokuja suala la dhamana Benki.
 
Kweli kabisa mkuu na achilia hati za kimila na hata leseni za makazi (residential licence) bank nyingi hawaziitaji
 
Serikali ya mkurupuko.
Huyu jamaa kashangaa kuona kuna mtu anamiliki hekari 3500 na akaizawadia serikali hekari 1500.

Sasa kwa statement yake hajui impact yake iko vipi.

Watanyang'anya watu ardhi na nyumba zao na sijui watataka nao watu wakakae wapi
 
Viongozi wengine wanafanya maamuzi bila kujua uwezo halisi wa watu wao!
Wananchi wengi bado wanahangaikia kula, halafu unataka hata ardhi wanayoimiliki, ambayo hawawezi kuikopea pesa benki itozwe kodi hii imekaaje?

Halafu kodi hii imeidhinishwa katika bunge lipi au katika vikao gani vya halmashauri za miji?
 
Mbona serekali hii imekuwa kama kupe mfyonza damu kila kona ni kodi,mwananchi atakamuliwa hadi povu litaisha.
 
serikali haina fedha kupimia viwanja ili iweze kukusanya kodi kirahisi ? ukitaka pesa wekeza kwanza.unataka kuvuna usichopanda ?
 
Hata hivyo kodi zenyewe huwa ni kiduchu sana.. Mie sijalipa tokea 2010 nilienda kutizama baada ya Tangazo la Kupelekwa Mahakamani nikakuta Deni kumbe ni Laki pamoja na riba... so miaka 7 chini ya laki si mbaya nikienda lipa nitalipa twice ili tutafutane 2024 huko deni litakapo kwisha... Jamani Kha!
 
nasikia ardhi ni ya serikali. je ile ambayo haitumiwi na mtu serikali itakuwa inailipia kodi? ardhi ya vijiji, vijiji vitailipia kodi?
 
Bila shaka una kiwanja chenye ukubwa chini ya Mita za mraba 450, matumizi ni makazi pekee na hakipo katika moja ya majiji. Mkuu kodi zilipanda kwa 300% wewe bado kodi ya 7yrs iko chini ya laki pamoja na penalty? Hongera.
 
nasikia ardhi ni ya serikali. je ile ambayo haitumiwi na mtu serikali itakuwa inailipia kodi? ardhi ya vijiji, vijiji vitailipia kodi?

Kwa mujibu wa sera ya Ardhi, inamilikiwa na wananchi ila ipo chini ya Rais kama mdhamini. Na ndio maana baada ya mabadiliko yaliyoleta sheria zinazotumika hivi sasa, ardhi inaweza kuchukuliwa na serikali baada ya fidia kwa mmiliki. Kabla ya hapo ardhi tupu haikufidiwa.

Na kuhusu kodi, inatozwa kwa maeneo yanayomilikiwa na watu ama taasisi with few exception kama Government allocations na maeneo ya ibada. Kwa hiyo obviously general land, village or reserved land haziwezi kulipiwa kodi hadi zitakapomilikiwa bila hizo exceptions hapo juu
 
Kwa maoni yangu, serikali iendelee kuchukua kodi kwa maeneo yaliyopimwa tu, makazi ambayo hayapo kwenye viwanja vilivyopimwa talipishwe property tax tu. Sio vizuri kumlipisha mtu kodi ya kiwanja wakati hana hata access ya barabara, mifumo ya maji taka na kadhalika.

Na ni uzembe wa serikali kutopima viwanja vya kutosha kwa bei nafuu.
 
Bila shaka una kiwanja chenye ukubwa chini ya Mita za mraba 450, matumizi ni makazi pekee na hakipo katika moja ya majiji. Mkuu kodi zilipanda kwa 300% wewe bado kodi ya 7yrs iko chini ya laki pamoja na penalty? Hongera.
Hakika atakuwa na kiwanja chenye sifa hizo. Nadhani Huyu hajui kuna viwanja vinalipiwa 100,000+ kwa mwaka.
 
Bila kuwa na sera thabiti, tutabaki kukurupuka tu na matamko . Mwisho wa siku unamlipisha kodi mtu ktk eneo la mtu mwingine au serikali ,halafu baadaye unasababisha mgogoro mzito. Serikali wekezeni ktk kupima ardhi na viwanja ili mkuasanye kodi halali.
 
Back
Top Bottom