Lukuvi pamoja na porojo zote lakini watoto wanakaa chini?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lukuvi pamoja na porojo zote lakini watoto wanakaa chini??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magezi, Dec 13, 2009.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  Dec 13, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  A stand V teacher of Mkombo Primary School at Vingunguti in Dar es Salaam teaches mathematics as his pupils sit on the floor due to acute shortage of desks. (Photo: Khalfan Said)


  Bila kuiondoa CCM haya hayatakoma. Hivi kikwete ukisitisha safari 2 tu za nje hiyo hela si ingeweza kununua madawati ya shule kama 10???
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  [​IMG]
  Lakini mi ninachoshangaa ni vp darasa zuri namna hiyo linakosa madawati?
  Hao wazazi wanasubiri Lukuvi apeleke madawati hapo shuleni?
  Mbona wamevaa sketi na kaptura nzuri sana, inakuwaje wanashindwa kuchanga madawati tu?
   
 3. M

  Magezi JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nilitoa wazo jana mkalipinga la kuwa na mifuko ya kuchangia vitu kama hivi sasa mkuu unauliza wazazi wako wapi?
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kumbuka jana ulisema kwamba watu wachange hela za kuwapeleka watoto sekondari kwa njia ya ushirikiano, badala ya kuchangia harusi!
  Hili jambo la kumchangia mtoto wa fulani aende shuleni ni tofautina kuchangia madawati ya darasa zima!
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Inatia simanzi kuona nchi yetu bado ina hali hii. Na ikumbukwe kwamba hapo ni mjini ambapo hata waandishi wa habari japo wanaweza kupita na kupiga picha kama hizi. Mimi nilikaa chini toka darasa la kwanza hadi la tatu. wala hakutokea yeyote kuja kusema mazingira ya ufundishaji ni mabaya. But kwa kumbukumbu zangu, pamoja na ugumu wa maisha wa wale wananchi wa kijijini. Ulianzishwa mkakati wa kila balozi kuchangia madawati kadhaa. Ikawa balozi na watu wake wanachangishana kuhakikisha wanatengeneza madawati. But kwa hapa mjini sijui wanaweza kutumia strategy gani. Infact wanaoteseka ni watoto wetu. Inatubidi tuchukue hatua. Hii habari ya kusubiri akina Lukuvi ambao watoto wao wanasoma katika shule ambazo ni standard, tutapoteza muda bure. Siunajua aliyeshiba hamjui mwenye njaa? Sisi tunayeona uchungu watoto wetu kukaa chini, tuanze kuchukua hatua mara moja.
   
 6. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ule mpango wa kufukuza kazi mkuu wa mkoa ambaye shule yake inakosa madawati uliishiwa wapi?

  Nakumbuka kijiji kimoja huko kaskazini mwenyekiti wa kijiji alipitisha by-laws kwamba kila mwanaume lazima ajenge nyumba ya matofali na bati ..hakuna nyumba ya udongo, miti na majani..walifanikiwa (alikuwa mjeshi mstaafu)...nafikiri tunawahitaji watu kama hao
   
 7. kalikumtima

  kalikumtima Member

  #7
  Dec 14, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo ni Dar es salaam. Nenda vijijini kule. shule inaezekwa kwa nyasi. mvua ikinyesha wanafunzi wanalowa kwa maji ya mvua. mfano hai Geita vijijini binafsi nimeshuhudia kule.
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kalikumtima, kinacho sikitisha ni hicho kwamba hali ni hii Dar es Salaam ambapo rais wa nchi anaishi je kule kalenge au nyarumbugu sijui hali ikoje.
   
 9. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #9
  Dec 14, 2009
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wengi wetu tuko mstari wa mbele kuchangia harusi na sherehe zingine ambazo hazina tija lakini likija suala la Elimu tunarudi nyuma tunajifanya hatujui kinachoendelea. Hiyo Kamati ya shule imefanya mikakati gani kupata madawati? Ni aibu kubwa. Hapa ni Dar je vijijini?
   
 10. M

  Mjasiliamali Member

  #10
  Dec 17, 2009
  Joined: Oct 17, 2008
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawashukuru wahishimiwa woote mnao jenga hoja katika wigo huu! ila napenda kuwa arifu kuwa kwa sasa ndiyo narudi tena katika kilinge hiki cha kuchangia mwawazo shii kwa manufaa ya waTanzania wote, Kipindi kilicho pita nilichangia katika kujaribu kuweka sawa mazingira ya kutofautisha mazuri na mabaya ya kibinaadamu, hasa kwa wale wanao onekana kama kioo cha jamii. Hapa majuzi tume ona ama kusikia mazungumzo ya hapa na pale kuhusu mambo mbalimbali hasa maneno makali kuyaweka pasipo stahili, na mazuri kuyaweka pasipo stahili, mfano kumuita mtu fisadi pasipo uhakika, je? hamuoni kama huu waweza kuwa mtego wa panya? maana wapo watu wa aina hii ila tusi washirikishe wasiohusika!!
   
Loading...