Lukuvi njoo hapa Mwanalugali ujionee uhuni

mtima nyongo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
1,947
2,047
Hapa sekondari ya mwanalugali kibaha kuna tatizo tena kubwa la ardhi.Toka mwishoni mwa miaka tisini serikali ilichukua maeneo ya wakazi wa hapa na kuyapima kwa ajili ya kuendeleza mji wa kisasa na wale waliochukuliwa maeneo yao walipewa ahadi ya kufidiwa cha ajabu mpaka leo hakuna cha fidia wala nini na lile eneo limekua pori maana amna anaelima wala kuendelezwa chochote maana serikali imezuia
Mwaka 2015 upande wa pili wa shule hiyo hiyo tanesco wamekuja wamepima na wamethaminisha ardhi yetu na wanataka kupitisha umeme mkubwa unaoelekea arusha mpaka sasa ni mwaka hakuna kinachoendelea na ikumbukwe kuwa wameshazuia uendelezwaji wa aina yoyote kwa maeneo haya sasa sijui serikali ina ajenda gani na sisi maana sehemu ya kilimo tumezuiwa na eneo ambalo tumeweka vibanda na wengine walikua wanaendelea na ujenzi wamestopu ina maana kila kilichopo pale lazima kitaharibika sasa je serikali aioni kama inatudumaza raia wake?
Lukuvi njoo ujionee ili utengue kitendawili hiki
 
Duh polen sna ndugu zangu mzungu kawapa shirika la elimu wameshindwa kuliendesha ni shida tupu naona wamewaada kwa kauli ya rais alisema maeneo ambayo ayajaendelezwa ambao walipewa waendeleze wataporwa na kurudishiwa wananchi so jipangeni mkilemba atapewa muwekezaji mpya mtaeleea kusua gaga fanyeni uchunguzi wa kina kimya kimya ili mpate maeneo yenu tena mana shirika wanaeneo kubwa ng'ombe wapo wachache wanaweza tumia eneo lao fanyeni ivo kabla kauli aijapoa ndugu zangu tumieni fursa
 
Back
Top Bottom