Lukuvi kwanini viwanja vya Songwe Mbeya bei zake zinatisha?

JembeNaNyundo

JF-Expert Member
Dec 9, 2016
533
652
Hivi viwanja vya Songwe Mbeya Vijijini kwanini vinauzwa kwa bei kubwa hivi? Kwenye makazi square metre wanauza 11,500/=. Hii ni ardhi ya Serikali au?

Kiwanja cha square metre 600 ni milioni 6.9!!!

Hivi viwanja wanataka wanunue watu gani? Mtumishi anayelipwa laki 3 kwa mwezi?

Mambo haya ndio huchochea ufisadi makazini, hasa kwa watumishi wa umma.
 
Ulitaka viuzwe bei gani?
 
Mbaya zaidi serikali imepora mashamba ya watu kupima viwanja!!!
 
Hivi viwanja vya Songwe Mbeya Vijijini kwanini vinauzwa kwa bei kubwa hivi? Kwenye makazi square metre wanauza 11,500/=. Hii ni ardhi ya Serikali au?

Kiwanja cha square metre 600 ni milioni 6.9!!!

Hivi viwanja wanataka wanunue watu gani? Mtumishi anayelipwa laki 3 kwa mwezi?

Mambo haya ndio huchochea ufisadi makazini, hasa kwa watumishi wa umma.
Fanya huo ufisadi uone moto wake, utakuwa wa kwanza kwenye ile mahakama.

Btw serikali iliangalie hili hiyo bei ni kubwa sana kwa wafanyakazi wa kada za kati na chini
 
watumishi wa umma mnataka kununua viwanja vya nini? subirii mkilipwa mafao yenu ya kustaafu ndio mnunue
 
Viwanja vikiuzwa hivi nchi nzima hakutakuwa na makazi holela, makazi ya ovyo yanatokana na halmashauri kukosa pesa za kulipa fidia wenye mashamba ili wagawe viwanja. Bei zikiwa hivi wataweza tena kwa faida, na hivyo wilaya nzima itapimwa.

Vile viwanja vilivyokuwa vinatolewa kwa bei ya ujamaa ndio vimesababisha 70℅ ya nchi kuwa makazi holela, eti wanawasaidia maskini???
 
Sasa we unataka uuziwe tsh ngap?huangalii hata potentiality ya eneo?kama hujui huko ndiko jiji linakoelekea sasa!

kama huna fedha si ununue hata NSALAGA DAMPO au UYOLE MILIMANI?
 
nimeona matangazo yao Azam tv,nafkir vitakuwa vimeshuka sasa,nasi wasulupwete tukauzunguke uwanja!!!
 
Back
Top Bottom