Lukuvi, CCM wanaogopa kuzunguka nchini, watazomewa kama September 2007 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lukuvi, CCM wanaogopa kuzunguka nchini, watazomewa kama September 2007

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SubiriJibu, Jun 29, 2012.

 1. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,126
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  William Lukuvi leo mchana wakati anafanya rewinding kujibu hoja za wabunge ameeleza jambo moja kwamba wabunge wa CCM wasitishwe na kitendo cha wapinzani kuzunguka sasa nchi nzima.

  Lukuvi inaelekea alikuwa anajibu hoja wanayoulizwa kwamba "mbona nyinyi CCM hamzunguki wakati wenzenu wanazunguka nchi nzima".

  Katika majibu yake Lukuvi kaeleza kwamba wao CCM hawazunguki kwa sababu wana kazi ya kufanya. Wao ndiyo wameshikilia serikali na hivyo wako kazini. Wasio na kazi waache wazunguke na huko wanakozunguka watakuta matatito ambayo hawawezi kuyatatua bali watayaleta tena kwenye serikali ya CCM iyatatue.

  Ni kweli CCM ndiyo iko serikalini.

  Sijui kama Lukuvi aliwasiliana na watu kama Nape Nnauye. Kwani wao wenyewe humo ndani ya CCM wamelaumiana kwamba Nape kazi yake ni kuzunguka mara kuwapaka wengine matope, mara kuwaita watu mafisadi, mara kuwaambia watu kuwa wajivue magamba. Yote hayo ni hukohuko ndani ya CCM.

  Lakini kazi nyingine anayofanya Nape na wenzake ni kuzunguka walikotoka wapinzani iwe kimaeneo au kikauli. Kikauli ameanza siku hizi. Wenzake wamebuni VUA GAMBA VAA GWANDA yeye kaiga kwa kusema VUA GWANDA VAA UZALENDO. Hiyo ndiyo CCM. Kila mmoja na kaui yake maadam imetoka ubongoni ikateremka mdomoni.

  Lakini Lukuvi kama walivyo wana CCM wengi wanadhani bado tu wepesi wa kusahau. Lukuvi anasahau kwamba Bunge la Bajeti mwaka 2007 lilipoisha Serikali ilituma Mawaziri wazunguke mikoani kuhubiri umuhimu wa Bajeti. Ni kipindi kile ambacho Zitto kabwe kafungiwa miezi kadhaa na akatumia kifungo hicho kuzunguka huku na kule kama Godbless Lema anavyofanya sasa.

  Kilichotokea ni kwamba mawaziri hao walizunguka lakini wakaishia kuwa wanazomewa ovyo. Matokeo ya kuzomewa tumeyaona, kidogo nchi iwachomoke 2010.

  Sasa, Lukuvi inawezekana kasahau na anafikiri na sisi tunasahau. Anasahau kwamba kuna kitu inaitwa Jamii Forum na mitandao mingine anayoiogopa inakumbushana kila leo na inachambua kila kauli wanayotoa.

  Hivyo, Lukuvi lete kauli nyingine hii umepitwa na hoja. bahat nzuri mawaziri siku hizi mnaangalia JF kila mpatapo nafasi. Hivyo, wakati mnarudi mjengoni jioni leo jua kwamba wananachi tayari tumeshatoa tamko letu kama hili mitandaoni na kauli zenu zinapata majibu palepale hukuhuku mitandaoni mapema ndani ya dakika chache.
   
 2. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Lukuvi ana wasiwasi wapo watu wanafikiria yeye sio kiongozi wa nchi hii,kwamba wako viongozi wengine. Sisi tunajua Lukuvi ni kiongozi. Hakuna mtu yeyote aliyekuwa kiongozi wa Tanzania katika siku hizi za karibuni isipokuwa Lukuvi na wenzake. Ndio maana haya makosa yote yanayotokea ni lazima walaumiwe wao.

  Na we sijui umewezaje kuandika all this stuff,kwa sababu Lukuvi amemaliza kuongea sasa hivi.
   
 3. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,126
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Mkuu Andrew,

  Kwanza Shikamoo.

  Eti nimewezaje kuandika yote haya wakati Lukuvi kaongea dakika hii. Baba yako mzazi watu walikuwa wanamshangaa hivyohivyo. Kuna story nilisikia Marehemu Prof. Haroub Othman anasema student wa UDSM walimfuata pale Ikulu kumpelekea vitabu vipya kabisa halafu wavijadili.

  Akawapa time ya wiki moja warudi. Wanafunzi wale walidhani kwa sababu ya majukumu mengi ya ukuu wa kila kitu yaani head of state, head of CCM, Head of frontline states wakadhani hatapata muda wa kuvisoma.

  Wiki ikaisha, wakakaribishwa state house. Wakajadili na Kambarage kana kwamba ndiye alikuwa mwandishi wa vile vitabu.

  Huo ndiyo urithi tulioufuata wa tabia ya huyu marehemu mzee wetu kipenzi chetu, kipenzi cha watanzania, aliyeipenda Tanzania kuliko hata familia yake yaani watoto wake wa kuzaa kama nyinyi.
   
 4. M

  Maseto JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 721
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Kile kitendo cha Lukuvi kumpongeza mwenyekiti wa kijiji aliyemzuia mbunge wa viti maaluma wa upinzani kufanya mkutano wa hadhara katika jimbo la Ismani la Lukuvi,hakikuwa sahihi na kilaaniwe kabisa.Mbaya zaidi Lukuvi ameahidi kwenda kumuona mwenyekiti huyo.Nadhani anataka kumpatia takrima.
  Mtu hatalaumiwa akidhani kuwa mwenyekiti huyu alitumwa na mbunge wake
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kazi nyingi za kufanya kama Mabwepande? Hata hivyo hao wanaozunguka wamekutana na tatizo, ni Dr Ulimboka, CCM wanatakiwa watatue ili tatizo.
   
 6. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,126
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Mkuu, naomba tusivuruge mada niliyoleta na kuwapa nafasi watu ambao mada imewafanya wakae kimya tofauti na tabia zao humu JF.

  Nimesikiliza vizuri ni kwamba yule aliyenyimwa nafasi kuhutubia hakuwa na kibali. Sasa utamtetea vipi. Mbona kwingine wengi wamenyimwa vibali na wakarudi. Jangwani wamenyimwa vibali mara ngapi.

  Cha msingi yule dada kama ni wa CHADEMA au vinginevyo basi aende aombe kibali arudi kuhutubia kijiji hichohicho alichonyimwa ndiyo utakuwa mwisho wa yote yale.

  Washabiki wa upinzani ndipo hapa mnapopotoka. Nchi nzima ina-sympathise kwa hoja zenu. Lakini msipitilize hadi kudhani kukosea taratibu kama vile kukosa kibali mtapata washabiki wa ku-sympathize na hilo.
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  huyu anaweza akabeba mikoba ya Pinda(endapo watafanikiwa 2015)
   
 8. Unkolonized

  Unkolonized Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hebu wapeni vidonge hao mahayawani sisiemu!!!
   
 9. Unkolonized

  Unkolonized Member

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lukuvi simpendi tangu akiwa RC wa Dom, coz alinichukulia demu wangu pale Udom alaf akamharibia maisha tu binti wa watu kwa kuridhika na kufuatwa na shangingi chuoni!
   
 10. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Mkuu, Haujatoa jibu. Na we sijui umewezaje kuandika all this stuff,kwa sababu Lukuvi amemaliza kuongea sasa hivi?
   
 11. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,126
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Mbona nilijiona kama nimetoa jibu. Baba yake Andrew aliturithisha elimu. Elimu kujizoeza hata kuandika au kusoma kilicholetwa mbele ya uso wako.

  Kama ni jibu mnalohitaji basi labda sijawaelewa, maana nimetumia dakika kama saba ku-draft na ku-click send button ya laptop yangu.

  Niko likizo wiki hii na hivyo naangalia bunge na mbele yangu kuna laptop.

  Labda mimi nimshange Andrew kwa sababu ameishi na baba ambaye huwa tunashangaa aliwezaje kutoa hotuba nyingi bila kuandika wakati viongozi wote waliomrithi hakuna mwenye uwezo kama huo.
   
 12. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  mkuu kwa hiyo kibali cha mkutano kinatolewa na mwenyekiti wa kijiji?
   
 13. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,126
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Hoja ya Lukuvi ilikuwa ni kwamba yule kama mkuu wa serikali kwa kijiji hakuwa anajua lolote kuhusu huo mkutano.

  Huwezi kulitetea hili hadi uje na maelezo kwamba inapotokea hali hii kinatakiwa kufanywa nini.

  Huwezi kuukwepa ukweli anaoutete Lukuvi lakini na wewe eleza ni nini mipaka ya huyu mtawala kiserikali wa kijiji ama ile kata.

  Ni bora ukalichukulia hili kama precidence lifanyiwe kazi maana likiigwa kote yaweza kuwa balaa.
   
 14. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Bado hujajibu swali husika, je, kibali cha kufanya mikutano kinatoka kwa mwenyekiti wa kijiji???
   
 15. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,126
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Sina hakika kama ni yeye anayetoa kibali. Ila nina hakika kwamba kama hakujua lolote kuhusu kuwepo kwa mkutano ana haki na uwezo wa kukataa.

  Labda nikuulize. Mwenyekiti wa Kijiji hana maguvu ya mwili kuzuia mkutano usifanyike. je, kama alikataa alitumia chombo gani kukataza mkutano? Kama ni polisi ambacho ni chombo cha dola, unadhani ilikuwaje chombo cha dola yaani polisi kikashindwa ku-sort out controversy ndogo ya kuruhusu mkutano kama kulikuwa na kibali rasmi.

  Kama kibali kilitoka juu na kisitoke kwa Mwenyekiti polisi wangeshindwa nini kulinda mkutano huo.

  Vinginevyo kama justice was not served basi hata wewe usingeishia kumtaja Mwenyekiti na ungeenda mbali hadi kuwataja polisi kwa irresponsibility ya kulinda mtu aliyekuwa ni halali kutumia eneo kwa mkutano.
   
 16. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #16
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Unakosea, hakuna kibali chochote, isipokuwa unayetaka kufanya mkutano huu ni lazima utoe taarifa polisi, na hii ni kwa sababu ya kupewa ulinzi
   
 17. m

  maingu z Senior Member

  #17
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza mkoa wenyewe anaotoka ndo wamechoka mbaya na baado wamekumbatia kijani ni wakuwaonea huruma angalia hata wabunge wanaotoka huko kama wakina LUSINDE, kweli hao watu wana akili timamu. waacheni wameshazoea kuishi kwenye vichuguu wameridhika. Kwahivyo ni wakusaidiwa tu njia rahisi wanayojua kuja kutusumbua kuomba omba.
   
 18. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #18
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Tunatoa taarifa na si kupewa kibali.
   
 19. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,126
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Unalotoa ni jibu rahisi sana ambalo sidhani kama brilliant people like CHADEMA mle bungeni wasingeweza kuinuka na kumpa Lukuvi kiitwacho TAARIFA ili kuweka hansard katika balance.
   
Loading...