Lukuvi atangaza vita ya kunguru weusi a.k.a kunguru wa Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lukuvi atangaza vita ya kunguru weusi a.k.a kunguru wa Zanzibar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Hofstede, Jul 28, 2009.

 1. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, ametaka kunguru weusi au maarufu kama kunguru wa Zenji waangamizwe. Mimi binafsi ninamuunga mkono mkuu wa mkoa kwani kunguru hawa ni kero kweli kweli hasa kwenye ma bar ya chini ya miti. Mimi binafsi wameisha nifanyia vurugu mara nyingi tu, nakumbuka kuna siku niliagiza maziwa fresh, nikanywa mara ya kwanza, kuweka grasi chini nikaona baadhi ya maziwa yameruka kama mtu katumbukiza jiwe vile. Nikaangalia juu nikaona kunguru wawili, machale yakanicheza nikaenda chukua grasi ingine kumimina chini kukawa na settlements za mavi ya kunguru, nikamwaga maziwa yote, ila kama nisingeona ilikuwa nikute settlements kwenye tone la mwisho kuelekea tumboni sijui ingekuwaje. Kuna issue kama kuchangia nao supu ukienda kunawa, au hata kukuchafulia nguo kwa vinyesi.

  Ila naona suala la hawa kunguru limekuwa out of control. Kwa mkuu wa mkoa kutangaza watu waanze kuwaua naona kama hayupo practical hivi. Nakumbuka huko nyuma amri ya kuwauwa kunguru ilikuwepo na hata kutangaza dau la shs 50 kwa mzoga wa kunguru. Kwa kumsaidia mkuu wa mkoa zoezi hili haliwezi kufanikiwa kwa agizo alilotoa. Ili afanikiwe kuna njia kuu mbili za kufuatwa ili kuwaangamiza hawa kunguru.

  1. Njia ya kwanza ni mkoa kutangaza kununua mzoga wa kunguru kwa shs 200 tu, yaani mtu akiua kunguru mmoja akimpeleka Ilala Boma anapata shs 200. Ninakuhakikishia baada ya mwezi mmoja watabaki kunguru kumi tu Dar nzima, maana dili hili litachamkiwa kweli kweli badala ya watu kupiga debe vituoni. Ila ubaya wa njia hii ni ufisadi wa watendaji wetu,ni dhahiri watakula dili na wawindaji ku-overstate namba ya kunguru waliouwawa ili baadae wagawane malipo na wawindaji, hii sii-recommend kwa mazingira ya Bongo.

  2. Njia ya pili ni kutumia SCIENTIFIC METHODS. Hizi zipo nyingi kama mitego, kudiscourage mazalia kwa bongo itakuwa ngumu sana kwani minazi ni mingi. Ila kuna njia moja "OVOCONTROL" hutumia dawa za majira kuwawekea ndege kwenye chakula ili kufanya mayai yao yasianguliwe. Hii imetumika sana katika kudhibiti ongezeko la njiwa na gees kwenye nchi zilizoendelea.

  Ila agizo la kutaka watu wawauwe tu ndugu mkuu wa mkoa bado utakuwa hujafanya kitu kwani, mkono mtupu haulambwi. kama serikali imeamua kuwaangamiza kunguru ifanye campaign kama ya Malaria ambayo huhitaji pesa na si maneno matupu


   
  Last edited: Jul 28, 2009
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,611
  Trophy Points: 280
  Kabla ya kupambana na kunguru weusi, aanze kwanza kupambana na uchafu uliokithiri katika jiji la Dar ambapo unasababisha katika baadhi ya maeneo kuwa na harufu mbaya kutokana na uchafu uliokithiri. Akishaliweka jiji katika usafi wa kuridhisha basi anaweza kuendelea na vita dhidi ya kunguru weusi lakini kwa sasa hili halihitaji kupewa kipaumbele chochote ukilinganisha na swala la uchafu uliokithiri.
   
 3. isambe

  isambe JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 2,053
  Likes Received: 881
  Trophy Points: 280
  Hiyo sio solution,hawa wanafuata uchafu na jiji hili uchafu ndio mahala pake.Leo utawaondoa wote kwenye anga ya Dsm,next months watarudi tena kama uchafu utaendelea kurundikana
   
 4. I

  Ipo Siku Member

  #4
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anaacha kupambambana na uchafu anapambambana na Kunguru weusi, hii ni hatari sana kwa viongozi wetu wa aina hii.
   
 5. Kilinzibar

  Kilinzibar Senior Member

  #5
  Jul 28, 2009
  Joined: Mar 6, 2008
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama walivo tangulia wenzangu,swala kwanza jiji liwe safi mtu unashangaa jiji utafikiri viongzi hawaishi humu bwana!!!

  Kitu kingine nafikiri naye avue joho moja wapo kati ya ubunge na ukuu wa mkoa mana wakati mwingine utakuta yuko jimboni kwake sasa atashika mangapi?
   
 6. E

  Evy Member

  #6
  Jul 28, 2009
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  i wonder how many foolish leaders r engineering stupid moves like this and we still sitting our butts wondering why we r so poor? hello?
   
 7. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Nyie mnaonunua maji safi kwa zaidi ya sh. 300/- kwa ndoo, baba yenu hana nguvu tena ya kuua simba.
   
 8. W

  WONDERWOMAN Member

  #8
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kERO ni nyingi sana ambazo muheshimiwa angetusaidia kupambananazo sio kunguru wa mungu!
  usafiri kwa wanafunzi ,ukosefu wa vifaa na walimu na hosteli katika shule za kata
  ujambazi,ukosefu wa huduma bora za zimamoto ,uchafu uliokithiri,watoto wa mitaani na ombaomba,machangudoa,na mengine meeeengi ambayo labda yeye hayamkeri lakini sisi wana bongo hatuna raha nayo1

  IT IS COMMON EXPERIENCE THAT PEOPLE PERISH BY THE VERY MEANS BY WHICH THEY SEEK TO DESTROY OTHERS
   
 9. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Bungeni walikuwa wanapiga kelele juzi kuhusu matiti feki. Do you see the trend?
   
Loading...