Lukuvi akacha kusaidia majeruhi ajali Oysterbay

sikiolakufa

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
411
54
Katika hali isiyo ya kawaida waziri wa nchi uratibu na bunge William Lukuvi jana alikwepa kutoa msaada kwa majeruhi wawili waliojeruhiwa vibaya katika ajali ya gari na pikipiki eneo la coco beach. Licha ya waenda kwa miguu kumpungia waziri huyo asimame lakini aligeuza shingo kwa dharau na kuondoka.

Mimi najiuliza hivi viongozi si wanapaswa kuwa mstari wa mbele kusaidia wananchi. Je iwapo ajali hiyo ingekuwa imetokea kwenye jimbo lake la uchaguzi angekacha. Imeniuma sana majeruhi wale walikaa takribani nusu saa bila kupata msaada huku vigogo wa oysterbay wakipita pembeni....

Ni wazungu fulani tu watu wa Mungu waliguswa wakajitolea Land cruiser yao kumpakia dereva wa pikipiki ambaye alikuwa amevunjika vibaya lakini bado alikuwa anahema.

Viongozi kama Lukuvi hawafai ni wanafikir mtu alikuwa mkuu wa mkoa anashindwa kuguswa na watu wa Dar es salaam. Angekuwa waziri mkuu sawa tungesema sababu za usalama lakini nani anamuwinda Lukuvi?
 
Siwezi kumshangaa Lukuvi kwa alilofanya kwani hawa viongozi wetu huwa wanawathamini wananchi pale tu wanapokuwa wanatafuta ulaji. Ingekuwa kipindi cha kampeni ama uchaguzi upo hivi karibuni lazima angesimama na kutoa msaada.
 
Viongozi wa nchi hii wanaipenda Tanzania lakini hawawapendi watanzania.
 
Huyo si fisadi wa elimu? Msemakweli alishatangaza na yeye kakaa kimyaaaaaa
 
kwani wewe ni mgeni na huyo lukuvi wangekuwa vimwana angesimama na kutoa msaada 100%
 
ungeweka picha ili tuwe na uhakika na habari yako isije ikawa majungu tu
Ingekuwa ndio kipindi cha uchaguzi...hapo yeye mwenyewe (Luku-uvi) angesimama kisha akatoa msaada na kumwambia mtu mwenye ''camera'' ampige picha ili aonekane mtu mwema katika macho ya watu(Watanza-nia).......na mda si mda tungeziona hizo picha kwenye ''blogs''zimejaa tele....
 
Lukuvi yuko fasta kwenye kujimilkikisha vibali vya kuvuna misitu Sao Hill kule tu kwa kisingizio cha kusaidia miradi ya maendeleo ya jimbo. mambo kama hayo ya misaada kwa majeruhi wapi na wapi?
 
alikuwa anakwenda kwenye sherehe ya kutimiza miaka 50 ya chuo kikuu cha Dar es salaam na huko ni makosa kwa viongozi wakuu kuwahi kufika kabla ya wale wa chini
 
kama ni wale boda boda waendesha pikipiki ni afadhali alimwacha angefia palepale wamekuwa chanzo cha ajali na usumbufu barabarani tumewachoka
 
kama ilichukua nusu saa kwa majeruhi kuokolewa basi si Lukuvu peke yake bali watanzania tulio wengi hatuna huruma kwani kwa idadi ya magari yanayopita coco beach sikutegemea kwamba ingechukua muda huo kutoa msaada... wenye roho mbaya ni wengi
 
kama ilichukua nusu saa kwa majeruhi kuokolewa basi si Lukuvu peke yake bali watanzania tulio wengi hatuna huruma kwani kwa idadi ya magari yanayopita coco beach sikutegemea kwamba ingechukua muda huo kutoa msaada... wenye roho mbaya ni wengi

kwa hiyo ww unahalalisha dhambi coz inafanywa na wengi?
 
kama ni wale boda boda waendesha pikipiki ni afadhali alimwacha angefia palepale wamekuwa chanzo cha ajali na usumbufu barabarani tumewachoka

Ni Binadamu wenzetu, sio kwamba wanaendesha bodaboda kwa kupenda wanatafuta maisha, maana ninyi mafisadi na magari yenu mnakunywa mpaka uji wa mgonjwa...Serikali inahitaji kutatua tatizo la ajira maana ndo chanzo cha yote haya.. Zile ajira 1M sijui walichukukiwa watoto wa akina nani? maana sisi ndo kwanza tunafukuzwa kisa hatuna vyeti, viwanda vinafungwa hakuna umeme, graduate hapati ajira kisa hana uzoefu na wengine hatujui kiingereza vizuri kama watoto wao walosoma nje....
 
kama ni wale boda boda waendesha pikipiki ni afadhali alimwacha angefia palepale wamekuwa chanzo cha ajali na usumbufu barabarani tumewachoka


Hivi binadamu huwa tuko wa aina ngapi jamani, huyu nae ni mtu na aliumbwa na Mungu kweli?
 
Back
Top Bottom