Lukuvi akabidhi ramani za maeneo yote ya mitaa ya Jiji la Dar kwa watendaji na wenyeviti wa mitaa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi amesema serikali inaanza zoezi la kutambua na kubomoa nyumba zote zilizojengwa kinyume na utaratibu hasa zile zilizoziba barabara na mitaro na itaanza na miji minne ikiwemo jiji la Dar es Salaam.

Lukuvi ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akikabidhi ramani za maeneo ya mitaa yote ya jiji kwa watendaji na wenyeviti wa mitaa ili kila mwananchi ajitambue eneo alilojenga kama hakustahili kuwepo aanze kujipanga.

Baadhi ya mameya waliohudhuria makabidhiano hayo mbali na kuelezea mipango ya manispaa zao juu ya suala la mipango miji wamesema baada ya wizara kutoa ramani hizo tatizo sugu la migogoro ya ardhi litapungua kwani kila mmoja atafuata taratibu na sheria zilizopo.

Wilaya ya Kinondoni ni miongoni mwa wilaya zinazodaiwa kuongoza kwa kuwa na migogoro mingi ya ardhi ambapo afisa mipango miji Bi Juliana Letara amesema asilimia 70 ya maeneo bado hayajapimwa wala kurasimishwa hali inayochangia manispaa hiyo kukosa mapato.
 
Hii ni hatari... Na ujue nje kidogo ya mji watu wanaendelea kuuziwa viwanja ambavyo havijapimwa na Lukuvibwapo kimya
 
Nyumba yoyote iliyojengwa bila ya kibali cha Manispaa ni Kinyume cha utaratibu jee zote zitapelekewa greda?
 
...asilimia 70 ya maeneo bado hayajapimwa wala kurasimishwa

Manispaa inachoangalia ni kukosa kodi WALA sio haki iliyopotea kwa muda mrefu kwa wakaazi wa K'ndoni.

Hawa ni "mbwa-mwitu" waliojaribu kujivisha "ngozi-ya-kondoo" kwa sababu hapo awali walikuwa chanzo cha upimaji holela "over-sudden" wamebadirika na kutaka kuwaadhibu wananchi kwa makosa yao wenyewe.

Wito: pamoja na nia nzuri ya utoaji ramani lakini wafatiliwe waliojenga kwenye maeneo ya wazi ili kujua kama mwananchi ndiye aliyevamia au aliuziwa na hawa "mbwa-mwitu".
 
wananchi wataadhibiwa mpaka lini?
ilisha tamkwa awali wale waliojenga katika makazi hatarishi ya usalama wao ndio watabomolewa hasa mabondeni /
LUKUVI HILI SIO JEMA,TULICHAGUWA ILI TUADHIBIWE?
 
Back
Top Bottom