Lukuvi aanika dhuluma maofisa mikopo benki

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Waziri huyo ameeleza jinsi ofisa mikopo wa benki moja jijini Dar es Salaam, alivyojipatia nyumba tano kutokana na kudhulumu wateja.

Alikuwa akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huduma ya utoaji mikopo ya muda mrefu ya ujenzi wa nyumba inayoitwa ‘Nyanyua Mjengo, inayotolewa na benki ya NMB.

Alisema kuna baadhi ya benki kwa kushirikiana na madalali matapeli wanawaibia wananchi na kuuza nyumba zao kwa mnada pasipo kufuata taratibu.

“Kuna ofisa mmoja wa benki ambaye anamiliki nyumba tano, zote amezipata kwa njia ya udanganyifu kwa kuwapora watu kwa kigezo cha wamiliki wake kushindwa kulipa,” alisema.

Alisema maofisa hao wanapotoa mikopo kwa wateja wao, wanasubiri ndani ya mwaka mmoja kisha wanafuata madalali ambao wanakwenda kupiga mnada mali iliyowekwa dhamana kwa madai ya kushindwa kulipa deni.

Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, serikali imegundua jambo hilo na kuwaonya watu wanaondesha mtandao huo kuacha mara moja.

“Watu hawa maskini wanakopa kwa ajili ya kuhakikisha wanapata angalau nyumba za kuishi, inapotumika hila ili kumfilisi kwa kuchukua nyumba yake haikubaliki kamwe,” alisema.

Aliipongeza uongozi wa benki ya NMB kwa kubuni na kuanzisha huduma hiyo (Ya Mikopo) ambayo alielezea ni mwarobaini wa wananchi wa ngazi zote kupata nyumba zenye ubora.

Alisema kuna watu zaidi ya milioni moja ambao wanamiliki hati ya viwanja, na kama NMB itaweza kuwafikia kutaleta mabadiliko katika upangaji na uboreshaji wa miji nchini.

“NMB ndiyo benki pekee nchini ambayo imeanza kutoa mikopo ya muda mrefu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba, nashauri kuongeza juhudi na mikakati ya kuwafikia watu wengi zaidi ili kuwapo na nyumba nyingi zenye ubora,” aliongeza.

Awali, Ofisa Mkuu wa Mteja Binafsi, Biashara ndogo na kati, Filbert Mponzi, alisema kwa kushirikiana na Taasisi ya Mikopo ya Nyumba Tanzania (TMRC), benki yake itatoa mikopo yenye riba ya asilimia 17 kwa watu watakaotaka kujenga nyumba za kisasa.

Alisema mkopo huo utaanzia Sh. milioni 10 hadi 200, na kuwa itawalenga wafanyakazi wa serikali na wajasiriamali wenye hati ya viwanja na wameshindwa kujenga makazi yao.

“Huduma hii itampa nafasi mteja kulipa deni kwa unafuu zaidi wakati anaendelea kuishi ndani ya nyumba yake na kuendesha shughuli zake bila hofu,” alifafanua Mponzi.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa NMB, Ruth Zaipuna, aliahidi benki hiyo yake itaendelea kushirikiana na serikali katika utoaji wa huduma hiyo mpaka idadi kubwa ya Watanzania watakapomiliki makazi yao.

Chanzo: Nipashe
 
And I Quote [“Huduma hii itampa nafasi mteja kulipa deni kwa unafuu zaidi wakati anaendelea kuishi ndani ya nyumba yake na kuendesha shughuli zake bila hofu,” alifafanua Mponzi.

1. Unafuu ni pale ambapo mteja atakuwa na uwezo wa kurudisha deni kwa kipindi kifupi. Maumivu kwenye mikopo ni pale muda wa marejesho unapofanywa kwa muda mrefu though mkopaji anaweza akahisi unafuu kwa kuona kiasi atakachorejesha let's say kwa kila mwezi ni kidogo.

2. Riba ya 17% bado iko juu sana na sio ngeni kwenye mikopo ya kawaida sema tuu hapa imekuwa reflected kwa msisitizo wa MKOPO WA UJENZI WA NYUMBA.
 
Lukuvi malizia swala la viwanja kwanza huku kwenye mikopo baadae
Kimara Goba Mbezi Mwisho Makongo mtamaliza lini kuwapa wananchi hati kila siku longalonga mara serikali za mitaa mara ardhi mara wizarani mnatuchosha mjue
 
Waziri huyo ameeleza jinsi ofisa mikopo wa benki moja jijini Dar es Salaam, alivyojipatia nyumba tano kutokana na kudhulumu wateja.

Alikuwa akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huduma ya utoaji mikopo ya muda mrefu ya ujenzi wa nyumba inayoitwa ‘Nyanyua Mjengo, inayotolewa na benki ya NMB.

Alisema kuna baadhi ya benki kwa kushirikiana na madalali matapeli wanawaibia wananchi na kuuza nyumba zao kwa mnada pasipo kufuata taratibu.

“Kuna ofisa mmoja wa benki ambaye anamiliki nyumba tano, zote amezipata kwa njia ya udanganyifu kwa kuwapora watu kwa kigezo cha wamiliki wake kushindwa kulipa,” alisema.

Alisema maofisa hao wanapotoa mikopo kwa wateja wao, wanasubiri ndani ya mwaka mmoja kisha wanafuata madalali ambao wanakwenda kupiga mnada mali iliyowekwa dhamana kwa madai ya kushindwa kulipa deni.

Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, serikali imegundua jambo hilo na kuwaonya watu wanaondesha mtandao huo kuacha mara moja.

“Watu hawa maskini wanakopa kwa ajili ya kuhakikisha wanapata angalau nyumba za kuishi, inapotumika hila ili kumfilisi kwa kuchukua nyumba yake haikubaliki kamwe,” alisema.

Aliipongeza uongozi wa benki ya NMB kwa kubuni na kuanzisha huduma hiyo (Ya Mikopo) ambayo alielezea ni mwarobaini wa wananchi wa ngazi zote kupata nyumba zenye ubora.

Alisema kuna watu zaidi ya milioni moja ambao wanamiliki hati ya viwanja, na kama NMB itaweza kuwafikia kutaleta mabadiliko katika upangaji na uboreshaji wa miji nchini.

“NMB ndiyo benki pekee nchini ambayo imeanza kutoa mikopo ya muda mrefu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba, nashauri kuongeza juhudi na mikakati ya kuwafikia watu wengi zaidi ili kuwapo na nyumba nyingi zenye ubora,” aliongeza.

Awali, Ofisa Mkuu wa Mteja Binafsi, Biashara ndogo na kati, Filbert Mponzi, alisema kwa kushirikiana na Taasisi ya Mikopo ya Nyumba Tanzania (TMRC), benki yake itatoa mikopo yenye riba ya asilimia 17 kwa watu watakaotaka kujenga nyumba za kisasa.

Alisema mkopo huo utaanzia Sh. milioni 10 hadi 200, na kuwa itawalenga wafanyakazi wa serikali na wajasiriamali wenye hati ya viwanja na wameshindwa kujenga makazi yao.

“Huduma hii itampa nafasi mteja kulipa deni kwa unafuu zaidi wakati anaendelea kuishi ndani ya nyumba yake na kuendesha shughuli zake bila hofu,” alifafanua Mponzi.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa NMB, Ruth Zaipuna, aliahidi benki hiyo yake itaendelea kushirikiana na serikali katika utoaji wa huduma hiyo mpaka idadi kubwa ya Watanzania watakapomiliki makazi yao.

Chanzo: Nipashe
HONGERA KWA WAZIR KUGUNDUA NA KUANIKA MBINU CHAFU ZA HAO MAOFISAA.

SASA LAKN KTK HIYO MIKOPO HAKUNA RIBAA??
 
Kitu kingine wanachofanya maofisa mikopo ni kwamba wanapoona mtu anasuasua kulipa mkopo na wakawa wameipenda dhamana ya muhusika iwe nyumba au kiwanja basi wanakula njama na madalali kufanya mnada wa kihuni wa harakaharaka na kuuza dhamana ya mdaiwa kwa bei ya chini sana na kisha wanaichukua wao au mnunuzi anawapoza kwani walishapanga!! Baada ya hapo mkopaji anaendelea kudaiwa eti pesa iliyopatikana kwa kumuuzia dhamana yake haijatosha kulipa mkopo wote!!! Wizi wa hali ya juu wa kitaasisi dhidi ya raia

Nasikia Waziri Lukuvi amepiga marufuku kuuza dhamana ya mdaiwa chini ya thamini iliyotathminiwa na bank(valution) kabda hawajatoa mkopo. Kama atafanya hivyo atakua amesimama upande wa wanyonge kweli
 
Back
Top Bottom