LUKU za kidijitali ni matumizi mabaya ya fedha

LUS0MYA

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
861
1,097
Kwa mara nyingine tena TANESCO inajiingiza katika gharama zisizo za lazima kwa kutaka kutekeleza mpango wa kubadilisha luku kuwa za kidigitali. Kama ilivyokuwa kwa kubadilisha nguzo za miti na kuweka nguzo za zege.

TANESCO itaondoa LUKU ambazo hazina matatizo yoyote kwa mteja auTANESCO na kuweka hizo mpya za kigitali wakati Tanesco ina madeni mengi na pia inashindwa kutekeleza miradi yake ikiwemo urekebishaji wa mifumo ya umeme na kuondoa ukatikaji wa umeme.

Nashauri uondoaji wa LUKU za zamani utegemee mahitaji binafsi ya mteja na ajigharamie mwenyewe kubadilisha LUKU na pia LUKU za kidigitali zitolewe kwa wateja wapya. Kubadilisha LUKU zote ambazo hazina tatizo lolote ni ubadhirifu na uchafuzi wa mazingira na sio kipaumbele cha tanesco wala matatizo yanayowakabili watumiaji.
 
Kwa mara nyingine tena Tanesco inajiingiza katika gharama zisizo za lazima kwa kutaka kutekeleza mpango wa kubadilisha luku kuwa za kidigitali...
Napendekeza watoe specifications ya mita ya LUKU iwe kama simu vile, zitengenezwe commercially. Wewe unanunua line (account) yako TANESCO buku tu mita unanunua kwa wauzaji mbali mbali mitaani.

Line hii inawezwa hata kuuzwa na machinga wanakusajili kwa alama za vidole, kazi imeisha. LUKU inakuwa na vikorombwezo mbali mbali kutegemea na bei yake.
 
Kwa mara nyingine tena Tanesco inajiingiza katika gharama zisizo za lazima kwa kutaka kutekeleza mpango wa kubadilisha luku kuwa za kidigitali.Kama ilivyokuwa kwa kubadilisha nguzo za miti na kuweka nguzo za zege...
Tunaheshim mawazo yako:

Lakini inaonekana huna ufaham wa faida zitokanazo na luku za digital! jipe muda ku study lengo lao! Utawashukuru sana!

Kongole kwa TANESCO, hakika unapokuwa popote ni unajaza tu bila kugusana na luku yenyewe! kama vocha tu!
 
Tunaheshim mawazo yako:

Lakini inaonekana huna ufaham wa faida zitokanazo na luku za digital! jipe muda ku study lengo lao! Utawashukuru sana!

Kongole kwa TANESCO, hakika unapokuwa popote ni unajaza tu bila kugusana na luku yenyewe! kama vocha tu!
Inawezekana wewe hujafahamu ninachokieleza...ukitengeneza mpango wa mabilioni kubadilisha mita za umeme wakati zilizopo hazina tatizo la kiufundi wakati unalalamika huna fedha za kukamilisha usambazaji wa umeme vijijini na pia unaongeza gharama za kuweka umeme inashangaza sana.

Hayo mabilioni ya kubadilisha mita ni afadhali yatumike kuweka ruzuku ili kupunguza gharama ya kuweka umeme majumbani na viwandani...kama Dawasco wakija nq mpango wa kuondoa mita za sasa za maji na kuleta za mfumo wa luku it make sense kwa sababu italeta impact ya moja kwa moja...
 
Huyu jamaa hajui kero zake, kuna muda umeme unakata afu ile mita ya kuwekea luku sehem ya betri mbovu unaanza gongea majirani. Hio ya digital ndo mpango mzima.
Unajua kuna mita ngapi za umeme chini ya TANESCO?na zinagharimu kiasi gani?hivi kweli Tanesco inaweza kujigamba kununua na kubadilisha mita zote za luku?kama mteja anahitaji kubadilisha basi gharama iwe ya mteja mwenyewe na siyo ya Tanesco...Tanesco ina vipaumbele vingi kuliko hiki.
 
Wabongo ni lawama kila kitu, hawana jema wala moja. Serikali iruhusu ndoa za jinsia moja watu kama watoa mada tuwaoe tu labda akili zao zitakuwa sawa.
Hizi sio lawama ni ushauri na siku zote ushauri haulazimishwi kama wanaona ni sawa waendelee na mpango...in short binafsi sioni sababu ya kubadilisha hizi Luku kwa gharama ya fedha za umma wakati hazina tatizo lolote.mteja binafsi na wateja wapya wanaweza kugharamia na kuweka mfumo mpya...
 
Kabla sijachangia naomba anayefaham hizo mita zitakuwa na uwezo wa kufanya kazi gani za ziada
Neno Digital nila ujumla sana. Tusijidanganye kuwa ikishakuwa digita basi itakuwa suluhisho la tunayotarajia; Tusipo kuwa makini hapo ndio tutapigwa kwa kutengenezewa specification za simu ya torchi ila digital


Huyu jamaa hajui kero zake, kuna muda umeme unakata afu ile mita ya kuwekea luku sehem ya betri mbovu unaanza gongea majirani. Hio ya digital ndo mpango mzima.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Kwa mara nyingine tena Tanesco inajiingiza katika gharama zisizo za lazima kwa kutaka kutekeleza mpango wa kubadilisha luku kuwa za kidigitali.

Kama ilivyokuwa kwa kubadilisha nguzo za miti na kuweka nguzo za zege.

Tanesco itaondoa luku ambazo hazina matatizo yoyote kwa mteja au Tanesco na kuweka hizo mpya za kigitali wakati Tanesco ina madeni mengi na pia inashindwa kutekeleza miradi yake ikiwemo urekebishaji wa mifumo ya umeme na kuondoa ukatikaji wa umeme.

Nashauri uondoaji wa luku za zamani utegemee mahitaji binafsi ya mteja na ajigharamie mwenyewe kubadilisha luku na pia luku za kidigitali zitolewe kwa wateja wapya. Kubadilisha luku zote ambazo hazina tatizo lolote ni ubadhirifu na uchafuzi wa mazingira na sio kipaumbele cha tanesco wala matatizo yanayowakabili watumiaji.
Tunazidi sana kulalamika.
Ivi kweli kuondoa nguo za miti ni matumizi mabaya ya pesa????
 
Tanesco wanachotakiwa Ni kuwaunganishia hawa wateja wapya alafu hawa wa zamani watazibadili kwa fetha zao maana hizo garama watakazo tumia kwa hizo mita ndo hilo bomu wanelitengeneza za watu wote karudishwa matumizi ya viwanda
 
Hizo za kidigitali ziratuwezesha kujaza umeme bila kuigusa mita Kama kutuma pesa' tu
 
Back
Top Bottom