LUKU: Mfumo wenye tija kwa wateja na TANESCO

TANESCO

Official Account
Jul 12, 2014
4,584
2,104
“LUKU ni aina ya mita zinazotumia mfumo rafiki kwa Mteja, zikitokana na Teknolojia mpya inayowezesha kuonekana kwa matumizi sahihi ya umeme yaani Lipa Umeme Kadiri Utumiavyo..”

Wakati Teknolojia hii inaanza hapa Nchini Mwaka 1995, Tanzania ilikuwa Nchi ya pili Barani Afrika kwa kutumia LUKU, ikitanguliwa na Afrika Kusini ambayo pia ilikuwa imeshaanza kutumia mfumo huu wa mpya wa lipa kadiri unavyotumia (pre-paid service)

Matumizi ya LUKU yalipoanza Tanzania, haikuwa kazi rahisi kuwashawishi Wateja kuachana na Mfumo wa awali wa kutumia mita za makadirio (Conventional Meters), kwani ndio mfumo ambao ulikuwa umezoeleka sana katika utoaji wa Huduma.

SABABU ZA KUINGIZA LUKU
Awali, matumizi ya LUKU yalianza kupitia mradi wa majaribio (Pilot Study) Mkoa wa Kinondoni Kaskazini ambao kwa sasa ni maarufu kama Mikocheni, kwa mujibu wa mgawanyo wa Kikanda wa TANESCO.

Kampuni ya Actaris ya Afrika Kusini ndio iliyofanya majaribio ya mradi huo wa ufungaji wa mita ambazo zilijulikana kama mita za Magnetiki (Magnetic meters).

Mita hizo zilikuwa katika mfumo unaojulikana kwa kiingereza (offline mode). Huu ni mfumo wa zamani ambao unagawanyisha eneo la mfumo (data base) na lile ambalo mfumo unafungwa.

Kwa maana hiyo, mnunuzi na muuzaji hawako katika eneo moja ili kutoa Huduma ya LUKU. Mmoja analazimika kuwepo Mashariki na mwingine Magharibi lakini wanaunganishwa na mfumo mmoja ili kuweza kutoa Huduma kwa kila mmoja.

Mfumo huu ulikuwa unafanya kazi maeneo husika yaliyoainishwa kama ya majaribio, ambapo Mteja anapotaka kununua LUKU ni lazima afike kwenye Kituo husika kinachouza umeme wa LUKU kwa njia ya kadi husika.

Mwisho wa siku Data zote zilizofanywa wakati wa mauzo zilichukuliwa na watu maalumu ambao walikuwa wanapita nyakati za jioni kuzichukua, jambo ambalo ni gumu katika utendaji wa kazi za kila siku.

UFANISI WA LUKU

Mwaka 1996, TANESCO ilibaini ufanisi uliotokana na matumizi ya LUKU hivyo kuongeza mtandao wa matumizi yake. kati ya Mwaka 2004 hadi 2005, Kampuni ya Conlog ya Afrika Kusini ilipewa dhamana ya kusimamia uendelezaji wa mifumo ya matumzi ya LUKU (Upgrading of the system).

Hivyo ilianza kwa usambazaji wa mita za LUKU jijini Dar es Salaam na baadaye Kampuni ya Actaris ikazisambaza kwa Mikoa mingine. Lengo kubwa la ufungaji wa mita za LUKU ni kuongeza mapato ya TANESCO yanayotokana na makusanyo ya ankara za Wateja.

Hali hiyo inalenga pia kuondokana na mfumo wa kukusanya mapato baada ya matumizi ya Nishati hiyo.

Mfumo huu ulikuwa hauleti Tija sana kwa TANESCO kwa sababu si Wateja wote walikuwa waaminifu ama kuwa tayari kulipia gharama za umeme kwa kadiri walivyotumia.

Wateja wengine walikuwa hawakubaliani kabisa na gharama halisi walizokuwa wanatakiwa kuzilipia kwa madai zilikuwa kubwa na hazikuwa halisi bali makadirio.

MIAKA 10 YA MAJARIBIO

Unaweza kujiuliza mbona miaka 10 kwa majaribio ni mingi? Muda huo ulitokana na sababu kuwa TANESCO ilikuwa inahitaji kujiridhisha na aina ya Kampuni pamoja na huduma na uwezo wa huduma kwa Wananchi, ndio maana ilikaa muda mrefu bila kuanza kusambaza LUKU maeneo yote.

Kazi kubwa ambayo TANESCO ilifanya ni kuanza kuweka maeneo ya kuuzia LUKU (Offline mode), kuweka maeneo ambayo yatatumika kwa ajili ya mauzo katika vituo na mauzo.

Wakati huo ulikuwa huwezi kwenda kununua umeme sehemu nyingine yoyote bali palipohusika ili kupata kadi ya kulipia nishati hiyo na kwenda kuweka kwenye mita yako.

Mwaka 2008 baada ya kuuzwa kwa hisa za Kampuni ya awali iliyoweka mifumo ya LUKU ya Actaris, Kampuni ya Eclipse ya Afrika Kusini, iliboresha mfumo wa LUKU kutoka wa awali wa kutumia mita za magnetiki (Magnetic meters) kuwa za kurasimisha mifumo ya uuzaji wa LUKU (central monitoring system).

MABORESHO

Hivi sasa kumefanyika maboresho makubwa katika mifumo inayotumika katika ununuzi wa LUKU, upatikanaji wa LUKU na hata mauzo ya LUKU mahali popote na kuruhusu mfumo huria wa Wateja kununua na kuuza LUKU mahali popote.

Mfumo huu umekuwa ni mkombozi mpaka sasa kutokana na ufanisi uliopo kwenye mifumo iliyowekwa ya kuruhusu Mteja kuuza, kununua na kupata huduma mahali popote.

Aidha, Mfumo huu uliruhusu mabadiliko ya matumizi ya mita za LUKU ambazo zilikuwa ni lazima ziendane na mifumo iliyowekwa badala ya mita za zamani za magnetiki zilizokuwa zinatumika.

Licha ya kuanza kutumika kwa mfumo huu, bado yako baadhi ya maeneo ambapo Wateja wanatumia mita za LUKU zinazotumia mfumo wa magnetiki. Matamanio ya TANESCO ni kuondokana kabisa na mita hizo katika mfumo wa sasa ambao umerasimisha kila kitu na kuwa katika mwamvuli mmoja.

UUZAJI NA USAMBAZAJI

Mwaka 2009 TANESCO ilifanya mabadiliko mengine kwa kuongeza washirika wengi zaidi katika uuzaji na usambazaji wa LUKU, ilisaini mkataba na wauzaji binafsi ambao sasa ni sehemu ya kusaidia mauzo ya LUKU katika vituo mbalimbali vinavyotoa huduma hapa Nchini.

Mwaka mmoja baadaye ikaongezwa Kampuni ya E-Fulusi ili kutanua wigo wa mauzo ya LUKU kwa Sellcom na watoa Huduma za simu za mkononi kama Airtel, Vodacom na Tigo. Zantel haikuwa kwenye mfumo wa mauzo.

Kupitia mfumo huo ndipo mabadiliko makubwa ya matumizi, uuzaji, ongezeko la wateja na kuimarika kwa huduma za LUKU Nchini na Mikoani kwa ujumla vinaonekana.

Ongezeko hilo la wateja linakwenda sanjari na ongezeko la makusanyo ambapo kwa Takwimu za 2008-2009, wateja waliokuwa wanatumia mfumo wa LUKU walifikia 400 na idadi hiyo iliendelea kuongezeka hadi kufikia 600,000 mwaka 2011.

Mfumo wa LUKU umeleta mafanikio makubwa na umesaidia sana kuleta tija na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi licha ya kuwapo changamoto ya ongezeko la idadi ya wateja wanaotumia huduma za mifumo ya LUKU.

Mnamo Mwaka 2015 TANESCO ilifanya mabadiliko katika mfumo wake wa LUKU kutoka Mfumo ujulikanao kama Eclipse Manager kwenda Mfumo mpya wa mauzo ya LUKU ujulikanao 3E (Eclipse Enterprise Edition). Awali, kabla ya kuingia katika Mfumo mpya TANESCO ilifanya upembuzi yakinifu kupata Kampuni itakayokidhi vigezo na itakayoweza kusaidia kuupa nguvu mfumo wa awali wa LUKU uliokuwa ukihitaji kuongezewa uwezo. Baadhi ya changamoto zilizopelekea kubadilishwa kwa Mfumo wa awali ni kutokana na Mfumo huo kuwa na uwezo mdogo wa kuongeza idadi ya Wateja, Aidha, ilikuwa na Kanzi Data (Data Base) mbalimbali na pia Wahasibu walikuwa na uwezo wa kuona na kufanya mabadiliko kwa Mteja katika Mfumo Nchi nzima.

Ni ukweli usiopingika kuwa Mfumo huu mpya wa 3E umeyatatua matatizo hayo yote kwani umezingatia kwa kiasi kikubwa uwezo wa kubeba mzigo katika kuhudumia Wateja wengi Zaidi wanaotumia Huduma ya LUKU. Aidha, Mfumo huu umeondoa Mita za (Magnetic) ambazo zilikuwa zimepitwa na wakati na zilikuwa zimefikia kikomo.

Unaweza kuwa na mfumo mzuri na wa haraka, lakini swali lingine la kujiuliza ni je, kwa kiasi gani Wananchi wamehamasika juu ya matumizi ya LUKU? Wakati Mfumo huu wa 3E unatumika, TANESCO inaendelea kutoa elimu kwa Wateja wake juu ya matumizi sahihi ya ununuzi na matumizi ya Mita za LUKU na umeme kwa ujumla. Wateja wengi wanaotumia Huduma ya LUKU wamepata fursa ya kufahamu aina mbalimbali za Mita ambazo wamefungiwa majumbani kwao na namna ambavyo zinafanya kazi.

Dunia ya sasa hivi ni ya ushindani mkubwa sana hususani katika masuala ya Teknolojia na TANESCO haijaachwa nyuma katika uboreshaji wa Mifumo yake ya TEHAMA. Afisa Mwandamizi Kitenngo cha Mita Mhandisi Ruti Misana akionesha namna Mita zinavyofanyiwa majaribio kabla ya kufungwa kwa Mteja.
 
Nahitaji kufunga meter ya luku ya matumizi ya peke yangu sehemu niliyopanga ili niachane na meter na wapangaji wengine natakiwa kufuata hatua zipi na gharama ya meter ni sh ngapi? TANESCO
 
Hongereni TANESCO hakika sasa mteja anaona thamani ya pesa yake,ila nawapa changamoto kuwe na utaratibu wa hata sms wa kutoa taarifa ya kukata umeme. Kama mmeweza kuwa na data base ya wateja nchi nzima naamini hamshndwi kuwa na namba za wateja wenu nchi nzima, pale panapokua na tatizo mnatoa taarifa hata sms mtu anajua muda fulani umeme utakatika au utarudi muda fulani.
 
Ila mtandao wenu ukipandwa na malaria inapanda kweli kweli

Ova
 
Nimefungiwa umeme tarehe 21.04.18 nikapewa unit 10 za mkopo then nikaambiwa nikishasajiliwa na kulipia izo unit 10 nitapewa unit 50 za kuanzia nimezilipia izo unit 10 Kama sh 18000 Jana. Kiujumla nililipa 20000
Wakata 17,812 ya Deni then 1793 wakanipa unit 6,2( jumla nikawa na unit 14hv) cha kushangaza zile unit 50 sijaziona Adi Leo!!
 
Kwa shirika la Umeme Tanzania,naomba kuwasilisha ulizo au ombi la msaada kutoka kwenu,mimi ni mteja wenu wa muda nina tatizo kwenye luku yangu, buttons/vitufe vya number havifanyi kazi hivyo nashidhwa kuingiza token number na nimebakiwa na unit 0.4 wakati token za kuongeza ninazo.

Swali langu ni je kuna njia nyingine mbala ya kuongeza unit wakati nasubiria mafundi kurekebisha hili tatizo maana naona siku zinasonga pasipo matumaini yoyote.
 
Nadhani aliweka mada hii ni mtu wa Tanesco. Ingekuwa vizuri, kama wauliza maswali ambao, baadhi ni wateja wenu, na wengine ni wateja watarijwa.
Ingekuwa vizuri maswali, kwa wakati, ingewafaidisha wengi.
 
Ni wazi kabisa hawa jamaa wako usinginizi maana hata ukiangalia ujibuji wao wa maswali ni mbovu kabisa......hii ni poor customer care,mtu anaweka swali toka April 28,2018 lakini majibu au hata kusema tunashughulikia swala lako hakuna.....wako kimya sasa tunawaelewaje hawa?????.....TANESCO ACHENI KUKERA WATEJA WENU.
 
“LUKU ni aina ya mita zinazotumia mfumo rafiki kwa Mteja, zikitokana na Teknolojia mpya inayowezesha kuonekana kwa matumizi sahihi ya umeme yaani Lipa Umeme Kadiri Utumiavyo..”

Wakati Teknolojia hii inaanza hapa Nchini Mwaka 1995, Tanzania ilikuwa Nchi ya pili Barani Afrika kwa kutumia LUKU, ikitanguliwa na Afrika Kusini ambayo pia ilikuwa imeshaanza kutumia mfumo huu wa mpya wa lipa kadiri unavyotumia (pre-paid service)

Matumizi ya LUKU yalipoanza Tanzania, haikuwa kazi rahisi kuwashawishi Wateja kuachana na Mfumo wa awali wa kutumia mita za makadirio (Conventional Meters), kwani ndio mfumo ambao ulikuwa umezoeleka sana katika utoaji wa Huduma.

SABABU ZA KUINGIZA LUKU
Awali, matumizi ya LUKU yalianza kupitia mradi wa majaribio (Pilot Study) Mkoa wa Kinondoni Kaskazini ambao kwa sasa ni maarufu kama Mikocheni, kwa mujibu wa mgawanyo wa Kikanda wa TANESCO.

Kampuni ya Actaris ya Afrika Kusini ndio iliyofanya majaribio ya mradi huo wa ufungaji wa mita ambazo zilijulikana kama mita za Magnetiki (Magnetic meters).

Mita hizo zilikuwa katika mfumo unaojulikana kwa kiingereza (offline mode). Huu ni mfumo wa zamani ambao unagawanyisha eneo la mfumo (data base) na lile ambalo mfumo unafungwa.

Kwa maana hiyo, mnunuzi na muuzaji hawako katika eneo moja ili kutoa Huduma ya LUKU. Mmoja analazimika kuwepo Mashariki na mwingine Magharibi lakini wanaunganishwa na mfumo mmoja ili kuweza kutoa Huduma kwa kila mmoja.

Mfumo huu ulikuwa unafanya kazi maeneo husika yaliyoainishwa kama ya majaribio, ambapo Mteja anapotaka kununua LUKU ni lazima afike kwenye Kituo husika kinachouza umeme wa LUKU kwa njia ya kadi husika.

Mwisho wa siku Data zote zilizofanywa wakati wa mauzo zilichukuliwa na watu maalumu ambao walikuwa wanapita nyakati za jioni kuzichukua, jambo ambalo ni gumu katika utendaji wa kazi za kila siku.

UFANISI WA LUKU

Mwaka 1996, TANESCO ilibaini ufanisi uliotokana na matumizi ya LUKU hivyo kuongeza mtandao wa matumizi yake. kati ya Mwaka 2004 hadi 2005, Kampuni ya Conlog ya Afrika Kusini ilipewa dhamana ya kusimamia uendelezaji wa mifumo ya matumzi ya LUKU (Upgrading of the system).

Hivyo ilianza kwa usambazaji wa mita za LUKU jijini Dar es Salaam na baadaye Kampuni ya Actaris ikazisambaza kwa Mikoa mingine. Lengo kubwa la ufungaji wa mita za LUKU ni kuongeza mapato ya TANESCO yanayotokana na makusanyo ya ankara za Wateja.

Hali hiyo inalenga pia kuondokana na mfumo wa kukusanya mapato baada ya matumizi ya Nishati hiyo.

Mfumo huu ulikuwa hauleti Tija sana kwa TANESCO kwa sababu si Wateja wote walikuwa waaminifu ama kuwa tayari kulipia gharama za umeme kwa kadiri walivyotumia.

Wateja wengine walikuwa hawakubaliani kabisa na gharama halisi walizokuwa wanatakiwa kuzilipia kwa madai zilikuwa kubwa na hazikuwa halisi bali makadirio.

MIAKA 10 YA MAJARIBIO

Unaweza kujiuliza mbona miaka 10 kwa majaribio ni mingi? Muda huo ulitokana na sababu kuwa TANESCO ilikuwa inahitaji kujiridhisha na aina ya Kampuni pamoja na huduma na uwezo wa huduma kwa Wananchi, ndio maana ilikaa muda mrefu bila kuanza kusambaza LUKU maeneo yote.

Kazi kubwa ambayo TANESCO ilifanya ni kuanza kuweka maeneo ya kuuzia LUKU (Offline mode), kuweka maeneo ambayo yatatumika kwa ajili ya mauzo katika vituo na mauzo.

Wakati huo ulikuwa huwezi kwenda kununua umeme sehemu nyingine yoyote bali palipohusika ili kupata kadi ya kulipia nishati hiyo na kwenda kuweka kwenye mita yako.

Mwaka 2008 baada ya kuuzwa kwa hisa za Kampuni ya awali iliyoweka mifumo ya LUKU ya Actaris, Kampuni ya Eclipse ya Afrika Kusini, iliboresha mfumo wa LUKU kutoka wa awali wa kutumia mita za magnetiki (Magnetic meters) kuwa za kurasimisha mifumo ya uuzaji wa LUKU (central monitoring system).

MABORESHO

Hivi sasa kumefanyika maboresho makubwa katika mifumo inayotumika katika ununuzi wa LUKU, upatikanaji wa LUKU na hata mauzo ya LUKU mahali popote na kuruhusu mfumo huria wa Wateja kununua na kuuza LUKU mahali popote.

Mfumo huu umekuwa ni mkombozi mpaka sasa kutokana na ufanisi uliopo kwenye mifumo iliyowekwa ya kuruhusu Mteja kuuza, kununua na kupata huduma mahali popote.

Aidha, Mfumo huu uliruhusu mabadiliko ya matumizi ya mita za LUKU ambazo zilikuwa ni lazima ziendane na mifumo iliyowekwa badala ya mita za zamani za magnetiki zilizokuwa zinatumika.

Licha ya kuanza kutumika kwa mfumo huu, bado yako baadhi ya maeneo ambapo Wateja wanatumia mita za LUKU zinazotumia mfumo wa magnetiki. Matamanio ya TANESCO ni kuondokana kabisa na mita hizo katika mfumo wa sasa ambao umerasimisha kila kitu na kuwa katika mwamvuli mmoja.

UUZAJI NA USAMBAZAJI

Mwaka 2009 TANESCO ilifanya mabadiliko mengine kwa kuongeza washirika wengi zaidi katika uuzaji na usambazaji wa LUKU, ilisaini mkataba na wauzaji binafsi ambao sasa ni sehemu ya kusaidia mauzo ya LUKU katika vituo mbalimbali vinavyotoa huduma hapa Nchini.

Mwaka mmoja baadaye ikaongezwa Kampuni ya E-Fulusi ili kutanua wigo wa mauzo ya LUKU kwa Sellcom na watoa Huduma za simu za mkononi kama Airtel, Vodacom na Tigo. Zantel haikuwa kwenye mfumo wa mauzo.

Kupitia mfumo huo ndipo mabadiliko makubwa ya matumizi, uuzaji, ongezeko la wateja na kuimarika kwa huduma za LUKU Nchini na Mikoani kwa ujumla vinaonekana.

Ongezeko hilo la wateja linakwenda sanjari na ongezeko la makusanyo ambapo kwa Takwimu za 2008-2009, wateja waliokuwa wanatumia mfumo wa LUKU walifikia 400 na idadi hiyo iliendelea kuongezeka hadi kufikia 600,000 mwaka 2011.

Mfumo wa LUKU umeleta mafanikio makubwa na umesaidia sana kuleta tija na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi licha ya kuwapo changamoto ya ongezeko la idadi ya wateja wanaotumia huduma za mifumo ya LUKU.

Mnamo Mwaka 2015 TANESCO ilifanya mabadiliko katika mfumo wake wa LUKU kutoka Mfumo ujulikanao kama Eclipse Manager kwenda Mfumo mpya wa mauzo ya LUKU ujulikanao 3E (Eclipse Enterprise Edition). Awali, kabla ya kuingia katika Mfumo mpya TANESCO ilifanya upembuzi yakinifu kupata Kampuni itakayokidhi vigezo na itakayoweza kusaidia kuupa nguvu mfumo wa awali wa LUKU uliokuwa ukihitaji kuongezewa uwezo. Baadhi ya changamoto zilizopelekea kubadilishwa kwa Mfumo wa awali ni kutokana na Mfumo huo kuwa na uwezo mdogo wa kuongeza idadi ya Wateja, Aidha, ilikuwa na Kanzi Data (Data Base) mbalimbali na pia Wahasibu walikuwa na uwezo wa kuona na kufanya mabadiliko kwa Mteja katika Mfumo Nchi nzima.

Ni ukweli usiopingika kuwa Mfumo huu mpya wa 3E umeyatatua matatizo hayo yote kwani umezingatia kwa kiasi kikubwa uwezo wa kubeba mzigo katika kuhudumia Wateja wengi Zaidi wanaotumia Huduma ya LUKU. Aidha, Mfumo huu umeondoa Mita za (Magnetic) ambazo zilikuwa zimepitwa na wakati na zilikuwa zimefikia kikomo.

Unaweza kuwa na mfumo mzuri na wa haraka, lakini swali lingine la kujiuliza ni je, kwa kiasi gani Wananchi wamehamasika juu ya matumizi ya LUKU? Wakati Mfumo huu wa 3E unatumika, TANESCO inaendelea kutoa elimu kwa Wateja wake juu ya matumizi sahihi ya ununuzi na matumizi ya Mita za LUKU na umeme kwa ujumla. Wateja wengi wanaotumia Huduma ya LUKU wamepata fursa ya kufahamu aina mbalimbali za Mita ambazo wamefungiwa majumbani kwao na namna ambavyo zinafanya kazi.

Dunia ya sasa hivi ni ya ushindani mkubwa sana hususani katika masuala ya Teknolojia na TANESCO haijaachwa nyuma katika uboreshaji wa Mifumo yake ya TEHAMA. Afisa Mwandamizi Kitenngo cha Mita Mhandisi Ruti Misana akionesha namna Mita zinavyofanyiwa majaribio kabla ya kufungwa kwa Mteja.
Mita zinazo tumia remoti zinatesa. Ukiwa mbali na ukaletewa taarifa ya kwisha umeme, ni lazima urudi, remoti lazima itunzwe secure. Inaaminika zililetwa kuzuia kuharibiwa na vishoka. Ushauri: kwenye next g, mita zinazopokea token kama simu itapendeza.
 
Nimefungiwa umeme tarehe 21.04.18 nikapewa unit 10 za mkopo then nikaambiwa nikishasajiliwa na kulipia izo unit 10 nitapewa unit 50 za kuanzia nimezilipia izo unit 10 Kama sh 18000 Jana. Kiujumla nililipa 20000
Wakata 17,812 ya Deni then 1793 wakanipa unit 6,2( jumla nikawa na unit 14hv) cha kushangaza zile unit 50 sijaziona Adi Leo!!
Mkuu inagawa mada ina muda ila ilikuwaje 10units ulipie shs 17,812?
 
leo watu wananunua luku pesa inatoka lakn token hazirud .mwish tunaambiwa mtandao amn tunaomb mtuambie tujue shid iko wap
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom