Luku haipatikani tena

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Hivi kuna serikali kweli luku haipatikani tena leo.

Kwanini luku haipatikani tena Rais chukua hatua acha kuchekea watu

Toka asubuhi luku haipatikani waziri wa nishati yupo ofisini.

====

KUPITIA MITANDAO YAKE YA KIJAMII, TANESCO IMEANDIKA:

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA MANUNUZI YA LUKU

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi wateja wake kutokana na kukosekana kwa huduma ya manunuzi ya umeme wa LUKU siku ya leo, Juni 7, 2021 na kusababisha baadhi ya wateja kushindwa kununua umeme.

Sababu: Hitilafu iliyobainika wakati wa maboresho yanayoendelea katika mfumo wa manunuzi ya LUKU.

Huduma inatarajiwa kurejea leo, saa 12 jioni.

Tunaomba uvumilivu wakati wataalamu wetu wakiendelea na kazi kuhakikisha huduma inarejea.

Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza
 
Za jion wadau nyie mnanunuaje umeme ndugu zsngu mm nimejaribu kila mahali inashindikana ndugu zangu km kuna aliyefanikiwa aniambie kanunua umeme kupitia nn akafanikiwa!!!
 
Wasiishie tu kuchukuliwa hatua bali kuanzia waziri na watendaji wote wa Tanesco wanaohusika na mfumo wa Luku wawajibishwe haiwezekani tatizo lilelile kujirudia kila mara bila hatua kali kuchukuliwa
 
Wasiishie tu kuchukuliwa hatua bali kuanzia waziri na watendaji wote wa Tanesco wanaohusika na mfumo wa Luku wawajibishwe haiwezekani tatizo lilelile kujirudia kila mara bila hatua kali kuchukuliwa
Ndugu yangu mambo ya mifumo ni mambo ya kisayansi yanahitaji majibu ya kisayansi kwa namna yoyote ile tatizo letu Kila kitu tunataka tuingize siasa juzi tu shida ilitokea Leo imerudi tena hapo hao wataalamu wa mifumo wanatakiwa watuambie shida ni nini lakini ukiomba watu watimuliwe tu hata hao watawekwa wapya huenda kabla hawajamaliza kulijua jengo lao vizuri nao wakatolewa.
 
Niju
Rais asipokuwa mkali atachezewa sana, na huu udhaifu wake ndio utafanya achukiwe, kazi kwake, hii nchi kuna watu bila viboko hawaendi.
Nijuavyo Mimi ni kuwa matamanio ya kumkwamisha yanaratibiwa na waliokwamia kwenye awamu yao pendwa na muda sii mrefu tutawatangaza kama maadui wa taifa letu pendwa Tanzania.
 
Kuanzia waziri,bodi na menejimenti yote ya TANESCO watimuliwe bila hivyo tatizo litaendelea kujirudia wale wote ni masalia wa jiwe.
Ni kweli hapa inaonyesha kuna shida,na shida yenyewe ni organised.Kwa mtazamo ni wapinga mabadiliko,mbaya zaidi wanashindwa kujua mabadiliko haya ni ambayo hayakutarajiwa ama kutegemewa,hivyo wasiokuwa flexible ni janga katika kupiga hatua.
 
Back
Top Bottom