Lukaku ataka jezi iliyowaponza wengi Chelsea

Alvajumaa

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
4,953
6,071
LUKAKU ATAKA JEZI ILIYOWAPONZA WENGI CHELSEA

LONDON, ENGLAND. WAKATI Romelu Lukaku anatua Stamford Bridge akirudi kuichezea Chelsea kwa awamu ya pili, kwenye tovuti ya Ligi Kuu England, aliorodheshwa kuwa atavaa jezi yenye Namba 18.

Lakini, wengi waliamini namba hiyo ingegawanyika kwa mbili kwa sababu, mchezaji aliyekuwa akivaa Namba 9 kwenye kikosi hicho, Tammy Abraham alikuwa anahusishwa na mpango wa kuondoka.

Hatimaye, Abraham ametimkia zake AS Roma na kuiacha Namba 9 ikiwa wazi jambo ambalo moja kwa moja atakwenda kuivaa straika wa Kibelgiji, Lukaku.

Lakini, wataalamu wa mambo wanamwambia Lukaku aendelee tu kuvaa jezi Namba 18 kwa sababu Namba 9 kwenye kikosi cha Chelsea inadaiwa kuwa ina gundu.

Kuna mastaa kibao waliowahi kuvaa jezi Namba 9 kwenye kikosi hicho cha Stamford Brigde ama walijikuta wakiwa kwenye viwango vya hovyo au kuishia tu kukaa benchi kama ilivyotokea kwa mtu wa mwisho wa kuivua, Abraham.

Cheki hapa kilichotokea kwa mastaa waliovaa jezi Namba 9 kwenye kikosi cha Chelsea na kutuma ujumbe kwa Lukaku anapaswa kujipanga kabla ya kuingia uwanjani.

Chris Sutton – mechi 39, bao 1

Msimu wa wa 1999-2000, kwenye kikosi cha Chelsea mchezaji aliyekuwa akivaa jezi Namba 9, alikuwa Chris Sutton. Hakuna, ambaye hakuwa anafahamu uwezo wa kufunga wa mchezaji huyo, lakini akiwa na jezi hiyo kwenye kikosi hicho cha Stamford Bridge, aliishia kufunga bao moja tu katika mechi 39.

Mateja Kezman –

mechi 41, bao 7

Chelsea ililipa Pauni 5 milioni kunasa saini ya straika Mateja Kezman, aliyekuwa moto wa kuotea mbali kwa kupachika mipira nyavuni huko PSV. Alitua zake Chelsea mwaka 2004, akiwa na jezi Namba 9, Mateja alikomea kufunga mabao saba tu katika mechi 41 alizochezea timu hiyo katika msimu wa 2004-05.

Khalid Boulahrouz – mechi 20, bao 0

Wanasema mabeki hawaruhusiwi kuvaa jezi Namba 9. Lakini, Khalid Boulahrouz wakati anatua Chelsea akitokea Hamburg kwa uhamisho wa Pauni 7 milioni aliamua kuvaa jezi Namba 9, ambayo inadaiwa kumtia gundu tu mchezaji huyo. Kwenye mechi 20, Boulahrouz hajafunga bao lolote, aliishia kujifunga tu na kukaa benchi akionekana kuwa na kiwango cha hovyo. Alipohama, mambo yalikuwa safi kwake.

Steve Sidwell – mechi 25, bao 1

Chelsea ilimnasa bure Steve Sidwell kutoka Reading mwaka 2007. Baada ya kutua Stamford Bridge, Sidwell alichukua Namba 9, ambayo hakika ilikuwa na mkosi kwa upande wake, akifunga bao moja tu katika mechi 25, huku sehemu kubwa mechi hizo akiwa anatolewa au kuingia kutokea benchi. Maisha yalipokuwa magumu sana aliuzwa kwenda Aston Villa kwa ada ya Pauni 5 milioni mwaka 2008.

Franco Di Santo – mechi 16, bao 0

Franco Di Santo alitua kwenye kikosi cha Chelsea mwaka 2008 kwa uhamisho wa Pauni 3 milioni akitokea Audax Italiano. Di Santo alijiunga na Chelsea akiwa na umri wa miaka 18 na hakupata nafasi yoyote ya kuanzishwa kwenye kikosi hicho, huku mechi zote 16 alizocheza alitokea benchi na jezi yake Namba 9 mgongoni na hakuna bao alilofunga. Alitolewa kwa mkopo kwenda Blackburn na baada ya hapo akauzwa jumla Wigan kwa ada ya Pauni 2 milioni mwaka 2010.

Fernando Torres – mechi 172, bao 45

Chelsea ilivunja benki kupata huduma ya Fernando Torres kwenye dirisha la Januari 2011, wakati ilipolipa Pauni 50 milioni kumnasa kutoka Liverpool. Ada hiyo kwa wakati hiyo ilivunja rekodi ya uhamisho England, lakini baada ya kutua Stamford Bridge mambo yalikuwa tofauti kabisa. Akiwa Liverpool, Torres alifunga mabao 81 katika mechi 142, lakini kwenye kikosi cha Chelsea akiwa na Namba 9 mgongoni, alifunga mabao 45 tu katika mechi 172. Akatolewa kwa mkopo kabla ya kuuzwa kabisa.

Radamel Falcao –

mechi 12, bao 1

Straika Falcao alitua Chelsea kwa mkopo wa msimu mzima akitokea AS Monaco mwaka 2015. Matumaini yalikuwa magumu wakati anatua Stamford Bridge, lakini alichokwenda kukifanya kwenye kikosi hicho hiyo kilichokuwa chini ya Jose Mourinho kilikuwa majanga makubwa. Akiwa na jezi Namba 9 mgongoni, mchango wa Falcao kwenye msimu wa 2014/15, alifunga bao moja tu kwenye mechi 12. Msimu ulipomalizika, akaachwa kurudi kwenye klabu yake ya Monaco, Ufaransa.

Alvaro Morata – mechi 48, bao 15

Antonio Conte akiwa Chelsea alifanya usajili wa Alvaro Morata akimnasa kwa Pauni 60 milioni kutoka Real Madrid. Baada ya kutua Stamford Bridge mwaka 2017, Morata alikabidhiwa jezi Namba 9 na hakika haikuwa nzuri kwa upande wake ndani ya uwanja, ambapo aliishia kufunga mabao 15 tu katika mechi 48. Walau, Morata alijitahidi kwa mabao hayo, akifunga pia hat-trick kwenye ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Stoke City.

Gonzalo Higuain – mechi 18, bao 5

Wakati Chelsea ikiwa chini ya kocha Maurizio Sarri ilinasa huduma ya Gonzalo Higuain kwa mkopo kutoka Juventus mwaka 2019. Hakuna ambaye hafahamu uwezo wa Higuain katika kufunga mabao na wakati anatua Stamford Bridge wengi waliamini kwamba makipa wa timu pinzani watakaokabiliana na The Blues watakuwa kwenye shida kubwa. Akachukua jezi Namba 9 akatinga na tangu hapo, akakosa maajabu kwenye kikosi hicho, akifunga mabao matano tu katika mechi 18.

Hernan Crespo –

mabao 13

Straika matata kabisa wa Kiargentina, Hernan Crespo alifunga mabao 13 tu katika msimu wake wa kwanza Chelsea, ambapo alinaswa kutoka Inter Milan kwa ada ya Pauni 16 milioni mwaka 2003. Kwa ubora wa Crespo kwa kipindi hicho na kuishia kufunga mabao 13 hakikuwa kiwango bora na matokeo yake, kocha Jose Mourinho aliamua kumwondoa kwenye kikosi chake akimpeleka kwa mkopo AC Milan na baadaye kwa mkopo Inter Milan na mkataba wake ulipofika mwisho 2008 akatemwa.
 
Lukaku kama vipi aachane tu na hiyo jezi. Asije akajikuta na yeye amekuwa kama hao watangulizi wake. Hiyo jezi itakuwa ina gundu kweli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom