Luhwavi, Membe na Lukuvi, mnayopanga Gizani ili Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM yawekwa Hadharani

Membe tulia kwa bwana wewe LOWASA milele na milele kamwe hamji kuwa maraisi WA nchi hii mmekataliwa Mbinguni na Tanzania yooote!! Makae kimya kwa jina LA Aliye juu!!! Jon pombe Magufuli hoyeeeeeeeee!!!! 100%

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo liko wapi hapo mkuu? Katiba yenu inamtaka alie Rais ndo awe mwenyekiti wenu sasa povu la nini hapo? nani asiejua kuwa magu ndo mwenyekiti ajae?

Umeandika herufi nyiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiingi bila mantiki...........liwake lisiwake Magu mwenyekiti sasa wewe unafichua nini?
 
Tengua kauli kusema lowasa aliangukia pua kwani nani asiejua kama hii nchi haina demokrasia ya kweli ila udikteta tuuu? Ni nani asiejua kama Kura za Edo zilifanyiwa figisufigisu? Acha ubabaishaji.
 
Siwezi kutengua kwani huo ndo uhalisia. Kwa haya makubwa anayofanya JPM kwa sasa hakika UKAWA itakufa kifo cha mende
 
Kidumu chama tawala
Siasa za makundi ziliathiri sana mfumo wa chama chetu.Waliokuwa na maamuzi ni wale waliokuwa na fedha hata kama hawana sifa za kuongoza chama.CCM mpya inayojali watu kwa sifa zao na si fedha zao naiona sasa.Magufuli apewe chama akifue na kukinyoosha kwa pasi ya umeme ili kuua kunguni wote.Waliozoea siasa za makundi wataisoma namba.
 
CCM hamna mwenye vision ya kulikomboa hili Taifa...unazuia mikutano ya kisiasa nn unaogopa kama utawala wako ni wa kidemokrasia.
 
Macc yote mapovu tu..hamna mwenye vision ya kulikomboa hili Taifa...unazuia mikutano ya kisiasa nn unaogopa kama utawala wako ni wa kidemokrasia.
Benki ya Exim ya China imekubali kutoa mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani Bilioni 7.6 sawa na zaidi ya Shilingi Trilioni 16 za kitanzania kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa mradi mkubwa wa reli ya kati hapa nchini kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) unaotarajiwa kuanza katika mwaka huu wa fedha.

Rais wa Benki ya Exim ya China Bw. Liu Liang amemueleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 20 Julai, 2016 kuwa pamoja na kutoa fedha hizo zitakazofanikisha ujenzi wa kilometa 2,190 za reli ya kati benki hiyo itashirikiana na Tanzania katika kubadilishana uzoefu na utaalamu katika ujenzi na uendeshajiwa reli.

Pamoja na kukubali kutoa fedha hizo, Rais huyo wa Benki ya Exim ya China amempongeza Rais Magufuli na serikali yake kwa dhamira ya dhati ya kuiletea nchi maendeleo ikiwemo kuharakisha ujenzi wa reli ya kati na ameahidi kuwa benki yake itatoa ushirikiano wa karibu katika kufanikisha mradi huo na miradi mingine ya maendeleo.

''Kuhusu huu mradi wa reli ya kati tuna mtazamo chanya, tunauona ni mradi mzuri na tutatoa ushirikiano wowote utakaohitajika. Tunaamini kuwa kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania mchakato wa utekelezaji wa mradi huu utafanyika kwa mafanikio na kwa kuzingatia muda "Amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wake Rais Magufuli amemshukuru Rais wa Benki ya Exim ya China Bw. Liu Liang kwa kukubali kutoa fedha hizo na amemuhakikishia kuwa Tanzania imedhamiria kutekeleza mradi huo ambao tayari ujenzi wake umepangwa kuanza katika mwaka huu wa fedha kwa kutumia fedha za ndani kiasi cha shilingi Trilioni 1 zilizotengwa katika bajeti.

Rais Magufuli amebainisha kuwa kutekelezwa kwa mradi huo kutasaidia kuinua uchumi wa Tanzania na nchi jirani zisizopakana na bahari zikiwemo Uganda, Rwanda, Burundi na Congo.

"Kwa hiyo kukubali kwao ambako ilikuwa ni kitu kikubwa, inaonesha kwamba juhudi za Tanzania kwenda haraka haraka zinakubalika kimataifa, na wenzetu hawa wachina wana pesa nyingi.

''Na kule kuaminika kwamba tunakopeshwa kwa masharti nafuu, riba yake ni ndogo na huku kwetu ni mafanikio makubwa, kwa hiyo mizigo mingi tutakuwa tunaisafirisha, tutaendeleza reli yetu na bandari zetu" Amesema Rais Magufuli.

Mradi wa ujenzi wa reli ya kati utahusisha ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) kutoka Dar es salaam-Tabora-Isaka-Mwanza, Tabora-Mpanda Kalemela,Tabora-Uvinza-Kigoma na saka-Keza-Msongati.

Mazungumzo kati ya Rais Magufuli na Rais wa benki ya Exim ya China yamehudhuriwa na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa Mnyaa, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU Dar es salaam

20 Julai,2016

magu-china-jpg.368221
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Nimeapa kusema kweli na nitasema kweli daima kwani hii ndio nguzo kuu ya kupambana na maovu yote nchini. Sitasema uongo na daima sitafumbia macho maovu yote yanayotendeka chamani bila kujali yanatendwa na nani.

Mtakumbuka ni hivi juzi tu nimeumbua mkakati wa chini kwa chini unaoratibiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Rajab Luhwavi wa kutaka kukwamisha Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM. Niliahidi kuwa nitaendelea kuwaumbua wale wote wanaoshirikiana na Luhwavi na ambao wana mikakati isiyo ya ushirika lakini dhamira yao ni kuona Magufuli hawi Mwenyekiti wa CCM iwe mwaka 2016 ama 2017. Nimerudi tena kama nilivyowaahidi na sasa ni zamu ya Benard Membe na Wiliam Lukuvi kuumbuka.

A. BENARD MEMBE
Mtakumbuka kuwa kwenye mchakato wa kumpata Mgombea Urais kwa Tiketi ya CCM, Benard Membe na Edward Lowasa ni makada wawili ambao walitengeneza kambi mbili hasimu. Makada hao wawili kila mmoja alijiona kuwa yeye ndiye mrithi pekee wa Dr Jakaya Kikwete kwenye nafasi ya Urais. Hata hivyo, kwa mapenzi ya Mungu, wote hawakuwa. Lowasa alikatwa mapema kabla hata ya kufika kwenye Tano Bora. Membe alifanikiwa kuingia Tano Bora lakini akashika mkia kwenye mchujo wa kwenda kwenye Tatu Bora ambapo Dr John Pombe Magufuli aliibuka mshindi na ndiye Rais wetu.

Hata hivyo, Lowasa aliamua kutimka chamani na kwenda kugombea CHADEMA ambako aliangukia pua kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015. Hivyo nguvu ya Lowasa ikazikwa rasmi ndani ya CCM. Benard Membe aliamua kubaki chamani kwa matarajio kuwa atapewa nafasi ya uteuzi ikiwemo nafasi ya Waziri Mkuu ambayo angeipata kama angekuwa Mbunge wa Jimbo lakini alishauriwa asigombee ubunge kwa ahadi kuwa angepatiwa nafasi nyingine. Haikuwa hivyo. Membe ana manung'uniko na yupo Bechi asijue hatma ya maisha yake kisiasa.

Kutokana na hali hiyo, Membe ameibuka kuwa na chuki na Rais Magufuli na amekuwa akiratibu na kushiriki mikakati ya chini kwa chini ili Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM akishirikiana kwa karibu na Naibu Katibu Mkuu Bara Rajab Luhwavi. Kwa nini Membe anafanya hivyo? Nitawaeleza.

1. Chuki na hasira ya kuukosa Urais. Baada ya Lowasa kubwagwa hata kabla ya kuingia kwenye Tano Bora, Membe akajiona ni Rais anayesubiri kuapishwa. Kubwagwa kwa Lowasa kulimfanya Membe ajione ni mshindi. Hata hivyo, kitendo cha mwanasiasa huyo kushindwa kuingia hata kwenye Tatu Bora kulimfanya ahisi kuwa amehujumiwa. Hasira zake alizielekeza kwa Benjamin Mkapa ambaye anasema kuwa ndiye aliyemwaga sumu ili asichaguliwe. Hivyo, Membe akawa na chuki na Mkapa na Rais Magufuli.

2. Kukosa nafasi ya Uteuzi. Membe alijiona kuwa anazo sifa za kiongozi mkubwa wa serikali ya Rais Magufuli. Hivyo kitendo cha Serikali hii kumuacha hata kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi hakika anaona kuwa ni dharau kubwa kwake.

3. Serikali ya Awamu ya Tano kushindwa kumsimamia kwenye nafasi za Uongozi wa Jumuiya ya Madola na AU. Membe anadai kuwa kwa uzoefu wake na kufahamika kwake, angefaa kugombea nafasi zilizojitokeza kwenye Jumuiya ya Madola na Umoja wa Afrika kama Serikali yake ingemtia moyo na kuahidi kumpa ushirikiano. Hata hivyo, anaona kuwa Serikali hii haina msaada kwake na anamshutumu Rais kuwa huenda anammaliza kisiasa ili ifikapo mwaka 2020 asiwe na mpinzani ndani ya chama.

4. Kuimarisha Mtandao. Membe anashirikiana na Luhwavi ili kutengeneza mtandao wa uongozi ndani ya chama. Taarifa zilizopo ni kwamba wanataka Kikwete aendelee kuwa Mwenyekiti hadi 2017 na Katibu Mkuu awe Luhwavi ili asaidie kutengeneza mtandao ambao utajenga safu ya uongozi kuanzia ngazi ya taifa hadi kwenye matawi kwenye uchaguzi wa chama utakaofanyika mwaka 2017. Ama ikiwa watashindwa kukwamisha Magufuli asiwe Mwenyekiti hapo Julai 23, watafanya hivyo mwaka 2017 ambapo chama kitafanya uchaguzi katika ngazi zote. Ajenda kuu ni kuhakikisha kuwa nguvu ya Membe inarejea ambayo itamsaidia kumuangusha Rais Magufuli kwenye mchujo wa Mgombea Urais wa CCM, uchaguzi mkuu wa 2020 ambapo amepanga kugombea.

B. WILLIAM LUKUVI
Huyu naye ana ndoto za kuwa Mwenyekiti wa CCM. Labda nikuulize Lukuvi, je Uenyekiti wa CCM Utauweza? Je wewe ni Presidential Material? Taarifa zilizopo ni kwamba Lukuvi anavizia nafasi ya Uenyekiti wa CCM. Kwa sasa anapima upepo na hasa anaangalia nini kitatokea Julai 23. Kwamba, ikiwa kundi la Wapinzani wa Magufuli litaelekea kushinda, anaamini kuwa anaweza kugombea na kushinda mwaka 2017 kwa vile anaamini kuwa yeyote atakayeshinda nje ya Magufuli Julai 23, atatengeneza ombwe la uongozi ambalo litahitajika kuzibwa mwaka 2017. Lukuvi anaona ni vigumu kwa sasa kumzuia Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti ila anaamini kuwa watafanikiwa kufanya hivyo mwaka 2017. Hivyo mkakati wa Lukuvi ni kwa ajili ya 2017 na si mwaka huu.

Swali la kujiuliza, je mikakati yote hii ni kwa faida ya nani? Kwani hakuna maisha nje ya siasa? Je wanafikiri ni rahisi kumuangusha Rais Magufuli sasa ilhali walishindwa hivyo mwaka 2015? Hakika huku ni kutapatapa. Siasa za mtandao zimeshazikwa Rasmi mwaka 2015 na wana CCM hatupo tayari kuona mitandao inarejea chamani

Wale wote ambao bado hamuamini kuwa Magufuli ndio Rais, mnapaswa kuamini hivyo sasa na ndiye Mwenyekiti wetu wa CCM.
Nishidaah sna

Sent from my GT-S7562 using JamiiForums mobile app
 
Ukiamini kwamba upo transit hapa duniani ' huwezi umiza kichwa na 2020 ,2017,2030 .....kwani wakati binadamu tunapanga yetu Mungu anapanga yake....chochote kinawezekana

Nani humu ana uhakika 2018 atakuwa hai??? Anyooshe kidole
 
Lizabon = DC
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom