LUHANJO: Sitta, Mwakyembe hawajazibwa mdomo kuzungumzia DOWANS

Luhanjo ni mtumishi chini ya rais wa nchi ambaye ni mwenyekiti wa vikao vya cabinet. Pia Luhanjo kama katibu mkuu anagopa kuwajibishwa kwa kuvuja kwa taarifa za siri za vikao vya cabinet hivyo kwa namna yoyote ni lazima atafute namna ya kujisafisha ila ukweli unabaki pale pale kuwa hawataweza kuwaziba midomo 6 na Mwakyembe labda kwa kuwatanguliza mbele za haki tu.
 
Kwa hiyo kikao hakikufanyika jana, na kama ni kweli basi kilifanyika siku ingine may be Juzi Jumatatu.

Kama kuna kikao kilifanyika Ikulu, kitakuwa si cha baraza la mawaziri, ni kikao labda cha dharula tu, chini ya mwenyekiti mwingine ambaye ameteuliwa na Rais
 
Naomba kuingia jamvini.Kwa bahati mbaya sana wengi hatukuelewa madhumuni ya habari ile ya Tanzania Daima labda kwa kutoisoma kikamilifu au kwa kutoielewa.Kwanza, habari hiyo ilikusudia kuwatisha wote ambao wangeungana na kina 6 katika mapambano dhidi ya malipo ya Dowans.Pili, imekusanya habari nyingi za matoleo ya nyuma na kuziunganisha katika kuonyesha kuwa malipo kwa Dowans ni halali na wanaoyapinga hawako sahihi.Kwa bahati mbaya habari hizo zilizounganishwa haziko balanced kwa maana kwamba yanazungumzwa ya Chikawe na Werema tu bila 6 na Mwakyembe kuhojiwa wanasemaje kuhusu shutuma dhidi yao.Siyo siri, kuhusu malipo ya Dowans Tanzania Daima linaunga mkono waziwazi kufanywa kwa malipo hayo.Kama Ikulu imewapandishia,hiyo ni safi sana ili wajutie kujikomba kwao kwa matapeli wa Dowans kusikoeleweka sababu yake.
 
Ukisikia paaaaaa ujue imekukosa aliyelenga hana shabaa. Hapa naona imewapata Ikulu ndo maana wanarudi na style yao ileile ya kukanusha kipumbavu wakijua watz ni walewale wa mwaka ule. Mbona hata Police wamekanusha mambo ya Arusha kibwegbwege hivyo hivyo?? JK atoke shimoni aongelee kuhusu Dowans ndo tutatulia.
 
Utaona wazi hii barua ni ya kujitetetea tu huku wakiwa na mshtuko wa nani kavujisha habari hizi. Inji ni mtumbwi usio na nahodha sasa, unaelea elea kutegemeana na upepo !

Yule waziri sijui Chikawe, juzi juzi si alisema hayo hayo kuwa hawa wakae kimya, au wafuate taratibu. Sioni ajabu leo kikao kikikaa na kuwaweka kitimoto hawa wapiganaji. CCM walivyo, kama ingekuwa urongo lazima hili gazeti lingeshikishwa adabu mara moja....

Si unasikia sasa wameitana Dodoma wabunge wote wa CCM, maana wengine nao washaanza kusema ovyo kuwa hii dili hadi kieleweke... Lembeli James wa shinyanga
 
Naomba kuingia jamvini.Kwa bahati mbaya sana wengi hatukuelewa madhumuni ya habari ile ya Tanzania Daima labda kwa kutoisoma kikamilifu au kwa kutoielewa.Kwanza, habari hiyo ilikusudia kuwatisha wote ambao wangeungana na kina 6 katika mapambano dhidi ya malipo ya Dowans.Pili, imekusanya habari nyingi za matoleo ya nyuma na kuziunganisha katika kuonyesha kuwa malipo kwa Dowans ni halali na wanaoyapinga hawako sahihi.Kwa bahati mbaya habari hizo zilizounganishwa haziko balanced kwa maana kwamba yanazungumzwa ya Chikawe na Werema tu bila 6 na Mwakyembe kuhojiwa wanasemaje kuhusu shutuma dhidi yao.Siyo siri, kuhusu malipo ya Dowans Tanzania Daima linaunga mkono waziwazi kufanywa kwa malipo hayo.Kama Ikulu imewapandishia,hiyo ni safi sana ili wajutie kujikomba kwao kwa matapeli wa Dowans kusikoeleweka sababu yake.

Mkuu unaweza kuwa sahihi kwenye analysis yako. Lakini sentensi ya mwisho ndipo ulipopotoka kidogo. Barua haijaonyesha mahali popote kwamba Ikulu imekerwa na/au kulipandishia gazeti la Tanzania Daima. Ni kwamba taarifa inakanusha kufanyika kwa kikao cha Baraza la Mawaziri siku tajwa.

Pamoja na hayo, siku habari hiyo ilipotoka, niliuliza swali: Hivi Manaibu Waziri nao siku hizi wanahudhuria vikao vya baraza la mawaziri? Kwa uelewa wangu Naibu Waziri haingii kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri. So, kusema kwamba Mwakyembe alihudhuria kikao hicho, tayari ilikuwa inatia walakini wa habari husika. Pili, agenda kuu ya kikao haikuwa DOWANS, so Mwakyembe aliingia kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri kama nani au kulikuwa na kipi cha muhimu ambacho kilisababisha Mwakyembe aruhusiwe kuingia kwenye hicho kikao?

It is possible, kwamba news za Tanzania Daima zilikuwa zinaongelea yaliyosemwa kwenye kikao cha Pinda ambacho aliwaita mawaziri na manaibu wao. Hicho sio kikao cha baraza la mawaziri. Bado kwenye hicho kikao cha Pinda agenda kuu haikuwa Dowans na kama kuna watu waliongelea hilo la Dowans ilikuwa ni kwa kupita tu.

Je, ni nani aliyewafunga midomo Sitta na Mwakyembe? Je, JK aliwaita moja kwa moja na kuwafunga midomo?

My guess ni kwamba kuna fisadi mmoja analitumia hilo gazeti indirectly ili kuua mjadala wa Dowans. Maana kuna baadhi ya makala na news za kuhusu Dowans, ziko pro-Dowans. Nilishangaa kuona kwamba Happiness Katabazi anamfuata Wakili Fungamtama ofisini kwake ili atoe maoni yake na maoni ya Fungamtama yakapewa headline kubwa, as if hakuna mawakili wengine. Why Fungamtama alone? Kwanini asipate views za mawakili tofauti ili ku-balance stori yake?

Kwa swala la DOWANS, Tanzania Daima haiwezi kufungiwa au kutakiwa kujieleza au hata kupewa karipio, maana liko upande wa mafisadi ambao wanazitaka hizo hela za DOWANS kwa nguvu zote. Ndiyo maana kanusho la Luhanjo halijaonyesha mahali popote likiwataka Tanzania Daima wajieleze kwanini wanapotosha umma kwa kulihusisha Baraza la Mawaziri na habari za uzushi, hilo nalo linaleta mashaka makubwa sana.

Something is fishy with Tanzania Daima katika baadhi ya mambo.
 
luhanjo mpaka ajibu ujue kunaukweli.na ametumwa aje kuchakachua kama walivyochakachua habari ya polisi walioua raia Arusha.
 
Naomba kuingia jamvini.Kwa bahati mbaya sana wengi hatukuelewa madhumuni ya habari ile ya Tanzania Daima labda kwa kutoisoma kikamilifu au kwa kutoielewa.Kwanza, habari hiyo ilikusudia kuwatisha wote ambao wangeungana na kina 6 katika mapambano dhidi ya malipo ya Dowans.Pili, imekusanya habari nyingi za matoleo ya nyuma na kuziunganisha katika kuonyesha kuwa malipo kwa Dowans ni halali na wanaoyapinga hawako sahihi.Kwa bahati mbaya habari hizo zilizounganishwa haziko balanced kwa maana kwamba yanazungumzwa ya Chikawe na Werema tu bila 6 na Mwakyembe kuhojiwa wanasemaje kuhusu shutuma dhidi yao.Siyo siri, kuhusu malipo ya Dowans Tanzania Daima linaunga mkono waziwazi kufanywa kwa malipo hayo.Kama Ikulu imewapandishia,hiyo ni safi sana ili wajutie kujikomba kwao kwa matapeli wa Dowans kusikoeleweka sababu yake.

Asante kwa kugundua hilo. Mimi ni mwandishi wa habari, ninajua nini kinatokea kwenye newsroom za Tanzania. Ukiongea na waandishi wa habari wa Tanzania Daima wanakiri kabisa kuwa Mhariri Mtendaji wao, Absalom Kibanda, amenunuliwa na Rostam Aziz na Edward Lowassa na huwa anatoa habari na makala kwa maagizo yao.

Nimesema humu JF mara nyingi, Tanzania Daima limekuwa likitumiwa na mafisadi kuunga mkono malipo kwa Dowans, kuwasafisha Rostam, Lowassa, Andrew Chenge na Nazir Karamagi na kuwatukana wapambanaji wazalendo wa nchi hii, Samuel Sitta, Dk. Harisson Mwakyembe, na wengine.

The irony of it all is that Tanzania Daima inamilikiwa na Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Chadema. Chadema inapigana vita na mafisadi na kupinga malipo kwa Dowans. Gazeti la Mbowe la Tanzania Daima linaunga mkono mafisadi na malipo kwa Dowans.

Eti Mbowe amekaa kimya anasema haingilii uhuru wa waandishi wa habari. Come on, Mbowe has to be serious kama owner and publisher kuhakikisha kuwa media yake haitumiwi na mafisadi. Mbona Reginald Mengi haruhusu wahariri wake kutoa kitu ambacho yeye hataki.
 
Habari za Kikao cha baraza la mawaziri ni confidential. Washtakiwe tuone kama watakuwa na defense juu ya habari yao.

ChiefmTz, kama Waziri Membe ameamua kufungua mashtaka kwa ajili ya kusingiziwa, inakuwaje Ofisi Kuu ya Nchi inasingiziwa na iache kufungua kesi. Kinachoaminika ni kuwa kikao kimefanyika ila Ikulu inaogopa kuchukua hatua zozote za kisheria kwa sababu hawajajua mtoa habari ametoa habari nyingi kiasi gani na kwa sababu hiyo hawataki kuumbuka kortini. Haya mambo ya kwetu ni ku-deny tu kila kitu. Wanasiasa wetu wanafikiri kuwa ukifagilia uozo chini ya kitanda watu watayasahau (kama ilivyokuwa zamani). Hawajajua kuwa mambo siku hizi ni tofauti.
 
hahahahhah
 
ukiona wanakurupuka na matamko ujue taarifa zilizopo ni za kweli.

yaani kurugenzi ya mawasiliano ikulu inawasiliana kwa e-mail account ya Yahoo??

kweli JK siyo makini.

Dah!!! Was wondering the same thing ila nimecheka sana
 
Back
Top Bottom