Luhanjo: Marufuku viongozi wa upinzani kualikwa kwenye mahafali sekondari

Mwamakula

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
1,891
382
Philemon Luhanjo amemtaka mkurungenzi wa Halmashauli Njombe na watendaji wote wa serikali kudhibiti wapinzani kualikwa kama wageni rasmi
 

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,504
Philemon Luhanjo amemtaka mkurungenzi wa Halmashauli Njombe na watendaji wote wa serikali kudhibiti wapinzani kualikwa kama wageni rasmi
Hebu fikirieni watu wenye akili kama za Luhanjo ndio wapo ikulu wanamshauri; it is real dangerous for our emerging democracy.

Sasa nimeelewa kwanini jk anaonekana kama is a joke kwa sababu ya watu kama ambao wana fikra na mawazo ya itikadi za ki imla za chama kimoja wameshapitwa na wakati.

Huwezi kuwajua mpaka wafungue midomo usikie kinachotoka midomoni mwao i feel sorry for jk kujizungushia watu kama hawa He has no body to blame but himself we gave him a power to fire outdated people, he chose not to exercise it .

Alhamsiki.
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
18,509
37,650
Mh! Nilidhani ni CCM peke yake kumbe hata serikali nayo imechoka kufikiri kiasi hicho? Lakini, je, haikupata kuandikwa mahala fulani kwamba mkiwazuia hawa mawe yatapiga kelele? Laiti angelijua kelele za mawe zinatisha kuliko kualikwa kwenye karamu na anasa za kijambazi.

Sawa, atazuia kualikwa kwenye karamu za kiserikali na za taasisi binafsi nazo atafanya hivyo hivyo? Ama kweli ulevi mbaya, mbona anawapa wapinzani hoja - tena hoja ya bure?
 

Gurtu

JF-Expert Member
May 15, 2010
1,237
317
Viongozi wa upinzani! Ni viongozi wa upinzani au viongozi toka vyama vya upinzani?kwanini viongozi wabaguliwe eti kwa sababu wanatoka vyama vya upinzani? Mtu akishakuwa kiongozi hapaswi kubaguliwa, huo utakuwa uzandiki na mgando wa kifikra.
 

FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,081
6,189
Philemon Luhanjo amemtaka mkurungenzi wa Halmashauli Njombe na watendaji wote wa serikali kudhibiti wapinzani kualikwa kama wageni rasmi
Hizo shule za sekondari ni za Luhanjo? au za baba yake Luhanjo? au za ukoo wake Luhanjo? Luhanjo anatoa wapi mamalka ya kuzuia watu kualika wanayeona anafaa? Siasa za ubaguzi ni jambo hatari kabisa na Luhanjo kama na akili timamu angerekebisha hii kauli kabla mambo hayajaharibika. Haikubaliji hata kidogo kwa kiongozi wa level ya Luhanjo kuhubiri ubaguzi kama huu?

Sasa naanza kuamini tuhuma walizokuwa wanatoa wabunge (tena wa ccm) kuhusu huyu katibu na ukabila.

Na kama katibu mkuu kiongozi anakataza wanasiasa wa upande wa upinza wasialikwe wanafunzi (hasa wa vyuo vikuu) wanaunga mkono upinzani watapata huduma gani toka kwa hili genge la wakina Luhanjo.
 

emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,743
3,031
Tutawaalika wabena wenzake aliowajaza mali asili, the man is tired and need to retire, hivi anastaafu lini? huyu jamaa uwezo wake wa kufikiri unaonekana kuwa mdogo, mara ya kwanza alisema atawachukulia hatua waliovujisha issue ya Jairo huku akicheka kwa vicheko vya kejeli leo hii anakuja na mpya kama hii. It is beyond my compehension that in our "white house" we have a mediocre man like Luhanjo.
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
27,994
30,723
Shule ni za kwake au za umma? sasa huku ni kuchanganyikiwa au kuzeeka bila busara? "ai kanti bilivu zis"
 

gepema

Member
Mar 25, 2010
97
9
Huyu mzee ameshalewa madaraka kabisa. Mvi zimemjaa lakini hana busara! Anatumia sheria gani kutoa agizo hilo?!!!
 

Mtumiabusara

JF-Expert Member
Nov 18, 2009
473
40
Kwani taratibu zinasemaje? Inabidi iwepo sheria inayozungumzia hilo. Kwa kuwa vyama vya upinzani vinapata ruzuku kutoka serikalini, wabunge wake wanalipwa na serikali, sasa kwa nini wasitembelee au kualikwa na shule?
 

Mwamakula

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
1,891
382
Tatizo lililopo ni Kwamba Thomas Nyimbo wa Chadema na Yono Kevela Mbunge wa zamani Wamekuwa wakialikwa ktk mahali na sherehe Mbali mbali za jamí na kumuweka kando Gerson Lwenge na Luhanjo.

Wapiga kura ktk jimbo la Njombe Magharibi hawamtaki Gerson Lwenge na wamekuwa wanampigia simu kumutukana. Madai yaliyopo ni kwamba Luhanjo ndiye aliyechakachua kura za maon Ccm na kumuweka Lwenge .Lwenge naye anadai ni chaguo la Ikulu.

Sasa wananch wamereact hawamtaki Lwenge. waziri Lwenge amepiga simu kwa Diwan Wa Luduga aitwaye Katanzi na Mtendaji wa kijiji cha Luduga aitwaye Chengula ,na Mkurungenzi wa Halmashauli na kuwatisha wasiwaruhusu Yono Kevela na Thomas Nyimbo kualikwa ktk mahafali ya sekondari na Msingi.
 

SEAL Team 6

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
655
118
Anayempa kiburi ni JK, siku alipokuwa anawaapisha wakuu wa Mikoa Luhanjo alikuwa pembeni ya JK, kwa hiyo anaona hakuna mtu wa kumbabaisha anawezakutamka lolote analojisikia kusema. Hii inatuthibitishia hata kauli ya Luhanjo kuhusu Jairo ilikuwa ni kiburi cha JK. Haya ngoja tuone hicho kiburi kitadumu hadi lini.
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Hizo shule wanasoma watoto wa ma CCM pekee au ni Watanzania wote ? Kwani Luhanjo anadhani kufanya hivyo anazuia nini ? Mbona hao wanajua zaidi kuliko yeye ? Na ni wapiga kura yeye hajui tu anavyo imaliza CCM.
 

Mwamakula

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
1,891
382
Waziri Lwenge hatakiwi jimboni na sasa anatumia Mamlaka ya serikali kudhibiti Upinzani.Hakuna mwenye uwezo wa kuzuia Upinzani kualikwa kwenye sherehe ya shule.Watoto wengi waliopo ktk shule za kata wengi ni kutoka upinzani kwani watoto wa ccm wanasoma ktk shule kubwa za mafisadi
 
  • Thanks
Reactions: FJM

Michese

JF-Expert Member
Feb 9, 2008
370
57
Huyu Luhanjo naona uzee unamsumbua nadhani angepumzika tu sasa,asije akaanza kutukana majukwaani bure maana akili zimekwisha kabisa
 

Baseba

Member
Aug 24, 2011
32
1
Njombe magharibi mtajuta kuichagua ccm! Mimi najua mtu wa kuleta maendeleo katika jimbo lenu alikuwa ni Nyimbo. Sasa mtajutia kura zenu kuwauzia magamba
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom