Farolito
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 11,634
- 26,373
Wakuu,
Leo tarehe 09.02.2023 Luhaga Mpina akihojiwa katika kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM amesema kwamba dharau anazoonesha Waziri wa Fedha Mwigulu Nchembe dhidi ya wabunge ni matokea ya matobo ya Katiba ambayo yanatakiwa kushughulikiwa.
"Waziri anaulizwa maswali anajibu anavyotaka kwamba nyinyi mkajadili Unganga,sijui Mimi nimesomea PhD sijapewa,haya yote ni udhaifu wa Katiba.
Pia aliendelea kuhoji kwanini mpaka sasa hakuna ratiba ya kujua Katiba inapatikanaje," Mpaka sasa ilitakiwe tuwe na jopo la wataalamu wawe wameanza kupitia Katiba Mpya kujua wapi pa kufanya marekebisho"alisema.
Pia alisisitiza kwamba Viongozi wasiteuliwe kwa kuangalia alisoma wapi na wapi au alipata A na B ndio maana tunapata Viongozi wasio na sifa kwa kuangalia vyeti pekee.
"Hili la kuteua tu mtu kwa kuangalia alisoma chuo fulani na chuo fulani au alipata A kweye cheti kisha unamteua ndio inafanya tunapata incompetent leaders,lazima tuanze kufanya usaili" Alisema.
Maoni yangu;
Hapa nawapongeza CHADEMA kwa kuipigania Katiba kwa maumivu naona somo lenu limeanza kueleweka kwa wana CCM