Luhaga Mpina apinga majibu ya Serikali kuhusu kauli kuwa hawana taarifa ya agizo la Mahakama kuhusu kurudisha mifugo ya wafugaji

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,798
21,368
Dodoma. Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amepinga majibu ya Serikali kuhusu kauli kuwa hawana taarifa ya agizo la Mahakama kuhusu kurudisha mifugo ya wafugaji kama ilivyoamuliwa na mahakama.

Mpina amesema inashangaza na kusikitisha kuona kuwa, Mahakama ilishamuru wafugaji warudishiwe mifugo yao ambayo ilikuwa imeporwa na watu wa TFS, TAWA na WMA na kwamba jambo hilo lilishazungumzwa na kutolea agizo na Waziri Mkuu.

“Hii inashangaza sana kuona leo Serikali inakataa kuwa haina taarifa hizo kuhusu mifugo, nataka kujua ni lini hasa wafugaji hawa watarudishiwa mifugo yao kama mahakama ilivyoagiza,” amehoji Mpina.

Haata hivyo katika majibu yake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema kuwa Wizara yake haina taarifa kuhusu agizo hilo kwamba wafugaji wapewe mifugo yao.

Masanja amesema kazi ya Serikali katika kesi hizo ni kupeleka vielelezo tu na hivyo wanaamini kuwa kila kitu kitatolewa ikiwa tu Wizara itapata taarifa sahihi ya nini kinatakiwa.

Amewataka wafugaji wanaodai mifugo yao kufanya mawasiliano na Wizara hiyo mapema iwezekanavyo na wakipokea taarifa hiyo watakaa pamoja kuchambua kesi hizo ili kuwalipa au kuwarudishia fidia wafugaji hao.
 
LUHAGA MPINA: NITAWEKA WAZI BUNGENI MAMBO YOTE YALIYOJIFICHA YALIYOSABABISHA KUCHELEWA BWAWA LA NYERERE, DENI LA TAIFA NA KUCHAFUKA KWA MTO MARA NA KUKATIKA KWA UMEME

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amesema kwa kuwa Bunge la Bajeti limeanza amejiandaa vizuri sana
kuwasilisha hoja mbalimbali bungeni na ataweka wazi mambo yote yaliyojificha yanayosababisha

(i) Kuchelewa kwa Mradi wa ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la
Julius Nyerere
(ii) Kukatikatika na migao ya umeme inayoendelea maeneo
mbalimbali nchini.
(iii) Tatizo la kupanda kwa bei za bidhaa (mfumko wa bei)
(iv) Kuchafuka kwa Mto Mara.
(v) Ucheleweshaji wa hukumu za mapingamizi ya kodi yenye
jumla ya ya kiasi cha Tsh. Trilioni 360.
(vi) Deni la Taifa
 
Sasa ni Luhaga Mpini na sio Mpina tena!

Simamia hapohapo maana wengine wameamua kuyatumikia matumbo yao badala ya wapiga kura wao!
Sawa , lakini ni lini Mpina atarejesha nyavu za wavuvi alizozichoma moto nchi nzima na wale samaki waliokuwa wanapimwa kwa rula?

FB_IMG_1648499814063.jpg
 
Anatafuta Kiki hiyo fever 2025!
Hatukupi kitu Luhaga mpima samaki!

Tulishakuwa na kichwa mmoja tokea kanda Ile haturudii, tunatafuta mndengereko, mmawia au msandawe, mbarbaigi! Nyie hapana
 
Shetani anapotaka kuwa malaika.

Kuna mamia ya wavuvi hawataki kusikia jina Kichaa Mpina. Huyu aliwanyang'anya nyavu zao na kuzichoma moto, na baadhi ya wavuvi walirundikwa ndani, tena wengine walikutwa wakiwa kwenye maisha tofauti na uvuvi, kwa maelezo tu kuwa waliwahi kuwavua samaki wasiotakiwa wakati fulani.

Wengine walikamatwa na kurundikwa ndani na kupewa kesi za uhujumu uchumi kwa vile tu walikutwa na nyavu (nyingine zikiwa zimechakaa) zisizoruhusiwa.

Yaani hata walionunua nyavu size ndogo, wakashtuka, wakaamua kuziweka kwenye mabamda ya uani, walikamatwa na kushtakiwa kwa kosa la uhujumu uchumi.
 
Wenzake Luhaga Mpina wanafurahi kuanza kulamba asali, yeye atakuwa hataki? Sasa ni mwendo wa kula kwa urefu wa kamba yako ukimaliza unaenda kulamba asali.
 
Anatafuta Kiki hiyo fever 2025!
Hatukupi kitu Luhaga mpima samaki!

Tulishakuwa na kichwa mmoja tokea kanda Ile haturudii, tunatafuta mndengereko, mmawia au msandawe, mbarbaigi! Nyie hapana
Yule hana njaa, amekuwa mbunge toka 2005-2025 atakuwa ametumikia 20 years(3years as Minister). Piga kazi Mpina, jamaa ni kati ya wabunge senior mle bungeni. Ni mzoefu na anazijua siasa za bungeni
 
Yule hana njaa, amekuwa mbunge toka 2005-2025 atakuwa ametumikia 20 years(3years as Minister). Piga kazi Mpina, jamaa ni kati ya wabunge senior mle bungeni. Ni mzoefu na anazijua siasa za bungeni
Wanasiasa ni mchwa au broiler, hawajawahi kushiba, wana addiction, ulevi wa madaraka, viherehere, kujulikana, fitina, pesa haijawahi kutosha ndiyo maana kila siku Bakressa na Mo na Wengineo wanabuni mbinu za kuongeza mapato!

Ana njaaa ni Mchumia tumbo kama Covid-19!
 
Back
Top Bottom