SULEIMAN ABEID
JF-Expert Member
- Feb 26, 2013
- 390
- 385
PANGA LA NEC LAMFYEKA LUHAGA MPINA- JINA LAKE LAENGULIWA KUGOMBEA UJUMBE WA NEC.
* Mambo 11 yaliyomponza yatajwa
HALMASHAURI Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi imeliengua jina la Mbunge wa Jimbo la Kisesa wilayani Meatu Mkoa wa Simiyu, Luhaga Mpina kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC) Mkoa wa Simiyu.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Chama hicho mara baada ya vikao vya Taifa vya uteuzi na kuthibitishwa pia na Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mohamed Ali Khalfan alisema jina la Mpina halimo kwenye orodha ya majina ya wagombea wa nafasi ya NEC Mkoa wa Simiyu yaliyopitishwa na vikao vya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.
Mpina alikuwa ni miongoni mwa makada wa CCM waliochukua na kurejesha fomu kuomba nafasi ya MNEC Mkoa wa Simiyu na NEC Viti 15 Tanzania Bara.
Hata hivyo katibu huyo wa CCM mkoani Simiyu hakuweza kuyataja majina ya walioteuliwa kwa kuahidi kuyataja baadae kwani wakati anazungumza na mwandishi wa habari hizi alisema yuko kwenye mkutano wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT Mkoa.
Baadhi ya makada wa CCM wamesikika wakidai huenda ikawa jina la Mpina limeenguliwa kutokana na misimamo yake anayoionyesha bungeni katika kuhoji mambo mbalimbali ya wananchi.
Makada hao wamedai miongoni mwa mambo yanayoweza kuwa yamemponza Mpina ni kuhoji bungeni kuhusu madai ya fedha za makinikia Trilioni 360 akitaka kujua nani alisamehe na kama ana mamlaka kisheria kusamehe madai halali ya watanzania ya kiasi cha shilingi Trilioni 5.5 kama ilivyoamuliwa na Mahakama za rufani za Kodi za TRAB na TRAT.
Lingine ni kuhoji bungeni juu ya Serikali kushindwa kudai madai halali ya Shilingi Trilioni 1.5 kwa ucheleweshaji wa mradi na CSR kutoka kwa Kampuni ya Arab Contractors ya Misri inayojenga mradi wa kufua umeme wa Bwawa la Julius Nyerere. Lakini pia Serikali kuendelea kutoa taarifa zinazokinzana juu ya ukamilishaji wa mradi huo.
Mpina pia kupitia Bunge alihoji kuhusu kupaa kwa Deni la Taifa kutoka wastani wa kukua kwa asilimia 4 hadi asilimia 13 na kutojulikana zilipo shilingi Trilioni 5 zilizokopwa nje ya bajeti kwa mwaka 2022.
Mbali na hilo Mpina pia alihoji bungeni kitendo cha TRA kushindwa kukusanya malimbikizo ya kodi yasiyo na kesi mahakamani kiasi cha shilingi Trilioni 7.5 na ucheleweshaji wa maamuzi ya mapingamizi ya kodi katika mahakama za rufani za kodi kiasi cha shilingi Trilioni 5 bila kuwepo sababu za msingi.
“Kuhoji bungeni uhalali wa malipo yaliyofanywa na Serikali kwa Kampuni ya Symbion LLC ya shilingi Bilioni 350 nje ya bajeti na bila kuzingatia madai halali ya Serikali ikiwemo kodi na gharama nyinginezo” alisema Jumanne Mashauri
Jambo lingine ni linalodaiwa kumponza ni kukataa bungeni juu ya uamuzi wa Serikali kujenga Bandari ya Bagamoyo bila kuwepo tathmini ya kina juu ya uwezo wa kiuchumi kugharamia mradi huo.
Suala lingine linalodaiwa kumponza Mpina ni kitendo chake cha kuhoji bungeni kuhusu Serikali kuingia mikataba mibovu, kushindwa kurejesha ngombe 6,000 za wafugaji walioshinda kesi mahakamani, kushindwa kudhibiti tembo wanaovamia mashamba na makazi ya wananchi na kusababisha vifo na majeruhi.
Jambo lingine ni kuhoji bungeni kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta kwa kisingizio cha vita ya Urusi na Ukraine hali iliyoilazimu Serikali kuweka ruzuku ya shilingi bilioni 100 kila mwezi bila kuwepo unafuu wowote kwa wananchi.
Hata hivyo makada hao walisema huenda pia msimamo wake wa kuhoji bungeni suala la katakata ya umeme na migao ya umeme isiyoisha nchini iliyopelekea kuathiri uchumi na utoaji wa huduma zinazotegemea nishati ya umeme huenda pia likawa limemgharimu kuenguliwa.
Maeneo mengine ambayo Mpina amekuwa akihoji bungeni ni kuhusu suala la usimamizi mbovu na kupanda kiholela kwa bei ya mbolea na namna ilivyowaathiri uzalishaji na upatikanaji wa chakula nchini
Pia amekuwa akihoji bungeni juu ya kupanda kiholela kwa bei za bidhaa na gharama za maisha hali iliyopelekea mfumko mkubwa wa bei nchini huku Serikali ikishindwa kudhibiti hali hiyo.
Mpina alipoulizwa kuhusiana na madai ya kuengeliwa kwenye kinyang’anyiro cha NEC Mkoa wa Simiyu simu yake iliita bila kupokelewa na baadaye alituma ujumbe mfupi wa maandishi kuwa yuko kwenye kikao cha Kamati ya Fedha, Utawala na Uongozi cha Halmashauri ya Meatu.`