VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Episode 1: Kamati ya Bunge yagundua utata wa mkataba kati ya kampuni ya Lugumi na Jeshi la Polisi. Mkataba unasemwa ni wa bilioni 37 na tayari bilioni 34 zimeshalipwa.
Episode 2: Wahusika wa Mkataba tata: Wizara ya Mambo ya Ndani,Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi kila mmoja akaeleza chake.
Episode 3: Wanasiasa na wananchi wakaanza mjadala wa mkataba huo ambao ukaibua watu na makampuni mengineyo yahusikayo na mkataba tata huo. Kati yao wapo Mhe. Charles Kitwanga anayetajwa kama kampuni ya Infosys,IGP mstaafu Said Mwema,na kampuni ya Biometrica ya Marekani.
Episode 4: Wasemaji wa Serikali na wa jeshi la polisi kuhusu mkataba wa Lugumi waliendelea kusisitiza kuwa mkataba ulikuwa halali na ulitekelezwa.
Episode 5: Bunge likaunda Kamati Ndogo kuchunguza utekelezwaji wa mkataba tata wa Lugumi.
Episode 6: Kambi ya Upinzani kupitia Msemaji wao wa Wizara ya Mambo ya Ndani ilitaka kuzungumzia suala la Lugumi Bungeni lakini kipande hicho cha hotuba kikafutwa na kukatazwa.
Episode 7: Pamoja na kuondolewa kwenye hotuba ya Kambi ya Upinzani,suala la Lugumi liliendelea kujadiliwa na Wabunge wakati wa kujadili Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Vijembe vikatawa
la.
Episode 8: Inaripotiwa na magazeti kuwa mashine za utambuzi wa alama za vidole kwenye vituo vya polisi,zilizopaswa kufungwa miaka kadhaa iliyopita katika kutekeleza Mkataba wa Lugumi,zinafungwa sasa. Wachambuzi wanaona hiyo ni hadaa,utapeli na sinema kwa Kamati Ndogo ya Bunge iliyopewa jukumu la kuchunguza utekelezwaji wa Mkataba wa Lugumi.
Episode 9: Mmoja wa wahusishwa wa mkataba tata wa Lugumi,aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Charles Kitwanga anaingia Bungeni na kujibu swali la Wizara akiwa amelewa.
Episode 10: Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani,Charles Kitwanga,anatenguliwa/anatumbuliwa kwa kujibu swali akiwa amelewa Bungeni. Hakutenguliwa kwa ajili ya Lugumi. Sasa aweza kukamatwa na kuhojiwa kwa sakata la Lugumi?
Nini kitafuata?
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam