snipa
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 4,290
- 1,780
This is made in green city, the beginning and the end.
Mbeya, where talent was born! Tanzania knows! Made in Green City talks about variety of things like poverty, war against ignorance and neocolonialism...against the system being precise! and yes, the great MCs in Tanzania were almost all influenced by Mbeya streets! Shots taken by Andy Zabron (Bantu Imagez) of SAE, Mbeya.
=====
MAKANTA BIOGRAPHY
Kundi la MaKaNTa, Maikini Katika Nchi Tajiri, liliundwa rasmi mwaka 2011 na kuanza shughuli zake tangu mwaka huo hadi hivi sasa. Kundi hili lina sifa kubwa ya kuongozwa na Mkufunzi wa Chuo kikuu, Mbeya University of Science and Technology, MUST, Frank Mwakyembe a.k.a Lugombo
Kimsingi kundi hili liliasisiwa na Lugombo na Mkolosae (Michael Mwakolo), Mkolosae kwa sasa amefariki, (Rest In Power) ambao walikutana 2010 na baada ya kuona mawazo yanafanana wazo la kuiokoa mitaa kwa muziki wa HipHop likaibuka tangu hapo. Kipindi hicho Mkolosae alikuwa anasoma TEKU, Lugombo akiwa ni mkufunzi wa MUST
Wazo lilipata mashiko mwaka 2011, baada Lugombo kukutana na “Siga Nyota” (Alex Msigala) katika maeneo yao ya kujidai ambayo alikutana na Mkolosae. Siga Nyota akawatambulisha kwa “Buggie” (Daniel Mwakolo). Kwa kipindi Mkolosae alipokuwa chuoni walifahamiana vyema na Adamoe (Adam Kaseko) ambaye alikuwa muhasibu wa TEKU. Adamoe alikuwa na urafiki wa karibu na Geez Mabovu(Rest in Power) wa Dirty South Family
Mkusanyiko wa watu hao, na kwa kuwa wote walikuwa na mawazo yaliyoendana kiitikadi wakaanza kufanya uandishi wa mashairi na kurekodi ngoma zao ambazo zilifanya wawe na kundi la kuitwa MaKaNTa
Kwa kifupi Kundi la MaKaNTa lilijumuisha wasanii kama Mkolosae (R.I.P), Siga Nyota, Adamoe, Lugombo, Jadah, Samicho Stimela, Tovuti Tata, Momumo and Ezedon.
MAKANTA walitoa album ya kwanza mwaka 2015 iliyoitwa MASKINI KATIKA NCHI TAJIRI (MaKaNTa). Baada ya album hiyo wakaendelea kutoa mixtapes na album binafsi za waliomo kwenye kundi hilo ikiwemo ya UHURU HAUPO HURU (Mixtape by Adamoe, 2014), MADE IN GREENCITY (Mixtape by Lugombo, 2016), MOMUMO (Album by Momumo and Patrino, 2018), UPENDO UTUONGOZE (Lugombo, 2018) and NJE YA MTAALA (Adamoe, 2018)
Mkolosae alifariki Agosti 2018 baada ya kifo chake album yake ilitolewa na kundi kwa heshima yake wakaiita The Life of Mkolosae, Mkolosae ameacha mtoto mmoja wa kiume.
Asili Mia Akili Mia, Tunavaa Machata Tu (TMT) ni kati ya projects ambazo makanta wanaendelea nazo hadi hivi sasa. Kwa sasa wana kauli mbiu “Hatutaki Umaskini Katika Nchi Tajiri” (Say No To Poverty in a Rich Country) ikiwa imebeba dhima nzima ya familia ya MAKANTA
NB: Jamaa wengi walioko MaKaNTa ni wenye usomi wao lakini pia ni watu wanaopenda kuendelea kujifunza na ndio sababu katika mixtape ya Made in green City kumekuwa na Kibao cha kuitwa Mwanangu soma Vitabu, ikiwa inasisitiza kujifunza