Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,552
W aziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola amesema hajawahi kupokea barua yoyote kutoka chama cha siasa kulalamika kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara au maandamano.
Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Septemba 26, 2019 baada ya kuzindua ofisi ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) mjini Dodoma.
Amesema sheria inawataka watu wanaotaka kukusanyika kulipa taarifa Jeshi la Polisi, wakiona kimya wanaendelea ila wakipewa barua ya zuio wanatakiwa kusitisha shughuli hizo na kukata rufaa kwa waziri mwenye dhamana ya wizara hiyo.
"Tangu nimeteuliwa sijawahi kupokea hata rufaa kulalamika kuwa wamenyimwa haki badala yake wanakurupuka na kulalamika sasa mimi nifanyeje," amesema Lugola.
Amesema wanaolalamika na kuanza kufanya wanachokitaka wao lazima wakutane na mkono wa sheria kwani polisi iko imara na hawawezi kuachwa.
"Tunao polisi imara, hakuna polisi anayeweza kuwakimbia watu hata kidogo lazima wasonge mbele, sasa hapo ndio mtasikia huyu kaumia au kaumizwa yote ni kwa sababu hawafuati sheria," amesema Lugola.
Amesema sheria zikifuatwa hakuna shida itakayotokea lakini kinyume na hapo mambo yanakuwa tofauti.