Lugola awatangazia vita wanaomkejeli Rais Magufuli mitandaoni

Waziri wa Mambo ya Ndani aliagiza Jeshi la Polisi nchini Tanzania kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kuwasaka watu wanaotoa maneno ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli na Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Februari 13, 2019 jijini Arusha Lugola amesema wanaotoa maneno ya uchochezi kupitia simu zao, Blogs na makundi ya WhatsApp watasakwa popote na kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Watanzania tumieni vizuri mitandao ya kijamii, msitumie kuvuruga amani ya nchi, usijidanganye unaweza kufanya uchochezi na usikamatwe,” amesema akidai watu hao wanamchonganisha Rais Magufuli na wananchi.

“Kama unatoa kauli za kumtukana Rais na uchochezi ina maana kuna watu nyuma wanakutuma,” amesema Lugola.

Chanzo: Mwananchi
Wanaochafua upinzani kama akina musiba wao wanafanyajwe? Hii ni nchi ya wote na si ccm pekee
 
Hivi ile marufuku iliyotolewa ya kuwazuia watanzania kuimba wimbo wao wa Taifa ilishatekelezwa au bado? Nakumbuka ni huyu Jamaa ndio alitupiga marufuku kuwa hatutakiwi kuimba wimbo wetu wa taifa.
 
Waanze kudeal na wale watu wa"ile pesa tuma kwenye namba hii" wakimaliza wale watafute kazi nyingine ya kufanya ....mungu aliyetuumba akatupatia pumzi na hela za kununua bundle tu watu wanamdhihaki wengine wanamtusi sembuse magu hajawahi kuumba hata sisimizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri wa Mambo ya Ndani aliagiza Jeshi la Polisi nchini Tanzania kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kuwasaka watu wanaotoa maneno ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli na Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Februari 13, 2019 jijini Arusha Lugola amesema wanaotoa maneno ya uchochezi kupitia simu zao, Blogs na makundi ya WhatsApp watasakwa popote na kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Watanzania tumieni vizuri mitandao ya kijamii, msitumie kuvuruga amani ya nchi, usijidanganye unaweza kufanya uchochezi na usikamatwe,” amesema akidai watu hao wanamchonganisha Rais Magufuli na wananchi.

“Kama unatoa kauli za kumtukana Rais na uchochezi ina maana kuna watu nyuma wanakutuma,” amesema Lugola.

Chanzo: Mwananchi
Huyo mzee anazeeka vibaya kujipendekeza kwa kiwango hicho ni aibu
 
Kipindi hiki hamna mawazo huru. Kila jambo ukifanya umetumwa. Na hasa mawazo mbdala yasiyo wafurahisha watawala. Utaitwa kila aina ya jina baya. Jambo pekee tunalopaswa kufanya ni kuwa upande mmoja ndo ujulikane ww ni mzalendo hata kama unaona jambo hilo haliko sawa.

Ni enzi tunapitia pamoja na kwamba kuna maumivu ndani yake lakini tukubali kuwa taifa linapitia stage mhimu katika ukomavu wake. Taifa letu ni Tanzania na Uongozi unapita ila nchi yetu itabaki kuwA Tanzania. Hata kama tunaumia ila tuamini tuvumilie.
 
Naunga mkono Marufuku ya kutuka Viongozi tena Mimi niombe marufuku hiyo iwe pia kwa wote wanaokejeli Juhudi za Serikali. Wakamatwe mara moja na kufikishwa mbele za sheria na kuadhiniwa mara moja wakithibitika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono Marufuku ya kutuka Viongozi tena Mimi niombe marufuku hiyo iwe pia kwa wote wanaokejeli Juhudi za Serikali. Wakamatwe mara moja na kufikishwa mbele za sheria na kuadhiniwa mara moja wakithibitika

Sent using Jamii Forums mobile app

Muulize huyo Lugola alimpata mbwa? Je alimalizana vipi na Lugumi? Hapa hatukanwi mtu bali wanapewa ukweli tu. Nyie mnaomsujudia mwenge ndio mtasifia kila kitu. Huko mitaani ndio kuna vilaza sio huku mitandaoni.
 
Tutukanane raia tu. Huu ulimwengu bwana eti kukukosoa ndo kutukana makubwa . Mungu kila siku asemwa bibaya na wala haachi kutoa riziki

Back
Top Bottom