Lugola aionya Jamhuri kumsotesha kortini

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
KANGI Logala, Mbunge wa Mwibara ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa onyo kwa Jamhuri kwa kukwamisha kuwasomea maelezo ya awali katika kesi inayowakabili.

Lugola, Victor Mwambalaswa, Mbunge wa Lupa na Murad Sadiq, Mbunge wa Mvomero wanatuhumiwa kuomba rushwa ya Sh. 30 mil kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Gairo tarehe 15 Machi mwaka huu.

Lugola ametoa madai hayo leo mbele ya Thomas Simba, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo baada ya wakili wa serikali Denis Lekayo kueleza kuwa, waendesha mashtaka wa kesi hiyo hawapo.

Wakili Lekayo amedai kuwa, shauri hilo liliitishwa kwa ajili maelezo ya awali lakini waendesha mashtaka hawakupo.

Kutoka na maelezo hayo Lugola amedai kuwa, ikemee tabia hiyo ya kuahirishwa kesi mara kwa mara.

Lugola amedai kuwa, kitendo hicho kinawanyima haki yao ya msingi ya kufanya shughuli zao za Bunge.

Imekuwa kawaida kwa washtakiwa wanapokuwa watoro mahakama huwaita kuthibitisha kwanini wakeshindwa kuhudhuria.

Baada ya kueleza hayo, Lekayo ameiomba mahakama radhi na kusema ‘tutafanya haraka kesi iendelee.’

Hakimu Simba amesema, kauli iliyotolea na mshitakiwa ni ya msingi. Baada ya kueleza hayo ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 12 Julai mwaka huu kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.
 
Wakwapuaji wa Ccm. Labda kesi yao inatakiwa ihamishiwe mahakama ya mafisadi
 
KANGI Logala, Mbunge wa Mwibara ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa onyo kwa Jamhuri kwa kukwamisha kuwasomea maelezo ya awali katika kesi inayowakabili.

Lugola, Victor Mwambalaswa, Mbunge wa Lupa na Murad Sadiq, Mbunge wa Mvomero wanatuhumiwa kuomba rushwa ya Sh. 30 mil kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Gairo tarehe 15 Machi mwaka huu.

Lugola ametoa madai hayo leo mbele ya Thomas Simba, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo baada ya wakili wa seriksli Denis Lekayo kueleza kuwa, waendesha mashtaka wa kesi hiyo hawapo.

Wakili Lekayo amedai kuwa, shauri hilo liliitishwa kwa ajili maelezo ya awali lakini waendesha mashtaka hawakupo.

Kutoka na maelezo hayo Lugola amedai kuwa, ikemee tabia hiyo ya kuahirishwa kesi mara kwa mara.

Lugola amedai kuwa, kitendo hicho kinawanyima haki yao ya msingi ya kufanya shughuli zao za Bunge.

Imekuwa kawaida kwa washtakiwa wanapokuwa watoro mahakama huwaita kuthibitisha kwa nini wakeshindwa kuhudhuria.

Baada ya kueleza hayo, Lekayo ameiomba mahakama radhi na kusema ‘tutafanya haraka kesi iendelee.’

Hakimu Simba amesema, kauli iliyotolea na mshitakiwa ni ya msingi. Baada ya kueleza hayo ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 12 Julai mwaka huu kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.

Mkui waswahili walsema mkuki kwa nguruwe kwa binadsmu mchungu. Wapinzsni wakisoteshws wanaonavni haki yao. Kuna siku zitskuja kutskuwa na vilio na kudaga meno. Hivyo vyeo walianzia magavana wa kikoloni, na leo hawapo.
 
Kumbe tunateua viongozi kwa vigezo vya ukibaka??

Hakika hili ni Taifa la "United Republic of Gangsters"
 
Nakumbuka kisa cha Mke wa Kaisari alichokitoa Mwl Nyerere. (RIP). Mke wa Kaisari alituhumiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu mwingine. Baadae Kasari akaitisha uchunguzi, lakini ikaja kubainika kuwa zile tuhuma hazikuwa za kweli. Pamoja na kuwa tuhuma hazikuwa za kweli, Kaisari aliamua kuachana na yule Mwanamke kwani tuhuma tu zilitosha kumkosesha sifa ya kuwa Mke wa Kaisari. Lakini Kaisari huyu!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom