Lugola aionya Jamhuri kumsotesha kortini

  • Thread starter Mwanahabari Huru
  • Start date

Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Messages
13,488
Likes
27,320
Points
280
Age
48
Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2015
13,488 27,320 280
KANGI Logala, Mbunge wa Mwibara ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa onyo kwa Jamhuri kwa kukwamisha kuwasomea maelezo ya awali katika kesi inayowakabili.

Lugola, Victor Mwambalaswa, Mbunge wa Lupa na Murad Sadiq, Mbunge wa Mvomero wanatuhumiwa kuomba rushwa ya Sh. 30 mil kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Gairo tarehe 15 Machi mwaka huu.

Lugola ametoa madai hayo leo mbele ya Thomas Simba, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo baada ya wakili wa seriksli Denis Lekayo kueleza kuwa, waendesha mashtaka wa kesi hiyo hawapo.

Wakili Lekayo amedai kuwa, shauri hilo liliitishwa kwa ajili maelezo ya awali lakini waendesha mashtaka hawakupo.

Kutoka na maelezo hayo Lugola amedai kuwa, ikemee tabia hiyo ya kuahirishwa kesi mara kwa mara.

Lugola amedai kuwa, kitendo hicho kinawanyima haki yao ya msingi ya kufanya shughuli zao za Bunge.

Imekuwa kawaida kwa washtakiwa wanapokuwa watoro mahakama huwaita kuthibitisha kwa nini wakeshindwa kuhudhuria.

Baada ya kueleza hayo, Lekayo ameiomba mahakama radhi na kusema ‘tutafanya haraka kesi iendelee.’

Hakimu Simba amesema, kauli iliyotolea na mshitakiwa ni ya msingi. Baada ya kueleza hayo ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 12 Julai mwaka huu kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.
 
kisepi

kisepi

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2015
Messages
1,784
Likes
468
Points
180
kisepi

kisepi

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2015
1,784 468 180
mbele kwa mbele
 
LESIRIAMU

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2008
Messages
4,527
Likes
3,008
Points
280
LESIRIAMU

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2008
4,527 3,008 280
Wakwapuaji wa Ccm. Labda kesi yao inatakiwa ihamishiwe mahakama ya mafisadi
 
Mawembasa1979

Mawembasa1979

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2015
Messages
616
Likes
366
Points
80
Mawembasa1979

Mawembasa1979

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2015
616 366 80
Wakwapuaji wa Ccm. Labda kesi yao inatakiwa ihamishiwe mahakama ya mafisadi
Mahakama ya mafisadi ni kwa waliokwapua tshs 1 billion +
 

Forum statistics

Threads 1,235,349
Members 474,523
Posts 29,219,571