Lugha zitumiwazo kwenye Filamu za Bongo

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Ukiangalia Filamu nyingi za Bongo matumizi sahihi na anuai ya Lugha ya Kiswahili hayapo. Tatizo hili linaweza kutokana na Filamu hizi kutokutumia andiko la Filamu "Script" na badala yake wanatumia muongozo wa Filamu ambao umejaa ni nini kitatokea kwenye Filamu.

Ninachokizungumza ni kule kutokujua kwamba Lugha husawiri au huleta tafisiri ya maisha halisi ya jamii husika. Inawezekanaje kwa mhusika wa kike kwenye Filamu amwambie mwanawe wa kike kwamba "usimwamini mwanaume hata akiwa baba yako mzazi" hivi kweli hii inasawiri maisha halisi ya watanzania?

Matamshi yao na unyoofu wa Lugha unakatiksha tamaa sana.
 
kuna moja nilikuwa natazama, eti huyu binti yuko fiti sana abstairs akimaanisha binti ana akili sana.
 
Yanachosha hayo mamovie ili upunzishe ubongo wako inabidi UYAPOTEZEE TUU.
 
Back
Top Bottom