Lugha za kichina: Kuna haja ya kuingiza kwenye mitaala mashuleni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lugha za kichina: Kuna haja ya kuingiza kwenye mitaala mashuleni?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mtanzania1, Jul 20, 2011.

 1. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  WanaJF uchumi na teknoloia ya china unakuwa kwa kasi kubwa. Wamefikia hali hiyo kwa kutumia lugha zao hasa katika upande wa teknologia. Hivi hakuna haja ya kuingiza lugha zao katika mitaala ya shule zetu kama vile yalivyo masomo mengine ya lugha kama kifaransa ili angalau tuweze kupata habari hasa za kiteknolojia kutoka kwao?
   
 2. N

  Nakei Member

  #2
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wachina ni tofauti na wazungu, wachina wanauza bidhaa kama simu na kutafuta mali ghafi kwenye nchi zingine ni wao wa kujifunza hizo lugha husika. Wazungu wamejikita kwenye mambo ya utafiti na masuala ya demokrasia na utawala bora, kwa kupitia wazungu, wasomi wetu wanapata ajira kwenye miradi ya utafiti na serikali pia wanachota hela kwa wazungu kupitia masuala ya utawala bora na demokrasia. Ukichunguza kwa makini utagundua 95% ya wasomi wetu hujipatia mkate wao kupitia wazungu kwenye miradi mbalimbali iwe NGO au utafiti. Pia kumbuka wanachangia bajeti za serikali zetu za kiafrika na hata vyama vya siasa. Mchina kajikita zaidi kwenye biashara.
   
 3. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Hawa sasa ni ndugu zetu inabidi tuanze mapema kujifunza maana kariakoo wamejaa sana, mtaani kwetu wameanza kuuza bar. Sasa maelewano kidogo ya shda.
   
Loading...