thesym
JF-Expert Member
- Aug 15, 2012
- 3,827
- 4,757
Ukitoa lugha za afrosemitic languages kama vile Amharic - Wikipedia, the free encyclopedia na Egyptian language - Wikipedia, the free encyclopedia ambazo kiujumla hizi zipo kwenye kundi moja na lugha kama hebrew, arabic, phonician, aramaic,asyriac nk. lugha karibia zote za kiafrika hazikuwahi kuwa na alphabet zake zenyewe asilia, ukiangalia watu weusi huku africa huwezi kuta records za kale ambazo zimeandikwa kwa herufi ambazo ni tofauti hizi roman alphabet ama arabic alphabet tofauti tu na michoro ya mapangoni, historia yetu inakuja kuanza moja moja kuja kwa wageni kiasi cha kwamba kama vile afrika haikuwepo, ni ngumu kukuta records zilizoandikwa labda miaka 1500BC kwa sehemu kubwa africa tofauti na zile nchi ambazo ni afro semitic kama ethiopia. mi natoa challenge kama kuna mtu anaweza weka records za tanzania hata 100BC aweke. hii inamanisha ni kwamba afrika ustaarabu umechelewa kufika lakini cha kushangaza kuna watu wanasema watu weusi(waafrika) walishawahi tawala dunia nzima na hata ulaya kwamba mababu zetu ndo walifundisha sasa cha kushangaza hata kabla ya european renaissance karne ya 15 sikuwahi kubahatika kumsoma ama great thinker yeyote ambaye ni mweusi au mwafrika, lakini utakuta wachina, wagiriki, waarabu, wakorea, wahindi,wayahudi wapo na rekodi zao zipo na wanajulikana hizo lugha zote na nyingi ya nchi za asia lugha zao zina alphabet zake asilia na rekod zao zimeandikwa na wao wenyewe na si mtu baki kwa kutumia herufi za lugha zao wenyewe. kwa mfano tunasoma mwaka 2500BC wanajimu wa kichina walirekodi tukio la kupatwa kwa mwenzi hili ndilo tukio la mwanzo la kupatwa kwa mwezi kurekodiwa ila ni ngumu sana kukuta vitu kama hivi barani afrika, Sasa mi swali langu kwa nini lugha za kiafrika hazikuwahi kuwa na alphabet ambazo zimetokea naturally mpaka tukaletewa hizi za kigeni ambazo ndo tunatumia sasa, ina maana waafrika ustaarabu umechelewa kuja? ingekuweje sasa kama hawa wageni wasingekuja tungeendelea kuwa na ujinga?