Lugha ya Kiswahili, Historia yake na Wasemaji

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
LUGHA YA KISWAHILI
Kiswahili ni lugha ya Kibantu yenye misamiati mingi ya Kiarabu (30%), lakini sasa ya Kiingereza pia (10%), inayozungumzwa katika eneo kubwa la Afrika ya Mashariki.

Lugha hii ina utajiri mkubwa wa misamiati, misemo, methali, mashairi, mafumbo, vitendawili na nyimbo. Kiswahili hutumika kufundishia shuleni na kuna vitabu vingi vilivyotungwa kwa kutumia lugha hiyo, vikiwa pamoja na vile vya hadithi, hekaya au riwaya.

Historia ya lugha
Kiswahili kilianza kuandikwa kwa herufi za Kiarabu pekee kwa karne nyingi: "Huu ni ukumbusho wa askari wenyeji Waafrika waliopigania katika Vita Kuu..." (Matini kwenye Sanamu ya Askari, Dar es Salaam).

Lugha ilianza takriban miaka 800-1000 iliyopita katika mazingira ya vituo vya biashara vya pwani ambako wafanyabiashara kutoka Uarabuni, Uajemi na Uhindi walikutana na wenyeji Waafrika. Lugha kuu ya kimataifa ya biashara hiyo ilikuwa Kiarabu.

Inaonekana ya kwamba lugha mpya ilijitokeza wakati wenyeji wa pwani, waliokuwa wasemaji wa lugha za Kibantu, walipopokea maneno mengi hasa ya Kiarabu katika mawasiliano yao. Kwa hiyo msingi wa Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu pamoja na maneno mengi ya Kiarabu. Imekadiriwa ya kwamba karibu theluthi moja ya maneno ya Kiswahili yana asili ya Kiarabu.

Kando ya Kiarabu toka zamani pia kuna athira ya lugha mbalimbali kama Kiajemi, Kihindi na Kireno.

Kuanzia karne ya 20 hadi sasa maneno mengi yamepokewa kutoka Kiingereza, na katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Kifaransa, lakini pia kutoka lugha nyingine, Kiarabu kikiwa mojawapo.

Kwa karne nyingi iliandikwa kwa herufi za Kiarabu (سواحلي sawahili au لغة سواحيلية lugha sawahiliya).

Sarufi ya kwanza pamoja na kamusi iliandikwa mwaka 1848 na Dokta Ludwig Krapf huko Rabai Mpya / Mombasa.

Kiswahili kilikuwa na lahaja nyingi kutokana na lugha mbalimbali za Kibantu zilizochangia katika eneo husika.

Tangu karne ya 19 lugha ilianza kuenea barani kwa njia ya biashara.

Wakati wa ukoloni wa Uingereza lugha ilisanifishwa na Kamati ya kimaeneo ya lugha ya Kiswahili kwenye msingi wa lahaja ya Unguja.

Wasemaji
Hakuna hakika kuhusu idadi ya wasemaji wa lugha hiyo; idadi zinazotajwa zinatofautiana. Tunadhani ni wasemaji 150 milioni

Wasemaji wanaoitumia kama lugha ya kwanza hawapungui milioni 15-25 na wasemaji wanaoitumia kama lugha ya pili ni zaidi ya milioni 125.

Idadi ya wasemaji wa lugha ya kwanza inakua haraka, kwa sababu lugha inaenea katika maeneo ambapo lugha nyingine zilikuwa lugha kuu, na hasa katika miji ya Tanzania imekuwa lugha kuu, badala ya lugha za kikabila, kutokana na mchanganyiko wa watu hata ndani ya nyumba moja, kama vile wanapooana watu wa makabila tofauti, jambo ambalo limekuwa la kawaida hasa Tanzania, ambayo inaongoza kwa matumizi ya Kiswahili. Kwa watoto wengi kimekuwa lugha mama.

Kati ya nchi nyingine ambapo Kiswahili kinatumika kuna Kenya, Uganda, Kongo-Kinshasa, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Somalia na visiwa vya Bahari Hindi kama Visiwa vya Ngazija (Komoro), Oman, Yemen.

Lugha rasmi
Kiswahili kimekuwa lugha rasmi katika nchi zifuatazo:

Tanzania: ni lugha ya taifa; ni lugha ya shule za msingi, lugha ya utawala serikalini na mahakamani; inatumika kote nchini, makanisani, misikitini, redioni, kwenye runinga na idadi kubwa ya magazeti. Serikali inatakiwa kukiendeleza Kiswahili kwa sababu ni lugha ya taifa. Sera ya elimu ya mwaka 2015 imechagua Kiswahili katika miaka 10 ijayo kiwe lugha ya kufundishia katika ngazi zote, ikiwemo ile ya chuo kikuu.

Kenya: ni lugha ya taifa tena lugha rasmi, sawa na Kiingereza, baada ya rasimu ya katiba mpya kupitishwa tarehe 4 Agosti 2010; Kiswahili ni lugha ya kwanza ya mawasiliano kati ya wananchi wakikutana nje ya eneo lenye kabila moja tu; ni lugha inayofundishwa lakini si lugha ya kufundisha mashuleni; ni lugha inayotumika na polisi na jeshi, ni lugha ya kuhutubia wananchi mjini na kitaifa; sehemu za ibada makanisani zinatumia Kiswahili; kuna gazeti moja tu la Kiswahili; sehemu za programu redioni na kwenye runinga ni kwa Kiswahili. Hata hivyo, lugha inachanganywa mara nyingi na Kiingereza na lugha za maeneo au za kikabila.

Uganda: kimetangazwa kuwa lugha ya taifa tangu 2005; iliwahi kuwa lugha ya taifa wakati wa utawala wa Idi Amin; wakati wa ukoloni ilifundishwa mashuleni ikaelekea kuwa lugha rasmi pamoja na Kiingereza lakini matumizi haya yalipingwa hasa na Waganda hivyo Waingereza waliacha mipango hiyo. Ni lugha ya polisi na jeshi, hali ambayo imeleta ugumu kwa lugha kukubalika na wananchi wengi kutokana na historia ya utawala wa kijeshi Uganda; watu wengi bado hukumbuka hasa matusi ya wanajeshi waliowatesa wakisema Kiswahili. Lakini kuna maeneo ya Uganda ambako Kiswahili kinatumiwa na watu wengi kama lugha ya sokoni na barabarani. Wona UBC, WBS tv. Mwaka 2005 bunge lilipiga kura kukifanya lugha rasmi ya pili kwa kuwa kinazungumzwa zaidi (nje ya Buganda).

Rwanda: tarehe 8 Februari 2017 bunge lilifanya Kiswahili lugha rasmi ya nne baada ya Kinyarwanda, Kifaransa na Kiingereza.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo: Kiswahili ni kati ya lugha nne za kitaifa (pamoja na Kilingala, Kiluba na Kikongo), pia lugha ya jeshi. Kiswahili kilifika mashariki ya nchi na misafara ya biashara ya watumwa na pembe za ndovu kutoka Zanzibar na pwani ya Tanganyika. Imeenea zaidi kati ya mchanganyiko wa wafanyakazi kwenye migodi ya Shaba.

Lugha ya kwanza, lugha ya pili
Kiasili Kiswahili kilikuwa lugha ya kwanza tu ya wakazi wa miji ya Waswahili kwenye pwani, katika sehemu za pwani pia kijijini. Baada ya kuenea kimekuwa lugha ya watu wengi mjini hasa Tanzania lakini pia Kenya.

Kimeenea zaidi kama lugha ya mawasiliano na biashara pale ambako watu wa makabila mbalimbali wanakutana. Pamoja na nchi zinazotajwa hapo juu Kiswahili kinatumika katika Kaskazini ya Msumbiji, Kusini kabisa ya Somalia, Mashariki ya Burundi.

Maeneo ya mpaka wa Tanzania kuna pia wasemaji kadhaa huko Malawi na Zambia.

Tanzania na Kenya zilipokea wakimbizi wengi waliojifunza Kiswahili lakini hakuna uhakika kama bado kinatumika wakirudi Rwanda, Sudan au Somalia.

Kimataifa
Radio France Internationale kwa Kiswahili.
Lugha hii leo imekuwa na umuhimu mkubwa duniani kwa jumla, na hasa Afrika, kwa sababu ya kuenea kwake nchi mbali mbali, na kukusanya kwake watu wa makabila na nchi kadha wa kadha wakaweza kufahamiana kwa lugha moja, hasa ilivyokuwa ni lugha mojawapo katika lugha kubwa za Africa ambazo zinachukuwa mahala pa lugha za kigeni na Wakoloni, kama Kiarabu, Kiurdu, Kiebrania, Kireno na kadhalika.

Leo imekuwa inatumiwa katika kusambaza habari katika vituo mbali mbali ulimwenguni kama vile Sauti ya Amerika, BBC, Deutsche Welle, Monte Carlo, RFI, na nchi nyinginezo kama vile Uchina, Urusi, Irani.

Aidha, imekuwa ni mojawapo ya lugha muhimu zinazofundishwa katika vyuo vikuu nchini Marekani, Uingereza, Ulaya bara, Urusi, Uchina, na barani Afrika.

Maendeleo ya Kiswahili
Lugha ina maendeleo: inaweza kukua, kukwama au kufa. Athira nyingi hutokea bila mpangilio pale ambako wasemaji wanapokea maneno mapya, wanaacha kutumia maneno mengine au hubadilisha kawaida ya matamshi au sarufi. Haya yote hutokea pia katika uwanja wa Kiswahili.

Kuna mzaha unaosimuliwa hasa Tanzania: Kiswahili kilizaliwa Unguja, kilikua Tanzania Bara, kikafa Kenya na kuzikwa Uganda. Hali halisi Kiswahili kina maendeleo yake katika nchi hizo zote labda zaidi Kongo.

Lakini itategemea pia juhudi za serikali kama umoja wa lugha utatunzwa kwa sababu kuna athari nyingi kutoka lugha za kila eneo zinazoingia katika ukuzi wa Kiswahili kwa namna zinazotofauitiana.

Taasisi zinazokuza Kiswahili
Kuna taasisi zinazolenga kukuza na kuimarisha Kiswahili kama vile Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na idara za Kiswahili katika vyuo vikuu vingine vya Kenya na pia Uganda.

Nchini Tanzania kuna Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) ilhali nchini Kenya kuna Chama cha Kiswahili cha Taifa (CHAKITA). BAKITA na CHAKITA pamoja na wawakilishi kutoka Uganda wanaandaa kuundwa kwa Baraza la Kiswahili la Afrika Mashariki (BAKAMA).

Uchunguzi wa Kiswahili huendelea pia katika idara za vyuo vikuu vingi duniani, kwa mfano katika Institute National des Langues et Civilisations Orientales, jijini Paris, Ufaransa. Matumizi yake ni kwa njia ya lahaja za Kingwana.

Kamusi za Kiswahili
Makala kuu ya: Kamusi za Kiswahili
Kati ya shughuli muhimu za taasisi hizo, mojawapo ni kazi ya kukuza misamiati ya Kiswahili yaani kutafuta maneno mapya au kupanua matumizi ya maneno yaliyopo ili kutaja mambo ya maisha ya kisasa yaliyobadilika. Utunzi wa kamusi za Kiswahili hupanua elimu hiyo.

Faida za kutumia Kiswahili kwa mataifa ya Afrika
Faida za kutumia lugha ya Kiswahili zinatajwa kama ifuatavyo:

1. Husaidia kuleta umoja wa bara zima.
2. Hudumisha utamaduni wa Kiafrika kuliko kufuata kasumba.
3. Hufanya Waafrika waamini zaidi mambo yao kuliko kutegemea tu ya kigeni.
4. Hurahisisha mawasiliano baina ya watu wa Afrika Mashariki.
5. Husaidia kuwa na mahusiano ya kibiashara na watu mbalimbali.
6. Ni ishara ya kuwa huru na kushikamana.
7. Ni utambulisho wa jamii husika (utaifa).
8. Husaidia kukuza na kuendeleza sanaa.
9. Husaidia kuimarisha ulinzi na usalama katika taifa husika.
10. Husaidia kupata ajira katika vyuo na shule mbalimbali zinazofundisha lugha ya Kiswahili hata nje ya nchi.
11. Husaidia kuongeza idadi ya wanafunzi wa lugha hiyo watakaofanya vizuri katika masomo kwa kuyaelewa zaidi.
12. Husaidia kuikuza na kuieneza ndani na nje ya jamii

images - 2021-10-28T103539.064.jpeg
 
Kiswahili ni Kikongo
Kiswahili ni kiarabu
Basi waswahili ndiyo Mayahudi original wa kutokea Israel!! Makabila mengine yote Africa ni wametokana na wamisri wa kale kina farao!!... ..........Wayahudi hawa!! woote wata twaliwa siku ya kiama!

dhambi zao Mungu kesha futa! hii ni kauli ya Mungu mwenyewe siyo maneno yangu!...na wayahudi watapigwa mihuri maaalum wkt wa Mateso ya shetani ktk vita ya almagedonia!! tena unabii unatimia sana kwao hata sasa!

Fikiria tu walio fanya Biashara Africa Mashariki siyo waarabu peke yao!!......na wala wengi hawakufika ndani ndani huko waliishia pwani tu, kwa nini?? waliogopa Mbung'o! lkn huko kiswahili kipo! ni usipime kwa nini??

Watu pekee walioingia ndani ndani bara huko ni wazungu wapelelezi kina Stanley, Speke nk! hawa walifungua hata makanisa bara kuliko misikiti mbona kizungu hakikuzungumzwaaa?? km kiarabuuu!!,...badala yake wazungu wakaiga kiswahili (kiyahudi original)

kwa sababu kiswahili ndo Lugha original ya kiyahudi!! alichoongea Yesu! kwa kuwa kiarabu cha leo kina maneno mengi ya kiyahudi! ambayo nayo pia kiswahili kinayo!! na kiswahili ni Lugha ya kibantu! kwa hiyo wabantu wana maneno mengi ya kiyahudi! upo hapo!

kwa Muktadha huo basi wabantu wote ndo Wayahudi original!! haiwezekani Kiarabu kisambae EA na eti kisi sambae Ugiriki na India ambao wapo hapo karibu pua na mdomo!! kuliko huku mbali EA, comoro! huko! eti kisa Biashara!! hapo tumepigwa na kitu kizito halafu tuna cheka!!!

Waarabu wa leo ni Machotara wa kigiriki, Waroma, Spain waliozaa na na waafrica hasa hasa Misri ya kale!! na watumwa wa EA ya leo! ila walitukataa maksudi tu! hapo unabii wa Mungu ukatimia kuwa Chuma na udongo kamwe havita shikamana!!

rejea ndoto ya Nabii Daniel! inahusika kwa hili!! ...angalia tu vitoto vikisha changanya damu ya kiarabu sijui kizungu havitaki Waafrica wenzao weusi KM vitoto vya Obama vina date na wazungu tu!

kifupi Yesu alikuwa ni uzao wetu sie waswahili!! tena wkt anatafutwa kuuawa na Herode alikimbilia kujificha Kusini mwa Misri ya kale hapa ni East Africa tu! ili adui Herode asimuone! ..Pia Bustani ya Edeni iko kati ya mto Euphrates na Gihon, huu mto Gihon ndo Mto Nile wa leo! ila wazungu wameficha hili!

unaoanzia ziwa victoria!! viko ndani ya Bonde la ufa la EA, na hili bonde limeanzia middle East mpkaaa Msumbiji then inapandisha mpaka Nile! Mungu alitamka hivi ''ngambo ya mito ya kush mabinti zangu na wanangu wataniletea matoleo"

wkt anatamka hili tamko alikuwa Israel ya leo!...Hitimisho.........kama umesomaa hili bandiko na umefika hapa na hujaelewa kitu basi jua kwamba wewe si Myahudi original!!.......... lkn km umeeelewa kwa kufikia hapa Basi weye ni Myahudi mwenzangu hongera sana!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom