Lugha ya kiingereza ina mahusiano makubwa na ugonjwa wa presha

mdundo ngoma sana

JF-Expert Member
Jan 2, 2016
1,002
955
Leo nimetembelewa na mzungu ofisini,nilikuwa na jamaa zangu ghafla nikaona pumzi inaniishia ,na maneno yangu niliyojifunza form six pale tambaza yanakuwa machache sana,jasho lilikuwa likinitoka na miguu kutetemeka.midomo yangu ilikuwa mizito na ,the the the kwa idadi zilifika hata mia tano kwa muda mchache.kweli kiingereza ni tishio sana kwangu
 
Mkuu kama lugha ya Kiingereza inamahusiono na ugonjwa wa moyo basi watu wasiombe visa kwenda Uingereza, na ninawapa pole sana raia wao wanoongea hii lugha.
 
Leo nimetembelewa na mzungu ofisini,nilikuwa na jamaa zangu ghafla nikaona pumzi inaniishia ,na maneno yangu niliyojifunza form six pale tambaza yanakuwa machache sana,jasho lilikuwa likinitoka na miguu kutetemeka.midomo yangu ilikuwa mizito na ,the the the kwa idadi zilifika hata mia tano kwa muda mchache.kweli kiingereza ni tishio sana kwangu

Hofu na wasiwasi wako ndo maradhi yako!

Huna sababu ya kujisikia hivyo.

Kukosea ni jambo la kawaida sana.

Na mara nyingi huwezi kujua kitu au jambo bila kukosea kwanza.

Hivyo usiogope kukosea.
 
Daah!!
Mi mwenyewe last week nilikuwa nawapigisha wamarekani flani hivi tour pale kariakoo, asee nilikuwa nasahau hata maneno madogo tu kama onion, potatoe. Yaan ikawa najikuta nafikisha ujumbe vile ambavyo sikutarajia.
Jamani hii lugha kwa kweli ina taka moyo, hata mkuu wa nchi hua simlaum sana anavo iogopa
 
Nilikutana na mzungu ni journalist raia wa Ujerumani, alikuja Tanzania wakati wa ule ubalozi wa marekani ulipolipuliwa. Kwakweli aliniambia alipata mahaba na zege yaani yai chips na mishikaki, ananiambia kile chakula ni kitamu bwana. Na alikujua Posta Mpya pale kuna kijana alikuwa anazitengeneza vizuri akawa mteja mzuri. Kijana hakujua kizungu kabisa.

Mzungu aliotoa order
Kijana: chips egg far far or confuse?
Mzungu: confuse.

Yule mzungu alinisifia uwezo wa muuza chips kuwa mbunifu wa kutumia maneno yaliyomwezesha kuendesha biashara yake na kuelewana na yeye pia.
 
Unajua nini_?! Nikujiamini tu then utashangaa mwenyewe umeweza vipi

Then ukiwa unafanya practise ya kuongea hiyo lugha mbele ya watu au mtu utakuwa confident when speaking that language coz unakuta mtu anaongea kiingereza kizuri akiwa mwenyewe au na mtu aliemzoea sana Lakini akiwa na watu wengine hawezi, hii ni sababu ya kutokuzoea kuongea mbele za watu ambapo inafanya unakosa kujiamini kama kweli unaweza kuzungumza vizuri.
 
Kuna wale wanaosema wakilewa wanaongea Kiingereza vizuri.
 
mi nakumbuka nilimaliza mafunzo yangu katk kazi niliyokua nasomea, gafla nikaitwa kwenye company moja kubwa hapa mjini inajishuhgusha na masuala ya utalii, kilicho fuata nilipewa ramani, oxgen cylinder, na first aid kit huku projector ikiwa imewashwa nikaambiwa nitoe briefing kwa wageni kutoka 16 USA, huku maboss wa hiyo company wakiwa wananisimamia!! hhahahahahaahahahah asikwambie mtu nilipatwa na hali ambayo haina jibu. kumbukeni wamarekani hawatumii meter wala kilometer !! wao ni feet and miles. najisikia kucheka kwa kweli. nilichokifanya mpaka leo hii mimi ni mtu mkubwa wakuheshimika ndani ya company yetu.
 
Back
Top Bottom