lugha ya kichaga na uandikaji wake

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,845
2,667
kichaga kukiongea rahisi (kwa mchaga) ila kuandika ni ishu. kuna maneno hayaandikiki mfano:
  1. shira (vita). hiyo 'r' kwenye kizungu ingetamkwa read. r inateleza
  2. mara (majani). hiyo 'r' sijui inafanana na neno gani. labda usemapo 'lile' kiswahili cha dar
  3. ngambura (kipande cha nyama). hiyo 'r' kwa kiswahili ingetamkwa ramani
  4. lanye (jamani). hiyo 'l' kwenye kiarabu ingetamkwa allah l inakuwa nzito
  5. chi inyi phfo (sio mimi). hiyo phfo sijui kama inatamkwa hivyo
  6. halya (pale). mgongo wa ulimi unagusa kaakaa la juu la kinywa, sio kichwa cha ulimi
  7. kyikyi (nini). mgongo wa ulimi unagusa kaakaa la juu la kinywa
kuna maneno mengine mengi tu. kama kuna wajuzi watuwekee utaratibu wa kuyaandika hayo maneno magumu
 
Ukitaka kuandika kichaga kwa kutumia alphabet ya kiswahili lazima utapata shida, kwa sababu kiswahili na kichaga ni tofauti. Haina tofauti na kutaka kuandika kiingereza kwa kutumia kanuni na misingi ya lugha ya kiswahili (e.g. read= ridi, reed=ridi ?)

Naamini kuna alphabet ya lugha ya kichaga ambayo nio tofauti na ya kiswahili (Nitashangaa kama haiko documented, maana wachaga ni mojawapo ya walioanza kwenda shule mapema katika nchi yetu!).
 
Kuna kitabu nilishakiona kimechanganywa kiswahili na kichaga, ila vichaga viko vingi. Kisarufi, kiswahili na kingereza vinatumia sarufi za aina moja so inakuwa rahisi. Kama wapo wenye kamusi ya kichaga watuwekee hayo maneno
 
Hakuna kabila la Kichagga,kuna Wa-Machame kuongea kwao awasikilizani na Wa-Rombo,na Wa Rombo awasikilizani na kibosho nk, Kwa hiyo hawa ni kabila tofauti.Labda Lugha sio kabila.
 
tUTENGENEZE KAMUSI MDHEE YA KICHAGGA.
THATHA THIJUI TUANDHE NA ILE YA KICHAGGA CHA OLD MOSHI AU CHA MACHAME?
unaonaje kama tungeanza na kisukuma?
Hakuna kabila la Kichagga,kuna Wa-Machame kuongea kwao awasikilizani na Wa-Rombo,na Wa Rombo awasikilizani na kibosho nk, Kwa hiyo hawa ni kabila tofauti.Labda Lugha sio kabila.

wewe utakuwa mhaya. Wahaya wengi hawana 'h'. Wote warombo, marangu, machame, kibosho, n.k ni wachaga mkuu
 
kichaga kukiongea rahisi (kwa mchaga) ila kuandika ni ishu. kuna maneno hayaandikiki mfano:
  1. shira (vita). hiyo 'r' kwenye kizungu ingetamkwa read. r inateleza
  2. mara (majani). hiyo 'r' sijui inafanana na neno gani.
Mkuu nadhani na wewe umesahau kichagga chenu.
Hilo neno MARA mbona niliambiwa kuwa maana yake kwa kiswahili ni MATE ?
 
sijasahau kitu hapo. Uliza majani yanaitwaje. Hilo neno pia linamaanisha mate. Mbona neno mbuzi hulishangai? Lina maana ngapi?
 
Hichi si kiChagga. Ni kiMarangu ndio unaulizia.
Machame hakuna shida ya maandishi, tunatamka r kama "gh" itamkwavyo na waSwahili katika kusema "ghafla" kwa mfano, "maare" = majani
Sehemu inayohitaji matamshi "wa" kama kumaanisha watoto tunaandika "v" = "vana"

Sioni ugumu wa kuandika kiMarangu pia, mbona vitabu vya nyimbo za kiLutheri vya kiMarangu vimeandikwa na vinasomeka?
 
Sasa wakuu,
Mbona hawa wachaga hawaeleweki?
 
kichaga kukiongea rahisi (kwa mchaga) ila kuandika ni ishu. kuna maneno hayaandikiki mfano:
  1. shira (vita). hiyo 'r' kwenye kizungu ingetamkwa read. r inateleza
  2. mara (majani). hiyo 'r' sijui inafanana na neno gani. labda usemapo 'lile' kiswahili cha dar
  3. ngambura (kipande cha nyama). hiyo 'r' kwa kiswahili ingetamkwa ramani
  4. lanye (jamani). hiyo 'l' kwenye kiarabu ingetamkwa allah l inakuwa nzito
  5. chi inyi phfo (sio mimi). hiyo phfo sijui kama inatamkwa hivyo
  6. halya (pale). mgongo wa ulimi unagusa kaakaa la juu la kinywa, sio kichwa cha ulimi
  7. kyikyi (nini). mgongo wa ulimi unagusa kaakaa la juu la kinywa
kuna maneno mengine mengi tu. kama kuna wajuzi watuwekee utaratibu wa kuyaandika hayo maneno magumu

Umeshajifunza kichaga?
 
ote umchihie koshaa!!!!
maana yake nini?

gKundi umeuliza swali hilo hapo juu.

Preta akajibu hivi: unafuraha sana.

Naomba Preta atufundishe taratibu neno moja moja yaani maana ya

OTE......
UMCHIHIE.......
KOSHAA.......

HAYA Preta na WACHAGA wengine leteni tuition hapa.
 
unaonaje kama tungeanza na kisukuma?

Kuna kamusi kibao za kisukuma wazee...Kisukuma ni simple as kiswahili...ngosha,bebenang'ho,namhala na mengineyo sasa wewe hebu niambie neno gani la kisukuma ambalo hutaweza liandika?tena ukome kabisa na hiyo lugha....kuna vitabu kibao vya kisukuma...nenda BUJOLA mwanza utapata translations nyingi tu toka kwa wasukuma pia DICTIONARY utapata mkuu..so ondoa shaka kwenye hilo li lugha wajameni
 
Back
Top Bottom