Lugha wanazotumia wanawake kupiga mizinga zinafanana

Rationale

Member
Mar 13, 2021
24
98
Kuna kitu nimekigundua siku za hivi karibuni, na naona kinafanana na wadada wengi, hata baadhi ya marafiki zangu nao wameanza kukumbana nacho.

Inaonekana mahusiano ya kimapenzi imekuwa mojawapo ya chanzo cha mapato kwa wadada wengi, au kwa maneno mengine wewe mwanaume umekuwa chanzo cha mapato kwa mdada au wadada unaofahamiana nao na kutoka nao.

Unapochukua namba ya simu ya dada na kutoka naye kwa kinywaji au mlo wa mchana au wa jioni, inategemea jinsi alivyo na anavyojiweka lakini kifuatacho ni mzinga.

1) Kioo cha simu yangu kimepasuka au simu yangu imeharibika, sijui nafanyaje?

2) Nimefiwa na babu yangu mkoani, yaani hapa hata sijielewi

3) Kodi yangu ya nyumba imeisha, sijui unanisaidiaje?

4) Naumwa, nimeenda hospitali na nimeshamwona daktari, nimeishiwa hela ya dawa.

5) Kesho ni birthday yangu, hata sijui nafanyaje.

Kama yamekufika na wewe, ongezea yako hapa.
 
Kuna kitu nimekigundua siku za hivi karibuni, na naona kinafanana na wadada wengi, hata baadhi ya marafiki zangu nao wameanza kukumbana nacho.

Inaonekana mahusiano ya kimapenzi imekuwa mojawapo ya chanzo cha mapato kwa wadada wengi, au kwa maneno mengine wewe mwanaume umekuwa chanzo cha mapato kwa mdada au wadada unaofahamiana nao na kutoka nao.
Ilikua na mwanamke mmoja single mothet bwana katika kuwasiliana akasema naumwa malaria yaani nimelazwa siko poa eeehhh mimi nikajua hiki kizinga. Kama zali sinikakutana naye mtaani kabeba ndoo anatoka kusaga mahindi mbona alitamani aridhi ipasuke.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa naona "mizinga" inashulikiwa kwelikweli
Huku watu walitoa mbinu mbalimbali za kujilinda
 
Nimefiwa na babu yangu mkoani, yaani hapa hata sijielewi
Jibu: kwan bby ulikuwa unataka kumfufua? Acha tu wazike

3) Kodi yangu ya nyumba imeisha, sijui unanisaidiaje
Jibu: yan kwa jinsi ninavyo kupenda siwez ruhusu uteseke tena na kodi ya nyumba,utabeba vitu vyako uamie kwangu

Kesho ni birthday yangu, hata sijui nafanyaje.
Jibu: wooo kumbe!!? Ebu nipe no za wazazi wako niwapongeze kwa kuniletea malaika wa moyo wangu.
 
Back
Top Bottom