nakubaliana na wewe, lazima tujifunze lugha za kigeni angalau moja kwa kila mtu, mtu kuwa na uwezo wa uelewa bila lugha tayari ni mapungufu, tuyaondoe, unadhnai kwa nini watu wanakimbilia kupeleka watoto wao kwenye shule za kimombo, ni ili wapate exposure ya language na mengineyo, hilo sasa la hao watoto kutoweza ku perform academically ni uvivu na usharobaro wao wenyewe, hivi ni lini unadhnai kiswahili kitakuwa lugha ya kimataifa, nadhani itachukua muda kidogo, kwa hiyo wakati tukisubiri hayo yatokee sisi tuendelee kumwaga ung'eng'e.
Nashangaa sasa hivi watu wako busy kubadili majina ya vitu vya wazungu kuwa kiswahili hebu angalia hapa chini kwanza:
Decorder=king'amuzi
Television=Runinga
Refridgerator=jokofu
Calculator= kolokotoa
Monopoly=ukiritimba
bureaucracy=umangimeza
Glass=bilauri
feedback=usuli
Guidelines=hadidu za rejea
na mengine mtaongezea mkiyakumbuka
Hivi ni mangapi kati ya haya maneno yanatumika, nasikia mpaka masomo ya sayansi wanataka kuyafundisha kiswahili, unajifunza urubani kwa kiswahili ukiingia kwenye cockpit unakuta instruments zote zimeandikwa kizungu. unafanyaje, jifunzeni kimombo shauri yenu.
bureaucracy ni urasimu sio umangimeza.