Lugha moja itawale ulimwengu?

Exaud J. Makyao,

ulishangaa Kwa nini mimi naona hatutakuwa na lugha rasmi 1 duniani na palepale nasema pia ya kwamba watoto wetu labda watajifunza Kichina.

Ni hivi: tutaendelea kuwa na lugha ambazo ni muhimu zaidi kimataifa kuliko nyingine. Kwa sasa Kiingereza ni lugha muhimu sana kitaendelea kuwa vile kwa muda. Siamini milele. Lugha nyingine zitakuwa muhimu zaidi kuliko leo ninahisi: Kichina, lakini bila shaka pia kwa muda.

Bado naona ni baraka kuwa na lugha nyingi na uwingi wa tamaduni. Tujifunze lugha 2, 3, 4 ili tuweze kuwasiliana na wengi!
 
Tofauti zetu ndiyo sura ya ulimwengu. tukiacha tofauti zetu, whether it be language, culture or beliefs, ili tuondoe ukabila au ubaguzi tutakuwa tuemkosea.

anayekubagua sio lazima awe kutoka kabila lingine au taifa lingine. Ndugu zetu wenyewe wanabaguana kwa sababu wana uwezo zaidi, wengine wamezaliwa mjini na mambo mengine yasiyo ya msingi.

Ingelikuwa vyema tuendelee na tofauti zetu ila tujifunze kuishi nazo na kuishi na watu wenye lugha tofauti, tamaduni tofauti na mitazamo tofauti
 
Ni wazo zuri makyao. Lakini nani atakubali kuacha lugha yake akumbatie ya mwenzie?
Pia ingekuwa vema ukitoa mapendekezo ya namna ya kuanzisha hiyo lugha na namna ya kumfikishia kila binadamu wa kila sehemu. Mfano, tukichukua kichagga kiwe lugha hiyo, tunaanzia wapi?

wabongo tuko tayari kabisaaa
 
Dunia ya sasa inataka mtu ajue lugha nyingi awezavyo.Kwamba ULIMWENGU unaweza kukubaliana kuwe na lugha moja tu... kwa maoni yangu naona itakuwa ngumu.... chukulia mfano wafaransa walivyo na kiburi na lugha yao.Ukienda kwao hata kama wanajua kiingereza, ukiwasemesha hawatajali kukujibu..inabidi uanze kutafuta vocabulaire yako iliyopotea miaka mingi uweze angalua kuomba maji.Lugha ni utambulisho - mara nyingi lugha zilizokomaa, wenyewe hawatapenda kuzipoteza na watazilinda kwa gharama yoyote ile.Hapa Tanzania kuna mapambano kutaka kukipandisha kiswahili kwenye chati zaidi ili angalau kiwe moja ya lugha zenye kutumika angalau kwenye bara la Africa....jitihada hizi haziko kwenye kiswahili tu, ziko pia kwenye lugha nyingine kama kihausa n.k. Mwelekeo nionavyo hauko katika kupata lugha moja bali kueneza lugha nyingi zaidi ulimwenguni.


na majina ni utambulisho. tunakubali hiki tunapinga kile
 
BLURAY,
Hitimisho lako linanitia wasiwasi.
Je ni lazima A akishindwa na B ashindwe?

Kama kuna uhusiano unaoshabihiana kwa karibu kabisa kati ya A na B, watu wanaotumia reason wataweza kuchukua uzoefu wa kushindwa kwa A katika ku asses uwezo wa kufanikiwa/ kushindwa kwa B.

Ushabihiano kati ya A na B hapa ni lengo la kutaka kufanya dunia iwe na lugha moja.

Ikiwa leo kuna watu Brazil hawajui Kireno, Guatemala na Mexico hawajui Kihispania na Tanzania hawajui Kiswahili, je unafikiri itakuwa practical dunia nzima iwe na lugha moja?

Dunia yetu inatajirishwa na wingi wa lugha zetu, kuna wanasosholojia wanafanya juu chini kuzinusuru lugha za watu wa Papua New Guinea (the most linguistically diverse place on earth) ili zisife, kwa maana kila lugha ina johari na hazina za kiutamaduni.Kuna Wsandawi na Ma Bushmen wanaoongea kwa kutumia sauti tofauti kabisa na Waingereza.Wakati Waingereza wana characters 26 katika alphabet yao, Wachina wana zaidi ya mia moja na kama unataka kuhesabu variations unaweza kupata characters mpaka 3,500. Sasa kama unataka kutumia Kiingereza si utam shortchange Mchina? Na kama unataka kutumia Kichina si utamchangenya Muingereza, na kama unataka kutengeneza lugha mpya si utawachanganya wote?

Kuwa na lugha moja ni ndoto ya Ki-Selassie, ya kufukuzwa bila kuweza kuipata.
 
Ndugu Exaud J. Makyao haiwezekani kukawa na lugha moja itawale duniani Mungu hakukosea kuumba watu wa Mataifa mbali mbali ili tupate kujuana wale wachina wale Wazungu waarabu Waafrika na wale Wa Asia kukiwa na lugha moja itakuwa kuipendelea hiyo lugha kuonekana kuwa lugha kubwa kuliko zingnine angalia Umoja waulaya kila mbunge akiingia bungeni anazungumza lugha yake sio lazima ajuwe lugha ya kiingereza upo hapo [URL="https://www.jamiiforums.com/members/exaud-j-makyao.html"]Exaud J. Makyao [/URL]
 
Toka mwanzo ilikuwa ni makusudio ya Mungu dunia iwe na mchanganyiko wa lugha (waaminio biblia watakubaliana nami), mfano mzuri ni pale Mungu alipomwambia Ibrahim wakti ule hana mtoto, alimwambia kuwa usisikitike nitakufanya kuwa baba wa mataifa (na ili kuwe na mataifa lazima kuwe na tofauti ya utamaduni, na lugha ni sehemu ya utamaduni), lakini kuon esha ubaya wa kuwa na lugha moja dunia nzima, hebu turejee hadithi ya Mnara wa Babeli.
 
Toka mwanzo ilikuwa ni makusudio ya Mungu dunia iwe na mchanganyiko wa lugha (waaminio biblia watakubaliana nami), mfano mzuri ni pale Mungu alipomwambia Ibrahim wakti ule hana mtoto, alimwambia kuwa usisikitike nitakufanya kuwa baba wa mataifa (na ili kuwe na mataifa lazima kuwe na tofauti ya utamaduni, na lugha ni sehemu ya utamaduni), lakini kuon esha ubaya wa kuwa na lugha moja dunia nzima, hebu turejee hadithi ya Mnara wa Babeli.
Unataka kutuambia kuwa kabla ya mnara wa babel lugha ya dunia ilikuwa moja!?
 
Hili lilishajaribiwa na lugha ya Esperanto ambayo ilishindwa vibaya sana, it is not practical at all.Ukitaka kujifunza how impractical this is study the fall of Esperanto.

Je, ulifuata shauri lako? Ulifanya utafiti kuhusu "the fall of" Kiesperanto? Kwa nini unaazima kwamba lugha ya Kiesperanto ilishindwa "vibaya sana"? Mimi mwenyewe naongea Kiesperanto pamoja na watu wengi ulimwenguni. Tafadhali soma zaidi (www.afriko.org)!

Lugha ya Kiingereza ni lugha ya ukoloni mamboleo.
 
Je, ulifuata shauri lako? Ulifanya utafiti kuhusu "the fall of" Kiesperanto? Kwa nini unaazima kwamba lugha ya Kiesperanto ilishindwa "vibaya sana"? Mimi mwenyewe naongea Kiesperanto pamoja na watu wengi ulimwenguni. Tafadhali soma zaidi (www.afriko.org)!

Lugha ya Kiingereza ni lugha ya ukoloni mamboleo.

SALEH,
Nimefurahia sana hiyo changamoto yako.
Naamini waliozungumzia KUSHINDWA KWA KIESPERANTO wataweza kuleta hoja zao za uthibitisho..
 
Kiesperanto, lugha iliyokuwa na aspiration ya kuwa lugha ya dunia, mpaka leo inaongewa na watu wangapi? Na imekuwapo kwa miaka mingapi?

Mbona unataka kukipa chati wakati hata wanaoongea kisukuma ni wengi zaidi? Lugha ya dunia hii? Walioandika story ya mnara wa Babeli, however mythological, walikuwa wana point kubwa sana ingawa wao walii reverse engineer idea nzima ya kwamba huwezi kuwa na lugha moja.

Kama Kiingereza ni ukoloni mamboleo, kiesperanto au lugha yoyote ya dunia itakayokuja itakuwa ya ukoloni zandiki mambokesho.
 
Kiesperanto, lugha iliyokuwa na aspiration ya kuwa lugha ya dunia, mpaka leo inaongewa na watu wangapi?
..............................Mbona unataka kukipa chati wakati hata wanaoongea kisukuma ni wengi zaidi? .

Kweli???????
 
Back
Top Bottom