Lugalo kusafisha figo kwa bei nafuu

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1571901779223.png

Tanzania imeendelea kuboresha huduma zake katika sekta ya afya nchini baada ya Hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo jijini Dar es Salaam jana kuzindua huduma ya kusafi sha fi go ambayo itakuwa inalipiwa Sh 180,000 kila mgonjwa anapokwenda kusafi shwa.

Hospitali hiyo ya jeshi inaungana na hospitali nyingine kama Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Regency zote za jijini Dar es Salaam, Benjamin Mkapa jijini Dodoma, kutoa huduma hiyo muhimu kwa wenye matatizo ya figo. Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo itakuwa inatoa huduma hiyo kwa wanajeshi pamoja na raia kwa gharama nafuu ambayo itakuwa ikitolewa kwa gharama za kawaida za serikali; kwa atakayetaka kutibiwa kwa fedha taslimu atalipia Sh 180,000 na pia iko huduma kwa bima ikiwamo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Gharama hiyo ya Sh 180,000 ni nafuu ambayo ni sawa na inayotozwa na Muhimbili kwa wanaofikishwa hapo na wale wa kujitegemea wanalipa Sh 400,000, wakati Benjamin Mkapa wanatoza Sh 250,000, zote kwa kila mgonjwa anapokwenda kusafishwa. Mara nyingi mgonjwa husafishwa kati ya mara mbili au tatu kwa wiki kutegemeana na hali ya tatizo lake.

Pia kuna vifaa vinavyoweza kuhudumia wagonjwa 10 kwa wakati mmoja na hadi sasa wenye uhitaji wa kusafishwa figo 19 wameshahudumiwa wakati wa kipindi cha majaribio kabla ya uzinduzi wake huo rasmi. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk Hussein Mwinyi ndiye aliyezindua huduma hiyo jana hospitalini hapo ukienda sambamba na uzinduzi wa jengo jipya litakalokuwa likitumika kutolea huduma hiyo.

Alisema jeshi linapaswa kuwa mfano wa kuigwa katika ufanisi wa utoaji wa huduma mbalimbali zikiwamo za afya huku akiwakumbusha kuwa kwa kutoa huduma bora za afya wanakuwa wanatekeleza sera za serikali za kuimarisha huduma bora za afya kwa Watanzania. Alisema uzinduzi wa huduma hii ya kusafisha figo umefanyika wakati mwafaka ambao serikali imekuwa ikiongeza ufanisi zaidi katika utoaji wa huduma zake za afya kwa wananchi.
 
tumia njia ya kienyeji kusafisha figo...madafu lita tano kwa siku tiba tosha!!
 
Hii huduma serikali iangalie upya; hili ni tatizo la kudumu kama ilivyo wagonjwa wa ukimwi; TZS 180,000 kwa wiki mara tatu ni sawa na TZS 540,000 kwa wiki na kwa mwezi ni TZS 2,160,000 kwa mwaka ni TZS 25,920,000. Bahati mbaya zaidi wanaopatwa na hili tatizo wengi ni wale wenye umri mkubwa na pengine walishastaafu utumishi hivyo hawana kipato kikubwa.

Chonde chonde Serikali ilibebe hili tatizo kwa kodi zetu kwani hata hizo mashine za Lugalo ni kodi zetu. Mwezi July 2019 nimemzika ndugu yangu kwa tatizo hili na ni bahati mbaya zaidi vifo wa wagonjwa wa figo huharakishwa kwa umaskinin wao yaana kukosa pesa ya kusafisha au kuotesha figo.
 
Kodi gani wewe unayolipa. Nchi maskini Hii Hata ulaya hiyo nayo Ni issue nzito. La Msingi tujitunze.
 
Kodi gani wewe unayolipa. Nchi maskini Hii Hata ulaya hiyo nayo Ni issue nzito. La Msingi tujitunze.
Kwa hiyo wewe unaona bora kodi itumike kuhudumia watu waliopata maambukizi kwa ngono uzembe kuliko wagonjwa wa kisurikari ambao baadhi wameupata kutokana na "stress" za haya maisha ya Bongo?
 
Kimsingi hawasafishi figo ila wanasafisha damu (dalaysis), figo zinakua zimefeli kwa hiyo kuna kua na mrundikano wa sumu nyingi kwenye damu,
 
Back
Top Bottom