Lugalo Hospitali kuna mkanganyiko juu ya malipo ya extra shift kwa wafanyakazi wa afya

Rosena

Member
Sep 11, 2012
51
4
Ulitolewa waraka juu ya malipo ya extra shift allowance kwa wafanyakazi wa afya kama ifuatavyo;
1. Wale wenye degree moja sh 15,000/ kwa siku
2. Mabingwa (degree mbili na kuendelea) sh 25,000/- kwa siku.

Matatizo yaliyojitokeza;

Kwa maslahi binafsi ya kundi la watu, wameamua kutoa viwango hivyo kinyume na waraka kwa kuleta tafsiri ya degree hizo ambazo zote ni muhimu ndani ya vitengo vya hospitali. hapa Lugalo kuna kitengo cha Social Work (Ustawi wa jamii) na huduma ya ustawi wa jamii ni moja ya vitengo muhimu ndani ya hospitali yoyote. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Lakini hapa wanasema,wenye Degree ya ustawi wa jamii hawastahili kulipwa kwa viwango vilivyoainishwa na waraka huo kwa siku. Huu ni uonevu na uzalilishaji wa fani. Sasa kitengo hiki cha nini hapa hospitali kama hakina umuhimu?
 
Mkuu Rosena, Poleni mkuu,...join tbe club in number of hospitals..ukiangalia kwa umakini hilo tatizo halipo hapo tu Muhimbili, M'nyamala, Amana, Bugando, Mbeya, KCMC na nyingine nyingi...ila ndio kile "kuridhika" kwa watumishi na wanaogopa kusema kwani walishaambiwa "asiyeweza na aende huko wanakoweza kumlipa hivyo"

I think on call allowances should be reviewed again, na ndio maana hospitali nyingi kwa sasa watu hawakanyagi call KABISA, if workibg hours zimeisha watu wanaondoka..na hii itakuwa mbaya kwani itafikia hata hatua ya emergency services tu..mtu anaona, kama hamwezi kunilipa on call allowances kwanini mniite?!

Hali hii ikiendelea, huduma za Afya katika hospitali zetu zitazidi kuwa mbaya zaidi ya ilivyo sasa.
 
Inabidi utaratibu ufuatwe kurejesha matumaini madogo waliyonayo watumishi wengi ndani ya hospitali zetu, vinginevyo watu wataendelea kupata huduma mbovu kwani watoaji wa huduma wana machungu mioyoni mwao.
 
Back
Top Bottom