Ludovick Mwijage: The Dark Side of Nyerere's Legacy

Mkuu hii ukiisoma humtamani Nyerere, jamaa kaelezea karibu mambo yote maovu ya Mwalimu ambayo siku hizo yalifanywa kwa siri na kufichwa na utawala wa kidikteta wa Mwalimu, kwa kuwa Mwalimu alidhibiti vyombo vya habari vyote, hakuna aliyethubutu kuhoji, wala kujuwa undani wa maovu ya rushwa, ukatili na ukiukwaji wa haki za binaadamu uliofanana na tawala nyingi za kidikteta za kiafrika wakati huo.

Udikteta wa Nyerere wa kudhibiti wapinzani wa serikali na uhuru wa kutoa maoni na kujieleza kwa ukatili wa namna kama hizo za yaliyowakuta akina Mwijage na wenzake, umefichwa na kumfanya Nyerere asionekane mwenye mikono ya damu, lakini hakuna jambo ovu litakalofichika, kama Nyerere alifunga milango ili watanzania wasijuwe ukatili wa utawala wake, basi milango mingine ipo wazi kufunua maovu hayo.

To be heard is a natural right. It’s one side of the story. Kama msomi naomba Ufahamu Hilo. Upo hapa kwa kuwa huyo Nyerere na wenzake wametufanya Hivi tulivyo. Amefanya pake. Na Sisi tufanye yetu. Wakati wake ulikuwa tofauti. Mwanzo. Imagine kuongoza familia ilivyo na changamoto and sembuse nchi.
 
Kwani Ludovick Mwijage ni mnyama gani? Maana katika binadamu amvao Mwalimu Nyerere alikuwa na upinzani nao sijawahi kumsikia. Kimsingi tukiupa nafasi mjadala huu basi kila Mtanzania anaweza kudai kuwa aliteswa na Nyerere. Tumdharau author kama crap material.
Mkuu ni kwamba haumini asemacho ama hutaki ukweli wake?
 
Nina umri mkubwa na mengi nimeyaona. Sisubiri kuamdikiwa na Ludovick Mwijage. Ametumia tu haki yake ya kujieleza
Ni kweli husibiri kuandikiwa na Ludovic, lakini haimanishi alichoandika ni uongo. Labda useme unajua mengi kuhusu Nyerere, kitu ambacho hakipunguzi ukweli wa Ludovic.
 
It is not a fiction we are used to like those authored by African writers; Ngugi wa Thiongo, Chinua Achebe, Ole Soyinka and other you know.. not, it is real life experience;

Kitabu cha The Dark Side of Nyerere, ni simulizi ya kweli ya masaibu aliyoata Ludovick Mwijage kwenye utawala wa Nyerere. Ludovick Mwijage alikuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa mfumo wa utawala wa Mwl Nyerere ambaye wakati huo alikuwa Rais wa Tanzania.
View attachment 2835669

Katika kitabu hiki cha the dark side of Nyerere's legacy Mwandishi anaanza kwa kurejea Jiji la Manane huko Afrika ya Kusini,mnamo Desemba 6 mwaka 1983,akiwa amemaliza kula mlo wa mchana akiwa na rafiki yake John kutoka Kenya ambaye alikuwa fundi wa magari, na wakati fulani ndie alikuwa akatengeneza gari ya Mfalme Moshoeshoe wa Lesotho, katika mazungumzo yao huyu mkenya alimjulisha mwandishi kuwa passport yake ilikuwa imechukuliwa hotelini kutokana na kushindwa kulipa deni la hoteli.

Mwijage anasema alikimbilia Mbambane kutafuta hifadhi baada ya hali yake kuwa. mbaya Tanzania, Ludovick Mwijage alikuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa mfumo wa utawala wa Mwl Nyerere ambaye wakati huo alikuwa Rais wa Tanzania,mwanzoni alikimbilia Nairobi Kenya ambako aliwekwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Thika, ila baadae aliona Kenya sio salama kwake,akaamua kukimbilia Swaziland Januari 1983. Kasisi mmoja wa kanisa Katoliki kutoka Ujerumani ndie aliyempa mwandishi kiasi cha 4200 Kenya shillings, ambayo ingemtosha kulipia tiketi ya Ndege kupitia Sudan ila alilazimika kuwapa marafiki zake wawili waliokuwa wametorokea Uganda ili waingie Sudan, maana Uganda bado ilikuwa na maofisa wengi wa usalama kutoka Tanzania! hawa rafiki zake waliokuwa wanakimbia mkono wa Nyerere hawakuwa na fedha tena, aliwatumia kiasi fulani na yeye Mwijage akatafuta hela zaidi kutoka kwa rafiki zake wa ng'ambo.

Mwijage anasema wakati anaondoka Kenya kwa msaada wa rafiki zake wa Ng'ambo hasa Ujerumani Mashariki, hakuwa na chochote zaidi ya mswaki,dawa ya meno, singlend, nguo moja ya ndani ya kubadili na karatasi zilizokuwa na mawasiliano ya rafiki zake wa Tanzania na Ujerumani. Wakati huo ukiwa na pasipoti ya nchi wanachama wa jumuia ya madola hakukuwa na haja ya visa kwenye nchi wanachama! alifika Mbabane akatoka na kuanza kutafuta sehemu gesti ya kufikia. Akiwa kwenye mitaa kutafuta sehemu ya kufikia ghafla alikutana na Mtanzania ambaye alikuja kugundua ni mtabiri maarufu wa nyota Sheikh Yahya Hussein.

Alitambua Sheikh Yahya Hussein kutokana na kumwona kwenye magazeti mbalimbali akitangaza biashara yake ya utabiri. Hapa Mbabane alikuja kwa kazi hiyo ambayo alikuwa anajiita Mtabiri, Nabii, Mnajimu, Mponyaji, ukiwa na tatizo lolote yeye anasafisha nyota yako! Sheihk Yahaya alimkaribisha nyumbani na kwa kuwa alikuwa ni Sheikh Mwandishi hakuwa na wasiwasi, walipofika Yahya alimtaka Mwandishi aeleze kisa chake, hata hivo Sheikh Yahaya alikuwa anajua kisa cha Mwijage. Sheikh Yaya alijitolea kumlipia gesi kwa siku kadhaa!

Katika mazingira ambayo ni tatanishi mwandishi alijikuta baadhi ya nyaraka zake hazionekani
Hata hivo nchi ya Swaziland ilimpa hati ya mkimbizi wa kisiasa ndani ya wiki moja.Mwandishi anasema kuwa anakumbuka mazungumzo yake na yule Mkenya kuhusu siasa za Afrika na Afrika Mashariki,kwa sehemu kubwa watu wasio Watanzania walikuwa anamwona Nyerere shujaa wa Afrika hasa imani yake ya Ujamaa na kwamba Mwafrika ni socialist kwa asili!ndivo aliamini Nyerere!

Aliamini tofauti na alishangaa Afrika kuwa maskini, na ukosefu wa Demokrasia,Mwijage aliamini ukosefu wa Demokrasia na mfumo wa vyama vingi ni kinyume na haki za binadamu na kwamba ingechelewesha maendeleo ya vitu na ya watu!pia ingepelekea utegemezi wa wahisani kwa kipindi kirefu sana.

Kusoma zaidi chukua kitabu kilichokuwa attached hapo chini
Duu huyu ndio Nyerere !
 
Nimesoma kitabu chote

Nilikuwa naamini Nyerere alikuwa ni mshenzi, ila hiki kitabu kimenithibitishia sio tu alikuwa ni mshenzi bali pia ni mnyama na katili, pia kuongezea upumbavu wake uliotutia umasikini.
 
Back
Top Bottom