Ludovick Mwijage: The Dark Side of Nyerere's Legacy

Sophist

Platinum Member
Mar 26, 2009
4,484
3,400
It is not a fiction we are used to like those authored by African writers; Ngugi wa Thiongo, Chinua Achebe, Ole Soyinka and other you know.. not, it is real life experience;

Kitabu cha The Dark Side of Nyerere, ni simulizi ya kweli ya masaibu aliyoata Ludovick Mwijage kwenye utawala wa Nyerere. Ludovick Mwijage alikuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa mfumo wa utawala wa Mwl Nyerere ambaye wakati huo alikuwa Rais wa Tanzania.
1701948364124.jpeg

Katika kitabu hiki cha the dark side of Nyerere's legacy Mwandishi anaanza kwa kurejea Jiji la Manane huko Afrika ya Kusini,mnamo Desemba 6 mwaka 1983,akiwa amemaliza kula mlo wa mchana akiwa na rafiki yake John kutoka Kenya ambaye alikuwa fundi wa magari, na wakati fulani ndie alikuwa akatengeneza gari ya Mfalme Moshoeshoe wa Lesotho, katika mazungumzo yao huyu mkenya alimjulisha mwandishi kuwa passport yake ilikuwa imechukuliwa hotelini kutokana na kushindwa kulipa deni la hoteli.

Mwijage anasema alikimbilia Mbambane kutafuta hifadhi baada ya hali yake kuwa. mbaya Tanzania, Ludovick Mwijage alikuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa mfumo wa utawala wa Mwl Nyerere ambaye wakati huo alikuwa Rais wa Tanzania,mwanzoni alikimbilia Nairobi Kenya ambako aliwekwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Thika, ila baadae aliona Kenya sio salama kwake,akaamua kukimbilia Swaziland Januari 1983. Kasisi mmoja wa kanisa Katoliki kutoka Ujerumani ndie aliyempa mwandishi kiasi cha 4200 Kenya shillings, ambayo ingemtosha kulipia tiketi ya Ndege kupitia Sudan ila alilazimika kuwapa marafiki zake wawili waliokuwa wametorokea Uganda ili waingie Sudan, maana Uganda bado ilikuwa na maofisa wengi wa usalama kutoka Tanzania! hawa rafiki zake waliokuwa wanakimbia mkono wa Nyerere hawakuwa na fedha tena, aliwatumia kiasi fulani na yeye Mwijage akatafuta hela zaidi kutoka kwa rafiki zake wa ng'ambo.

Mwijage anasema wakati anaondoka Kenya kwa msaada wa rafiki zake wa Ng'ambo hasa Ujerumani Mashariki, hakuwa na chochote zaidi ya mswaki,dawa ya meno, singlend, nguo moja ya ndani ya kubadili na karatasi zilizokuwa na mawasiliano ya rafiki zake wa Tanzania na Ujerumani. Wakati huo ukiwa na pasipoti ya nchi wanachama wa jumuia ya madola hakukuwa na haja ya visa kwenye nchi wanachama! alifika Mbabane akatoka na kuanza kutafuta sehemu gesti ya kufikia. Akiwa kwenye mitaa kutafuta sehemu ya kufikia ghafla alikutana na Mtanzania ambaye alikuja kugundua ni mtabiri maarufu wa nyota Sheikh Yahya Hussein.

Alitambua Sheikh Yahya Hussein kutokana na kumwona kwenye magazeti mbalimbali akitangaza biashara yake ya utabiri. Hapa Mbabane alikuja kwa kazi hiyo ambayo alikuwa anajiita Mtabiri, Nabii, Mnajimu, Mponyaji, ukiwa na tatizo lolote yeye anasafisha nyota yako! Sheihk Yahaya alimkaribisha nyumbani na kwa kuwa alikuwa ni Sheikh Mwandishi hakuwa na wasiwasi, walipofika Yahya alimtaka Mwandishi aeleze kisa chake, hata hivo Sheikh Yahaya alikuwa anajua kisa cha Mwijage. Sheikh Yaya alijitolea kumlipia gesi kwa siku kadhaa!

Katika mazingira ambayo ni tatanishi mwandishi alijikuta baadhi ya nyaraka zake hazionekani
Hata hivo nchi ya Swaziland ilimpa hati ya mkimbizi wa kisiasa ndani ya wiki moja.Mwandishi anasema kuwa anakumbuka mazungumzo yake na yule Mkenya kuhusu siasa za Afrika na Afrika Mashariki,kwa sehemu kubwa watu wasio Watanzania walikuwa anamwona Nyerere shujaa wa Afrika hasa imani yake ya Ujamaa na kwamba Mwafrika ni socialist kwa asili!ndivo aliamini Nyerere!

Aliamini tofauti na alishangaa Afrika kuwa maskini, na ukosefu wa Demokrasia,Mwijage aliamini ukosefu wa Demokrasia na mfumo wa vyama vingi ni kinyume na haki za binadamu na kwamba ingechelewesha maendeleo ya vitu na ya watu!pia ingepelekea utegemezi wa wahisani kwa kipindi kirefu sana.

Kusoma zaidi chukua kitabu kilichokuwa attached hapo chini
 
Attachments

  • the-dark-side-of-nyerere-1.pdf
    179 KB · Views: 19
Mkuu hii ukiisoma humtamani Nyerere, jamaa kaelezea karibu mambo yote maovu ya Mwalimu ambayo siku hizo yalifanywa kwa siri na kufichwa na utawala wa kidikteta wa Mwalimu, kwa kuwa Mwalimu alidhibiti vyombo vya habari vyote, hakuna aliyethubutu kuhoji, wala kujuwa undani wa maovu ya rushwa, ukatili na ukiukwaji wa haki za binaadamu uliofanana na tawala nyingi za kidikteta za kiafrika wakati huo.

Udikteta wa Nyerere wa kudhibiti wapinzani wa serikali na uhuru wa kutoa maoni na kujieleza kwa ukatili wa namna kama hizo za yaliyowakuta akina Mwijage na wenzake, umefichwa na kumfanya Nyerere asionekane mwenye mikono ya damu, lakini hakuna jambo ovu litakalofichika, kama Nyerere alifunga milango ili watanzania wasijuwe ukatili wa utawala wake, basi milango mingine ipo wazi kufunua maovu hayo.
 
Mkuu hii ukiisoma humtamani Nyerere, jamaa kaelezea karibu mambo yote maovu ya Mwalimu ambayo siku hizo yalifanywa kwa siri na kufichwa na utawala wa kidikteta wa Mwalimu, kwa kuwa Mwalimu alidhibiti vyombo vya habari vyote, hakuna aliyethubutu kuhoji, wala kujuwa undani wa maovu ya rushwa, ukatili na ukiukwaji wa haki za binaadamu uliofanana na tawala nyingi za kidikteta za kiafrika wakati huo. Udikteta wa Nyerere wa kudhibiti wapinzani wa serikali na uhuru wa kutoa maoni na kujieleza kwa ukatili wa namna kama hizo za yaliyowakuta akina Mwijage na wenzake, umefichwa na kumfanya Nyerere asionekane mwenye mikono ya damu, lakini hakuna jambo ovu litakalofichika, kama Nyerere alifunga milango ili watanzania wasijuwe ukatili wa utawala wake, basi milango mingine ipo wazi kufunua maovu hayo.

ndugu yangu junius unakuwa mwepesi sana wa kujudge mambo ya upande mmoja, hiyo statment au maelezo ni ya upande mmoja tu, wewe unaamini vipi kwamba huo ndio ukweli halisi.

Pili huyu bwana na kikundi chake inaonekana ni kikundi cha ukabila (HAYA TRIBE) na kwa asilimia kubwa kina ushirikiano mkubwa na nchi ya jirani Uganda kutokana na maelezo ya huyo bwana.

TATU hakuna kiongozi au state yoyote inayoweza kusimama bila ya damu kumwagika na watu kupata mateso makuu, hata Muhamadi alipokuwa anasimamisha dini watu wengi walikufa kwa sababu tu ya kutomwamini/kutomkubali, sasa iweje unashangaa ya Nyerere, lakini hata tukimwacha Nyerere je waliomfuata walishakuwa na mambo kama hayo ya Nyerere, ndugu yangu Junius hebu angalia vifo vya utata vya KOLIMBA, KOMBE, MALIMA, BALALI, sasa hapa utamshirikisha Nyerere, wewe umecomment hii issue kwa chuki za dhairi kwa Nyerere.

kuna mambo mengi tu yanatokea na kuna watu wengi tu wanashindwa hata sasa kukanyaga Tanzania japo Nyerere keshakufa, ajali ya Mwakyembe mpaka leo ni utata mtupu, kifo cha Wangwe mpaka leo ni utata mtupu,

NNe, sio Tanzania tu ndio watu walikuwa wapo detained hiyo nni system ya dunia nzima, Moi aliua (R.Auko na wengineo), Iddi Amini alikua, Bush, Putin, na viongozi almost wote katika hii dunia

Mwisho kabisa, ni kwamba usijudge vitu kwa chuki binafsi hata kama ni kweli huyo bwana aliteswa lakini alikuwa anadeserve kwa sababu alikuwa kinyume na misingi iliyokuwa inasimamishwa wakati ule, na sio yeye tu hata Kambona alishindwa ile misingi na akaamua kutimkia UK
 
Kituko,
Nashindwa kukuelewa unachokubali kipi na kipi unakataa. Kweli sipendi maovu ya Nyerere na sitaki unifanye niamini kuwa hakuwa nayo.
 
Kwani kitabu ni kitu gani hasa cha kumaanisha kuwa jambo hilo ni kweli!

Mbona kuna vitabu vya dini vingine ni vya uongo kabisa kabisa lakini watu wanaviamini na wako tayari kuua na kufa kuvitetea!

Kinacho mata ni kweli hayo?
 
Ludovick, kwa vijana wa hapa naona utadunda, tafuta watu wa kuzungumza nao. Hata huku kwetu Zanzibar unapo jaribu kutowa machafu ya Karume, utaambiwa ahaa kutokana na hali ya hewa ya wakati huo, basi alipaswa, kuuwa, na yote yaliyo machafu, hata kuwachukuwa wake za wapizani wao. Haya kwa vijana wa Jamii forum ni sawa sawa...

Ubaya lazima usemwe, Mitume waliteswa kwasababu wakisema ukweli na kwa imani ya ki-islamu waumini wote wa kweli ni warithi wa Mitume kwa kufanya kazi hiyo hiyo yakuambrisha yale yaliyo ambrishwa kwenye Qur-an, inawezekana na Bible ina ujumbe huo huo, kwa hiyo usichoke kusimamia haki japo kuwa kuna wachache watachukia
 
Hata mimi baada ya kusoma simulizi la Ludovick Mwijage nilipunguza Imani kwa Hayati JK!
Ludovick aliteswa sana na nyendo alizopitia ni dhahiri kabisa kulikuwa na Udikteta wa siri siri!
Ila kila jambo lina mwisho wake!

Mara nyingi viongozi wa huwa hawawapendi wanaowapinga kwa hoja nzit hasa inapotokea Siasa ni za Zidumu Fikra Sahihi za kama Mwenyekiti wa CCM!

Ludovick mwijage Mie namwonaga kama Shujaa!
 
Kwani Ludovick Mwijage ni mnyama gani? Maana katika binadamu amvao Mwalimu Nyerere alikuwa na upinzani nao sijawahi kumsikia. Kimsingi tukiupa nafasi mjadala huu basi kila Mtanzania anaweza kudai kuwa aliteswa na Nyerere. Tumdharau author kama crap material.
 
Hahahahahah! Bado Nyerere alikuwa kiongozi shupavu, huwezi kuongoza nchi na kupendwa na kila mtu kama kweli huyu msimulizi angekuwa hana hatia hata kidogo faili lake lisingekuwa Ikulu kuna vitu bado naamini zaidi ya anavyosema vimepelekewa kuingizwa kwenye 18 lakini TISS noooma kweli jamaa wana mkono mrefu.
 
ndugu yangu junius unakuwa mwepesi sana wa kujudge mambo ya upande mmoja, hiyo statment au maelezo ni ya upande mmoja tu, wewe unaamini vipi kwamba huo ndio ukweli halisi
pili huyu bwana na kikundi chake inaonekana ni kikundi cha ukabila (HAYA TRIBE) na kwa asilimia kubwa kina ushirikiano mkubwa na nchi ya jirani Uganda kutokana na maelezo ya huyo bwana
TATU hakuna kiongozi au state yoyote inayoweza kusimama bila ya damu kumwagika na watu kupata mateso makuu, hata Muhamadi alipokuwa anasimamisha dini watu wengi walikufa kwa sababu tu ya kutomwamini/kutomkubali, sasa iweje unashangaa ya Nyerere, lakini hata tukimwacha Nyerere je waliomfuata walishakuwa na mambo kama hayo ya Nyerere, ndugu yangu Junius hebu angalia vifo vya utata vya KOLIMBA, KOMBE,MALIMA,BALALI , sasa hapa utamshirikisha Nyerere, wewe umecomment hii issue kwa chuki za dhairi kwa Nyerere,
kuna mambo mengi tu yanatokea na kuna watu wengi tu wanashindwa hata sasa kukanyaga Tanzania japo Nyerere keshakufa, ajali ya Mwakyembe mpaka leo ni utata mtupu, kifo cha Wangwe mpaka leo ni utata mtupu,
NNe, sio Tanzania tu ndio watu walikuwa wapo detained hiyo nni system ya dunia nzima, Moi aliua (R.Auko na wengineo), Iddi Amini alikua, Bush, Putin, na viongozi almost wote katika hii dunia
Mwisho kabisa, ni kwamba usijudge vitu kwa chuki binafsi hata kama ni kweli huyo bwana aliteswa lakini alikuwa anadeserve kwa sababu alikuwa kinyume na misingi iliyokuwa inasimamishwa wakati ule, na sio yeye tu hata Kambona alishindwa ile misingi na akaamua kutimkia UK

Nyerere si Mungu, ana udhaifu mkubwa.
 
Du!v nimemaliza kuisoma. Nyerere alikuwa na maovu yake. Halafu kuna kanisa wamependekeza jina lake lipelekwe Vatican for sainthood!
 
Nyerere was very right. sio kila mtu ataku-support kwa kila unachofanya kama kiongozi hasa wa nchi. Wale wachache wanaokuwa against na uongozi wa nchi na huenda wakawa na mipango mibaya (e.g. uhaini and the like) hiyo ndio dawa yao - na hii sio kwa Nyerere tu, wamefanya hivyo viongozi wengi duniani -Kina Mobutu, Amini, Obotte, n.k.
 
ndugu yangu junius unakuwa mwepesi sana wa kujudge mambo ya upande mmoja, hiyo statment au maelezo ni ya upande mmoja tu, wewe unaamini vipi kwamba huo ndio ukweli halisi.

Pili huyu bwana na kikundi chake inaonekana ni kikundi cha ukabila (HAYA TRIBE) na kwa asilimia kubwa kina ushirikiano mkubwa na nchi ya jirani Uganda kutokana na maelezo ya huyo bwana.

TATU hakuna kiongozi au state yoyote inayoweza kusimama bila ya damu kumwagika na watu kupata mateso makuu, hata Muhamadi alipokuwa anasimamisha dini watu wengi walikufa kwa sababu tu ya kutomwamini/kutomkubali, sasa iweje unashangaa ya Nyerere, lakini hata tukimwacha Nyerere je waliomfuata walishakuwa na mambo kama hayo ya Nyerere, ndugu yangu Junius hebu angalia vifo vya utata vya KOLIMBA, KOMBE,MALIMA,BALALI , sasa hapa utamshirikisha Nyerere, wewe umecomment hii issue kwa chuki za dhairi kwa Nyerere,

kuna mambo mengi tu yanatokea na kuna watu wengi tu wanashindwa hata sasa kukanyaga Tanzania japo Nyerere keshakufa, ajali ya Mwakyembe mpaka leo ni utata mtupu, kifo cha Wangwe mpaka leo ni utata mtupu,

NNe, sio Tanzania tu ndio watu walikuwa wapo detained hiyo nni system ya dunia nzima, Moi aliua (R.Auko na wengineo), Iddi Amini alikua, Bush, Putin, na viongozi almost wote katika hii dunia

Mwisho kabisa, ni kwamba usijudge vitu kwa chuki binafsi hata kama ni kweli huyo bwana aliteswa lakini alikuwa anadeserve kwa sababu alikuwa kinyume na misingi iliyokuwa inasimamishwa wakati ule, na sio yeye tu hata Kambona alishindwa ile misingi na akaamua kutimkia UK

Hata yesu aliwaua wasio muamini
 
It is not a fiction we are used to like those authored by African writers; Ngugi wa Thiongo, Chinua Achebe, Ole Soyinka and other you know.. not, it is real life experience;

"It was a Wednesday, December 6, 1983. A friend and I had just finished a frugal lunch in a shed next to a butchery in Mbabane, Swaziland, opposite the Swazi Observer newspaper. We had bought meat from the butchery, roasted it, and then eaten it with hard porridge. It was a popular place where people would meet for a midday meal and chat. I had just lunched with a Kenyan friend, John Cartridge, who had been in Swaziland for several days, stranded.

His version of how he ended in this predicament was not entirely coherent, though it sounded circumstantial. He said he had been working in Lesotho, another Southern African kingdom, as a motor mechanic and businessman. Cartridge even boasted of having repaired the official car of King Moshoeshoe II, the Lesotho monarch who died in 1996.

He said he was stranded because his passport had been impounded by a local hotel where he and a Malawian business associate had failed to pay their bills from a previous visit. Rumour had it that Cartridge's passport had indeed been impounded by the hotel, but only after a business deal with the hotel turned sour.

Cartridge and his partner had apparently tried to sell petrol economisers to the hotel's manager. As it turned out, the economisers proved quite useless to the manager and, according to some sources, he then decided to keep Cartridge's passport in the hope of recovering his money. Cartridge strenuously denied this claim.

Whatever the truth, it was because Cartridge's passport had been impounded that he was unable to proceed home. It was at this time that I first got to know him, through another Kenyan expatriate who was then working with Posts and Telecommunications as an accountant in Mbabane. I had come to Swaziland from Nairobi in April 1983 to seek refuge after a spate of arrests in Tanzania, my home country, in January.

Julius Nyerere's government was arresting people it accused of dissension. I considered myself unsafe in Nairobi because of the proximity of Tanzania and because of threats I had received before the Kenyan authorities transferred me to Thika Refugee Reception Centre. A benign German Catholic church minister at Thika town had given me 4200 Kenya shillings,.......(text attached)"

Hio ndio wakati pia Mzee Ngaiza akikuwa matatani? Yeah ilisemekana walishikwa kwa kutaka kuivuruga serikali lakini waliachiwa. Sasa KENYA -waliotaka kuipindua serikali ya KENYA kama Robert AUKO waliishia wapi?
 
Back
Top Bottom