Ludovic Utoh aunga mkono hoja ya kukagua deni la Taifa

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
10,561
19,056
Kuna mjadala mzuri ulikua unaendelea kwenye chanel ya UTV ambapo CAG mstaafu Bwana Ludovic Uto ameunga mkono hoja za Wabunge wanaotaka ufanyike ukaguzi kuhusu deni la taifa. Pamoja nae alikua ni Professor Ngowi na Dr Bernie.

Ludovic Uto ameenda mbali zaidi na kutaka ifanyike ukaguzi maalum(Special Audit) ili kuibua mambo kadhaa kuhusiana na deni la Taifa.

Wamesema Bunge ni vizuri likaiandikia ofisi ya CAG na kuitaka ifanye ukaguzi huo na Bunge litengeneze Hadidu za rejea maalum kwa ukaguzi huo ili kuibua mambo yote yanayotakiwa kujulikana na kuwekwa wazi kwa walipaji wa deni hilo ambao ni wananchi.

Wote wamesama kimsingi Wananchi ndio wamekasimu mamlaka ya kukopa kwa serikali na wanahaki ya kujua pesa zilizokopwa zimefanyia nini na kwa kiasi gani.

Wote wameipongeza hatua ya serikali ya awamu ya sita kwa uwazi wa kuwataarifu wananchi kua wamekopa na kuweka mchanganuo wa matumizi ya pesa hizo mpaka senti ya mwisho.

Maoni yangu ni kwamba, hatua hiyo ni muhimu na nzuri ila inabidi kuchukua tahadhari kwani kuna uwezekano wa kuleta mpasuko baina ya waungaji mkono wa serikali ya awamu ya tano na hii ya Mama Samia.
 
CAG walikuwa akina Aboud bwashee.

Kuanzia Uttoh, Assad ilikuwa ni kukomba mboga tu na kuwagombeza watoto.

Walau huyu Kichele anaonekana hana tamaa ya kujilimbikizia mali.
Unataka kusema Prof Assad alikua mtu wa tamaa za kujilimbikizia mali!!!!? Hebu ulizia historia yake kuanzia watu aliowahi kufanya nao kazi, wanafunzi wake na wote wanaomjua vyema huyu jamaa watakwambia yupo vipi kwenye suala la ethics
 
Back
Top Bottom