Mchaga 25
JF-Expert Member
- Oct 29, 2011
- 464
- 114
Katika hali isiyo ya kawaida uvunjifu wa amani umeanza kutokea wilaya ya ludewa baada ya wanakijiji kuanza kudai fedha zao ambazo walizichanga kama fedha za kianzio katika miradi ya vijiji kumi maarufu ya world bank lakini ni ADB. Utapeli huu umefanywa na kila mwansiasa aliye madarakani kuanzia......., wabunge, madiwani, wenyeviti mpaka shina. Sasa hali ni mbaya sio ludewa tu hata vijiji vingine ni baada ya serikali kushindwa kupata fedha ya kugharamia vijiji kumi na kuishia 2 au 3 ikiwa wamechukua hela za wanavijiji kuanzia 2006. Mbaya zaidi wanakijiji wanasema fedha zao zinapungua kila mwezi kwa kukatwa 8000 kama bank charges hivyo kudai bora zirudisshwe wagawiwe wale sasa ndio kitimtim kimeanzia ludewa. Chondechonde wizara ya maji toeni muongozo amani inakaribia kuvunjika wilaya zote semeni kabisa michango ya vijiji ambavyo hamta gharamia ifanyweje damu itamwagika.
Ludewa juzi FFU wamezima jaribio lakini ni kwa muda tu.
DEO filikonjombe nenda jimboni sio kukaa tu unatulia kwa kuwa madunda wamepata maji na umeme usio wa Tanesco kutoka shirika la ACRA na kuacha maeneo mengine ya jimbo watu wauane maji hakuna.