Ludewa - Ufisadi wa kutisha ujenzi wa barabara

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
MWANRI AONYA VIONGOZI LUDEWA KUWA MAKINI NA USIMAMIZI WA MIRADI

Ziara ya ghafla ya naibu waziri Mwanri kwenda kufichua ufisadi wa kutisha Lupanga kwa kukataa nyumba ya mganga iliyochakachuliwa ujenzi wake

DSCF8430.JPG
DSCF8431.JPG

Picha Kushoto:
Naibu waziri wa Tamisemi Aggrey Mwanri akiingia chini ya kalavati kuchunguza wizi wa mkandarasi alioufanya katika barabara ya Lusitu baada ya kudaiwa kujenga chini ya kiwango

Picha Kulia:

Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akimvuta naibu waziri wa Tamisemi kutoka katika mtaro baada ya kujihakikishia mwenyewe wizi uliofanywa na mkandarasi
DSCF8412.JPG
DSCF8428.JPG

Picha Kushoto:
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe aliyesimama akimtazama naibu waziri Tamisemi Mhe.Mwanri akipima urefu wa barabara iliyochakachuliwa badala ya kuwekwa upana futi 7 imewekwa 6

Picha Kulia:
Mwanri akijiandaa kuingia katika mtaro kuhakiki ujenzi wa barabara Ludewa ,ni viongozi wachache sana wanaofuatilia mambo kama hivi​

DSCF8420.JPG
DSCF8449.JPG

Picha Kushoto
Hapa akibaini uchakachuaji uliofanywa na mkandarasi katika kuibana barabara hiyo

Picha Kulia:
Ziara ya ghafla ya naibu waziri Mwanri kwenda kufichua ufisadi wa kutisha Ludewa ujenzi wa barabara na nyumba ya mganga mkuu Lupanga.

NAIBU waziri wancho ofisi ya waziri mkuu serikali za mitaa na serikali za mikoa (TAMISEMI) Aggrey Mwanri ameibua madudu ya kutisha katika miradi ya ujenzi wa nyumba na barabara za wilaya ya Ludewa mkoa mpya wa Njombe na kuonya viongozi wa Halmashauri hiyo kuwa makini na Wizi wa fedha za serikali unaofanywq katika idara ya ujenzi katika wilaya hiyo ya Ludewa.

Akizungumza na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa baada ya kukagua ujenzi wa nyumba za watumishi wa Halmashauri hiyo ,kabla ya kuwahotubia wananchi wachache katika viwanja via stendi kuu ya Ludewa,Mwanri alisema kuwa pamoja na kuwa wilaya hiyo ya Ludewa bado inakabiliwa na changamoto mbali mbali za kimaendeleo ila bado idara hiyo ya ujenzi katika Halmashauri hiyo inaongoza kwa utendaji mbovu na usimamizi mbaya wa fedha za miradi.

Mwanri ambaye leo alilazimila kuwafuata wananchi wa mji wa Ludewa stendi baada ya uwanjani ambako viongozi wa Ludewa waliandaa mkutano wake kukosa watu,alisema kuwa baada ya Kutembelea miradi ya barabara na nyumba za watumishi katika wilaya hiyo ya Ludewa alibaini kuwepo kwa uchakachuaji mkubwa wa fedha za umma.

Kwani alisema kuwa pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na mbunge wa jumbo hilo la Ludewa Deo Filikunjombe katika kulipigania jimbo hilo na wilaya ya Ludewa ili lisonge mbele kimaendeleo ila bado baadhi ya watumishi wamegeuza wilaya hiyo ni sehemu ya wao kuchuma fedha za miradi na kutumia kujineemesha wao.

Alisema kuwa pamoja kuwa Halmashauri mbali mbali zina mchwa ambao wanatafuna fedha za miradi ila kuwa Ludewa inatisha kuona nyumba na barabara zinajengwa chini ya kiwango wakati mhandisi wa wilaya yupo na anaendelea kutazama bila kuchukua hatua.

Pia alisema kuwa tatizo kubwa na mambo Kwenda holela katika wilaya hiyo hasa katika usimamizi wa miradi ya ujenzi wa miradi ni katakana na mhadisi kutokuwa makini na kushinda ofisini badala ya Kwenda kusimamia miradi hiyo.

Hat a hivyo Mwanri alisema katika ziara yake hiyo alipata Kutembelea barabara ya Lusitu ambayo alidai kuwa mkandarasi aliyejenga amejenga chino ya kiwango kutokana na kufinya mita kutoka mita 7 halali hadi mita Kati ya 6 na 5 na nusu na kuagiza mhandisi wa ujenzi katika wilaya hiyo kumtafutia BOQ na mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akimshukuru naibu waziri huyo Mwanri alisema kuwa naibu waziri huyo amekuwa ni kiongozi wa pekee wa kitaifa kufanya ziara katika wilaya hiyo katika kipindi hike cha masika na kudai. Kuwa iwapo viongozi wote wa kitaifa wataiga mfano wa Mwanri Kutembelea wilaya hiyo masika upo uwezekano wa wilaya hiyo kupiga hatua katika maendeleo.

Alisema kuwa Ziara ya Mwanri katika wilaya ya Ludewa imekuwa ya matumaini makubwa katika wilaya ya Ludewa baada ya kubaini kasoro mbali mbali katika miradi na kuwa iwapo kasoro hizo zitafanyiwa kazi wilaya ya Ludewa itapiga hatua katika maendeleo na kuwa kwa upande wake ataendelea kuwatumikia wananchi hao kwa nguvu zake zote.

Kwa hisani ya Mzee wa Matukio Daima
 
Duh, ufisadi kote kote, na huko pembezoni ndo kabisaaaa! Wakuu hawaendi huko ndo wamefanyaga shamba la malinia ati. Nikipangiwa huko ndo kwa kujifunzia ulaji mwenzangu.
 
Asante Mh Naibu Waziri, mimi nakukubali kwa jinsi unavyoibua issues. Big up pamoja na Mh Deo Filikunjombe munaonyesha mumedhamiria kuwatumikia waTanzanzania
 
Baada ya hapa ndio walienda kulima eeeh naona mwajiri wako DEO bado hajavua jezi zake.....................
 
Isije ikawa mbwembwe tu manake hayo mambo mengine ya kitaalam!! Kama kuna ufisadi isiishie kwenye picha tu za Naibu Waziri akipima upana wa barabara. Kama kuna ufisadi kweli basi wahusika wachukuliwe hatua kwqa kushiriki kuiibia serikali.

Mbona Naibu Waziri alimwagiza Mhandisi wa Ujenzi amtafutie BOQ na Mkataba kwani wakati anapima barabara alikuwa ana base wapi kama hakuwa na BOQ na Mkataba. Mimi nitaamini tu pale ambapo nitasikia mhandisi wa ujenzi amechukuliwa hatua kwa kushiriki katika wizi.
 
Binafsi nampongeza huyu Mwanri kwa kazi nzuri. Naona wamekutana vizuri na Mbunge wa Ludewa Deo haule aliyejitahidi kufichua hayo na Naibu waziri kufanya ile mbinu ya hayati Sokoine mpango mzima ulisukwa maana wangejulishwa viongozi waandamizi wilayani wangvuruga mipango na kutoa visingizio vyao. Kwa utaratibu huu viongozi wahusika mambo yanawawia magumu sasa hakuna pa kushika kwani matawi yote huteleza siku ya kifo cha nyani. Haya fidadi mkuu mhusika yuko taabani hospitalini sasa.
 
DSCF8430.JPG
DSCF8428.JPG

Naibu waziri wa Tamisemi Aggrey Mwanri akiingia chini ya kalavati kuchunguza wizi wa mkandarasi alioufanya katika barabara ya Lusitu baada ya kudaiwa kujenga chini ya kiwango

Jamaa kiboko yao, waziri anaingia huko shimoni kukagua ujenzi wa barabara? nilifikiri wanaoingia shimoni huko ni wanaozidiwa ujanja kama lile jabali la Libya, Sijua kapata wapi ubavu huyu? Hivi huyu waziri ni mbunge wa jimbo gani vile?
 
Isije ikawa mbwembwe tu manake hayo mambo mengine ya kitaalam!! Kama kuna ufisadi isiishie kwenye picha tu za Naibu Waziri akipima upana wa barabara. Kama kuna ufisadi kweli basi wahusika wachukuliwe hatua kwqa kushiriki kuiibia serikali.

Mbona Naibu Waziri alimwagiza Mhandisi wa Ujenzi amtafutie BOQ na Mkataba kwani wakati anapima barabara alikuwa ana base wapi kama hakuwa na BOQ na Mkataba. Mimi nitaamini tu pale ambapo nitasikia mhandisi wa ujenzi amechukuliwa hatua kwa kushiriki katika wizi.

Magufuli yuko wapi? Huyu Mwanri anakaimu nafasi ya Mwakiembe? Ukaguzi wa ujenzi wa barabara uko chini ya ofisi ya waziri mkuu au wizara ya ujenzi?
 
Mbwembwe zote za huyu waziri hajawahi kufanikisha kutimua hata mtumishi mmoja mwizi, ni geresha tu.
 
Isije ikawa mbwembwe tu manake hayo mambo mengine ya kitaalam!! Kama kuna ufisadi isiishie kwenye picha tu za Naibu Waziri akipima upana wa barabara. Kama kuna ufisadi kweli basi wahusika wachukuliwe hatua kwqa kushiriki kuiibia serikali.

Mbona Naibu Waziri alimwagiza Mhandisi wa Ujenzi amtafutie BOQ na Mkataba kwani wakati anapima barabara alikuwa ana base wapi kama hakuwa na BOQ na Mkataba. Mimi nitaamini tu pale ambapo nitasikia mhandisi wa ujenzi amechukuliwa hatua kwa kushiriki katika wizi.

Kuna kitu umekisema hapo. Inatakiwa tufafanuliwe vizuri. Hao ma injinia huwa wanasema quantities zilizoko kwenye boq ni estimates na kwa maana hiyo kama ni mkandarasi atalipwa kutokana na actual quantities alizofanya. Hii kitu inaitwa measure and re-measure ili hatimaye ipatikane kitu iitwayo as built drawing. Binafsi sijajua ufisadi hapo ni nini. Tupewe details ili tuchangie vizuri.
 
Magufuli yuko wapi? Huyu Mwanri anakaimu nafasi ya Mwakiembe? Ukaguzi wa ujenzi wa barabara uko chini ya ofisi ya waziri mkuu au wizara ya ujenzi?

Mkuu kuwa makini, TAMISEMI na kwa maana ya halmashauri zina ujenzi wa barabara na mwanri ana wajibu wa kuzikagua. Fuatilia vizuri.
 
.

Umenifurahisa sana Mh. Naibu Mwanri, Big Up sana. Nimesikia unaratiba ya kukagua miradi ya Mikoa yote miwili ya Njombe na Iringa. Ni matumaini yangu utaibu mengi katika miradi mikubwa yote ya wilayani. Mzeeeeeee usikubaliane na ratiba waliyokupangia, watakuwa wamechangua miradi mizuri mitu ambayo haina changamoto kama za huko Ludewa. Nashauri uwe unapiga Suprize za ukweli, kama umedhamiria utaona mengu zaidi ya hayo. Pitia miradi kama ya ujenzi wa machinjio Njombe, masoko ya mazao, maghara, miradi ya umwagiliaji, nyumba za watumishio wako, mifuko ya pembejeo, mifuko ya elimu, nk...........!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!. NAKUAMBIA UTASHANGAAAAAAA HADI BASI, naamini umetumwa na MUNGU Mwenye. Kwa kweli nitakuleta hadi Huku niliko uone kazi zaidi................................ Big Uppppppppp
 
Mwanri anapeleka ualimu wake wa Kivukoni kwenye ujenzi wa barabara? Hajui hafui dafu katika nchi hii ambayo
imekubuhu kwa ufisadi.

Pengine ndiyo namna ya kupata masurufu ya safari.
 
.

Umenifurahisa sana Mh. Naibu Mwanri, Big Up sana. Nimesikia unaratiba ya kukagua miradi ya Mikoa yote miwili ya Njombe na Iringa. Ni matumaini yangu utaibu mengi katika miradi mikubwa yote ya wilayani. Mzeeeeeee usikubaliane na ratiba waliyokupangia, watakuwa wamechangua miradi mizuri mitu ambayo haina changamoto kama za huko Ludewa. Nashauri uwe unapiga Suprize za ukweli, kama umedhamiria utaona mengu zaidi ya hayo. Pitia miradi kama ya ujenzi wa machinjio Njombe, masoko ya mazao, maghara, miradi ya umwagiliaji, nyumba za watumishio wako, mifuko ya pembejeo, mifuko ya elimu, nk...........!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!. NAKUAMBIA UTASHANGAAAAAAA HADI BASI, naamini umetumwa na MUNGU Mwenye. Kwa kweli nitakuleta hadi Huku niliko uone kazi zaidi................................ Big Uppppppppp

Damu ya Sokoine, maana Sokoine alikuwa na kawaida ya kuvizia ofisini, viongozi wazembe walipata matumbo moto. Ukichelewa kufika ofisini utakuwa kiti kimeondolewa, maana yake uende kujieleza kwake kulikoni, hapo ndipo mtu anapopata kigugumizi cha ghafla.
 
Magufuli yuko wapi? Huyu Mwanri anakaimu nafasi ya Mwakiembe? Ukaguzi wa ujenzi wa barabara uko chini ya ofisi ya waziri mkuu au wizara ya ujenzi?

Kunahitajika kufanyika utaratibu wa kufumua mifumo iliyopo kwani inaingiliana sana katika utendaji, ndio maana wakati mwingine mambo hayaendi kwa sababu ya kuwekeana viporo kila mmoja kuona anayehusika mwingine, na pengine kutokea migongano ya kiutendaji. Kwa nini ujenzi wa barabara usiwe moja kwa moja chini ya wizara ya ujenzi, maana kutenganisha bajeti hizi husababisha matumizi makubwa zaidi ambayo yanaweza kukwepeka. Nyumba za watumishi ni sawa, lakini hili la ujenzi wa barabara?
 
Mkuu kuwa makini, TAMISEMI na kwa maana ya halmashauri zina ujenzi wa barabara na mwanri ana wajibu wa kuzikagua. Fuatilia vizuri.

Mimi nilifikiri Wizara ya ujenzi iko kote kote, ni mipaka ipi ya wizara ya ujenzi na halmashauri? Hizo idara za ujenzi za halmashauri haziko ndani ya wizara ya ujenzi? Hospitali nazo haziko kwenye wizara ya afya kwa vile ziko chini ya halmashauri? Wanatukoroga hawa.
 
Back
Top Bottom